Hiyo nyumba itabaki kuwa yakwenu wote kama mliipata ndani ya ndoa (kwa mujibu wa sheria) hata kama jina linasomeka lake. Jambo alilolifanya mkeo sio jema na nahisi alikuwa anajenga kwa siri ili wewe usijue ila kuna watu wamemshauri kuwa anachokifanya si kizuri kwa ndoa yenu ndio maana amehamua kukufanyia zuga kama ya surprise ili aweke mambo sawa. Kwa ufupi anarekebisha alipokosea.
Kimaandiko na kiasili mwanaume ndio kichwa cha familia na iwapo vitu ambavyo vilipaswa kufanya kwa uongozi wa m/ume vikafanywa na m/mke uwa inaleta makwazo ya kisaikolojia na kukufanya ujihisi chini sana (inferiority complex)
Wanachoshauri wengine kuwa hiyo nyumba muipangishe na mjenge nyingine wako sahihi sana ili kukuweka huru kisaikolojia, lakini pia unaweza hata kuhamia kwenye hiyo nyumba ila kichwani mwako jipange kujenga yenu ya pamoja kwa kumshirikisha. Usimwambie mkeo kuwa kuna kitu unafikiria kuhusu hiyo nyumba aliyojenga lakini unaweza ukamsaidia kwa moyo mmoja kuimalizia kisha ukamwambia mjenge nyingine ambayo akikisha unachora ramani nzuri na ya kisasa kuliko hiyo ya surprise na baadae kumshauri mhamie huko.
Ndoa ni ushirikiano na dini zinasema mnapooana mnakuwa mwili mmoja hivyo mwenzako kukuficha kitu kama hicho tayari ni walakini ila libebe hilo kwa akili na ujiongeze ila kama nilivyosema mwanzo kukuonyesha hiyo nyumba ni kwamba amejirudi mwenyewe kwa kosa alilolifanya hivyo wewe nje chukulia kama ni kitu kizuri alichokufanyia ila moyoni na akilini fanyia kazi kuhusu kujenga nyumba nyingine nzuri Zaidi.
Nimeongea mengi sana ingawa story yako inaonekana kama chai ila nadhani yatawasaidia wengine wenye matatizo yanayoshabihiana na ili.
Wenu Funzadume