Hii sijui ni dharau, kukomoana au ulimbukeni

Hii sijui ni dharau, kukomoana au ulimbukeni

tatizo baadhi yetu wanaume tunapenda sana viporo. Kula kitu kipya anza nacho mwenyew ....

Sasa huyu bwana kakimbilia kula kiporo kilichoachwa na wenzake ameanza kuharisha anakuja kuomba msaada kwetu...

kitu kipya kipi mkuu kwa dunia ya sasa labda umuwah aliemaliza drs la 7 au hujasoma yule aliechwa dar toka mbeya na binti wa miaka 22? hakuna la afadhali mkuu.
 
Kwako kunaungua kwa mwenzio kunateketea, hili sekeseke la aina yk, kazi kweli kweli
idd njema kama unasherekea...

Moja kwa moja kwenye lengo..
Rafiki yangu kapata demu, of course ni mwanamke aliemzidi kwa takribani miaka 4, mshkaji ana 27 na mdada ana 31... Sio shida kwake hilo..
Mshkaji aliamini kuwa huyo bidada kwa umri aliokuwa nao na experience ya kuumizwa labda angekuwa demu mwema (huyo mtoto alizaa na mume wa mtu ambae hakuwahi kumwambia kama ameoa. Jamaa alikuwa amemwacha mkewe kijijini yy akaenda dar kutafuta maisha) dada wa watu kuja kugundua kuwa baba wa mwanae ni mume wa mtu tayr mwanae ana miaka 3.
Kwa maana hiyo ukijumlisha na mahusiano mengine aliyopitia kuanzia akiwa mdogo mpaka umri huo jamaa yangu akajua demu atakuwa makini sana..

Matatizo yakaanza;
mara baada ya miezi minne tu demu ameonekana kuwa dependant sana kwa jamaa, asipotuma vocha asubuhi hata salamu hapati.. Akiuliza kulikoni anadai simu haikuwa na salio (ni kila siku)
na anafanya kazi yenye mshahara mzuri tu..

Akituma vocha watachati tu.. Hapigiwi..

Demu mtu mzima kila siku matatizo, leo naumwa kichwa, leo kifua, mara nina hamu ya kitimoto, sijanywa wine siku nyingi n.k..

Amemfundisha huyo mwanae kuwa huyo jamaa ni mjomba wake.. (kwa hiyo dogo anamwita mume wa mamaake mjomba)

akikuta simu ya jamaa iko busy watagombana... Hata kama alikuwa anaongea na mamaake.

Anamshawishi sana msela achukue mikopo bank na hawana plani yoyote ya biashara..

Sasa kwa style hii huyu dada akiachwa na huyu akafikisha miaka 50 atasema ana mkosi?
 
Kuikweli kuna baadhi ya wanawake hawajiyambui.
 
Kwani umesahau "Penzi kitovu cha uzembe"? ngoswe na mazoea by Zaina mwanga
Tatizo huwa mnawaonea huruma kuwaacha. Dalili kama hizi ni wazi penzi limeota kidonda. Usipokitibu mapema, daktari atakufa ukose tiba.
^^
 
huyo aliwachukia wanaume toka siku aliyotendwa..SASA BASI AINA HIYO YA WATU HUWEKA KISASI CHA KUMKOMOA MWANAUME YEYOTE ATAKAYEJAA ANGA ZAKE.. hii psychologically huona kama ni relief kwao especially anapogundua mwanaume anaweweseka because of her
 
Wanawake/wanaume waliotendwa hawafai kuwa wapenzi...
Hapo ukute alitumika sana na yeye kaamua kutumia...
 
Hapa kwanza nahisi maelezo aliyopewa juu ya mzazi wa mtoto siyo ya ukweli. Inaezekana hawakuachana kwa sababu ya kugundua jamaa ana mke. 3 years mke asije kumtembelea? Hana watoto.. Mke asipige hata simu especially usiku kulinda ndoa three years? No way. Jamaa yako alikosea toka mwanzo. Alichokiamini sio story kamili. Ajipange upya! Asije kua anatumiwa kipindi cha mpito bidada akiwa anaangalia mwelekeo mpya.
 
wala huyo kaka asimwache kwanza watu wakiumizwa wanabadilisha mtazamo sana juu ya wanaume yawezekana huyo baba mtoto alikuwa anampigia simu tu fresh alivyotendwa akaona mwanaume hata ukiwa unampigia mwisho ni kuumizwa hvyo azungumze naye kisaikolojia zaidi yawrza kuisha

Kisa alitendwa kule hasira aje amalizie kwangu???
 
Kikosi cha mizinga nyimbo ya songa inahusika sana hapa
Kikosi cha mizinga ringa na mabosi wako wanakinga kutoka kwa wadosi na wasinga singa, 18 anazotinga hazienei, naipenda sana ile nyimbo mkuu
 
JF ...never boring...

Huyu alikuwa kimada tu...hakuna cha sikujua wala nini...3 good years hujui kama mtu ana mke na watoto mkoani...

Kumbe we ndo mhusika. Si ungesema toka mwanzo? Pengine kuna ambao wangechangia tofauti
 
JF ...never boring...

Huyu alikuwa kimada tu...hakuna cha sikujua wala nini...3 good years hujui kama mtu ana mke na watoto mkoani...

wewe inawezekana kabisa kuna watu amemtreat mke wake hata akiongea naye utajua ni msela wa kawaida tena kama mke kaachwa kijijin anapigiwa simu kila baada hata ya week na maongezi ni shoty sana hamuulizi watoto wangu wanaendeleaje anataja kwa majina john vip?, janeth. bibi yao? haya jaman wasalimie wote
 
mdada hajiamini huyo teh teh sijui nisemeje
 
Back
Top Bottom