Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,192
- 680
juzi kati nilikuwa na jamaa yangu mmoja akanihadithia mkasa wa kweli ambao nilicheka sana, na nnaona ni jambo jema kizuri kula na wenzio. sasa wacha niimwage hapa
anasema kuna jamaaa mmoja alitembelewa na baba toka kijijini kwao hapo kwake da re salam, sasa alikaa kama wiki moja, siku ya baba kurudi kijijini, mtoto alimchukua baba yake na kupita nae kwenye ATM machine na kutoa kama laki tatu na kumkabidhi baba kwa ajili ya nauli na matumizi kule kijijini, kisha akampeleka Ubungo kwa safari
kama baada ya siku mbili, akapokea simu kutoka kwa Baba Mdogo akitaka amtumie kama shilingi laki mbili, jamaa akamtumia. kama siku tatu hivi shangazi nae akataka atumiwe mapeni. na kila siku zikienda waombaji wanaongezeka na wanaomba dau kubwa.
mtoto akampigia simu mama yake kumsikitikia kuhusu hio tabia iliozuka, mama akamwambia mwanawe kuwa yote hayo baba yako huyo, amewaambia watu wewe mjini uko na kibanda cha pesa unaenda kuchukua tu