ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 24,792
- 60,618
Siku hizi ukikutana na kijana ana laptop, ring light na simu nzuri usidhani ni IT specialist… mwingine anakesha usiku kucha akihariri video ya sekunde 45 huku background kuna motivational music na caption “never give up”.
Lakini ukiangalia reality ya game yenyewe unaweza ukaanza kujiuliza… hivi hawa vijana wanatafuta mafanikio au wanatafuta stress za bure?
Kuna vijana wanatumia muda mwingi kupanga maudhui:
leo prank, kesho podcast, kesho kutwa street interview, mara “day in my life”, mara “nilitumia siku nzima bila kula”.
Views zinaingia, followers wanaongezeka, comments moto… lakini mwisho wa mwezi account inasoma elfu 78.
Meta monetization kwa sasa imekuwa kama bahati nasibu.
Unaweza kuwa na followers laki tano lakini hela inaingia kama nauli ya kwenda Mbezi.
Unakuta content creator ana jina kubwa, anajulikana kila kona, lakini deal anayopata ni kutangaza duka la viatu Sinza, mgahawa Mwenge au perfume za Kariakoo huku akipewa laki mbili na soda mbili za bure.
Wakati huo huo kuna kijana mwingine hata hana Instagram yenye picha tano.
Yupo Manyara huko anachimba, analima vitunguu, viazi, maharage, hoho… msimu ukifika anapiga million 10 kimya kimya bila kujua hata algorithm ni nini.
Mmoja anahangaika:
“Jamani tusaidiane kufikisha views laki moja.”
Mwenzake yupo shambani:
“Mvua ikinyesha wiki hii naongeza ekari mbili.”
Hii haimaanishi content creation haina future. Hapana.
Ila vijana wengi wameingia wakiamini kila mwenye followers ni tajiri. Kumbe wengine wanaishi kwa pressure ya kuonekana wana maisha mazuri kuliko walivyo nayo kweli.
Mwingine anakodisha gari kwa saa mbili apige content ya “hard work pays”.
Lakini mkulima wa nyanya ndio analipa cash gari lote.
Tatizo kubwa ni kwamba vijana wengi wanafuata trend kuliko uhalisia wa maisha.
Kila mtu anataka kuwa influencer, lakini hakuna anayetaka kuwa producer wa chakula ambacho hao influencers wanakula.
Mwisho wa siku unaweza kucheka ukagundua:
Yule anayehangaika kutafuta likes mjini, anaweza kuwa maskini kuliko yule anayehangaika na mbolea kijijini.