Hii Shule ni Nzuri sana! Nimeipenda

Hii Shule ni Nzuri sana! Nimeipenda

bashiru1

Member
Joined
Nov 10, 2013
Posts
38
Reaction score
1
Wakuu imebidi nije niwashirikishe hapa.

Kuna shule moja hapa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro inaitwa Patmos Secondary School..

Nimevutiwa na mengi sana kwenye hii shule inayochipukia kwa kasi sana.
Ilikuwa siku ya Jumapili wakati niko na wadau flani kuelekea Chemka! Chemka ni sehemu yenye hot spring.
Wakati tunaelekea ndio tukakiona kibao cha hii shule ya sekondari ninayoisema hapa.

Maeneo ya shule siyo mazuri sana, ni changa! ila utashi na uwezo wa wanafunzi ndiyo ulitufurahisha sana, wana nidhamu ya hali ya juu na ukarimu uliotukuka.

Tuliyajua haya baada ya kusema na wachache, pia ni shule (naamini) yenye wanafunzi wenye uwezo mkubwa katika kuimba na kuabudu kuliko shule yeyote ile kwa Mkoa huu wa Kilimanjaro.

Uzuri na nidhamu ya wanafunzi ilitufanya jumatatu iliyofuata kutafuta records zake kitaaluma,

Tulikutana na Mwalimu wa taaluma aliyetuonyesha recently records, kwa kidato cha pili
Kwa mwaka huu na mwaka jana.
Ambapo mwaka jana Walishika nafasi ya 6 kati ya shule 40 zilizoshiriki mtihani wa taifa
Na kuna kijana aliyepata 99% kwenye hisabati.

Mwaka huu kwenye mtihani wa Mock wilaya walishika tena nafasi ya 5 kati ya shule 39 zilizofanya Mtihani huo..

Niliipenda sana hii shule hasa kwenye malezi yao ya kiroho na jinsi wanavyomaintain nidhamu kwa wanafunzi.

Regardless mazingira yao kuwa machanga still they can run beyond many Old Schools in Kilimanjaro.

Viva Patmos!!
Hapa ni mahali salama kwa watoto wetu kupata elimu bora.
Mdogo wangu sasa kapata shule..
 
mkuu mapya yaja sina hata hisa kwenye hii shule, wamiliki wake hata hawanifahamu..
 
Umetumia vigezo gani kusema ni bora kuliko zingine
 
Asante kwa taarifa nzuri. Je ni O Level tu au hadi A level
 
Me natafuta A level kwa masomo ya arts. Pls. Wadau nisaidieni ni shule ipi nzuri kimaadili na kielimu
Natanguliza shukrani
 
Wakuu imebidi nije niwashirikishe hapa.

Kuna shule moja hapa Wilaya ya Hai Mkoa wa Kilimanjaro inaitwa Patmos Secondary School..

Nimevutiwa na mengi sana kwenye hii shule inayochipukia kwa kasi sana.
Ilikuwa siku ya Jumapili wakati niko na wadau flani kuelekea Chemka! Chemka ni sehemu yenye hot spring.
Wakati tunaelekea ndio tukakiona kibao cha hii shule ya sekondari ninayoisema hapa.

Maeneo ya shule siyo mazuri sana, ni changa! ila utashi na uwezo wa wanafunzi ndiyo ulitufurahisha sana, wana nidhamu ya hali ya juu na ukarimu uliotukuka.

Tuliyajua haya baada ya kusema na wachache, pia ni shule (naamini) yenye wanafunzi wenye uwezo mkubwa katika kuimba na kuabudu kuliko shule yeyote ile kwa Mkoa huu wa Kilimanjaro.

Uzuri na nidhamu ya wanafunzi ilitufanya jumatatu iliyofuata kutafuta records zake kitaaluma,

Tulikutana na Mwalimu wa taaluma aliyetuonyesha recently records, kwa kidato cha pili
Kwa mwaka huu na mwaka jana.
Ambapo mwaka jana Walishika nafasi ya 6 kati ya shule 40 zilizoshiriki mtihani wa taifa
Na kuna kijana aliyepata 99% kwenye hisabati.

Mwaka huu kwenye mtihani wa Mock wilaya walishika tena nafasi ya 5 kati ya shule 39 zilizofanya Mtihani huo..

Niliipenda sana hii shule hasa kwenye malezi yao ya kiroho na jinsi wanavyomaintain nidhamu kwa wanafunzi.

Regardless mazingira yao kuwa machanga still they can run beyond many Old Schools in Kilimanjaro.

Viva Patmos!!
Hapa ni mahali salama kwa watoto wetu kupata elimu bora.
Mdogo wangu sasa kapata shule..

Asante afisa masoko Wa shule.umejitahidi kufanya promo nzuri
 
wamekulipa shilling ngapi kuwapigia promo mkuu
 
Promo safi ya kijanja, ila kwa taarifa tu mtihani wa Kidato cha Pili sio wa Taifa (isipokuwa kuanzia mwaka huu) na kuna shule zaidi ya 40 (kitaifa) unless ulimaanisha kimkoa (hata hapo nadhani zipo zaidi)
 
Umetumia vigezo gani kusema ni bora kuliko zingine

mimi ni mkazi wa kilimnjaro nimeishi wilaya zote za Kilimanjaro nimefanya kazi na mashirika yasiyo ya kiserikali mojawapo ni YES.
 
Promo safi ya kijanja, ila kwa taarifa tu mtihani wa Kidato cha Pili sio wa Taifa (isipokuwa kuanzia mwaka huu) na kuna shule zaidi ya 40 (kitaifa) unless ulimaanisha kimkoa (hata hapo nadhani zipo zaidi)

nimetaja kimkoa mkuu.
mkoa wa Kilimanjaro.
 
Hivi mods hakuna ada ya matangazo....?????

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
kweli wewe mchaga! si bora thread yako ungepeleka jukwaa la matangazo madogo madogo
 
Back
Top Bottom