Kaboom
JF-Expert Member
- Nov 6, 2011
- 10,828
- 14,996
Salaam Wapendwa
Mi bado ni mgeni kwenye hii taasisi ya Ndoa..Japo kuna changamoto za hapa na pale ila Nashukuru Mungu bado hazijanizidi uwezo..Ila hii ya Juzi imenifikirisha kidogo.
Mi na wife tunashauriana,Shirikishana na kupanga mengi kwa Pamoja..Juzi kanichukua na kunipeleka maeneo ya Bunju kwa madai ya kwamba kuna sapraizi anataka kunifanyia..Nikajua uenda amenunua shamba anataka kunionyesha Au alishalima anataka kunionyesha maendeleo ya mazao yake..Mana kuna kipindi stori za kilimo zilikuwa hazikauki ndani ya nyumba..
Kinyume na mawazo yangu..Baada ya kufunguliwa kitambaa usoni Nakutana na Nyumba ambayo hiko kwenye hatua za Mwisho kabisa Kukamilika..Nikashikwa na Bumbuwazi baada ya kuniambia ni nyumba yetu..
Sina wasiwasi kwamba atakuwa kajenga kwa nguvu zake..Ila najiuliza mbona hajawahi kunishirikisha wala kugusia hili swala..Nilipomuuliza akaniambia hakutaka kunishirikisha kwa sababu alitaka iwe sapraizi...Hii ni sawa kweli kwa wanandoa??..
Embu naombeni mawazo yenu ya chap chap kabla na mi sijaamua kumuanzishia sapraizi mfululizo