Hii ni laana au kuna mkono wa mtu

Hii ni laana au kuna mkono wa mtu

Inaendelea...............
Basi baada ya mtoto wa pili, taratibu za ndoa zikaanza baada ya yeye kurudi toka Dar alikoenda kusalimia na kupeleka mtoto.

Na kama nilivyowadokeza wazazi wake hawakuwa radhi basi ikabidi mipango ifanyike kwa Babu na Bibi yake.

Ila kila mkipanga linatokea tatizo ambalo mtafanya muhairishe kwa mwaka husika.

Mara ya kwanza aliumwa baba yangu mkubwa mpaka akafariki ikabidi tuhairishe.

Mara ya pili aliumwa Mama yangu mzazi, chuou chupu kumpoteza.

Hatimaye ndoa ikafungwa kwa mara ya tatu ambapo wazazi wake hawakuhudhuria ila ikapita pita kibingwa na zawadi zao walipelekewa huko huko majumbani.

Baada ya Ndoa

Kupita ndani ya ule mwezi anafaliki baba yangu, tunaenda kumfanyia postmortem tunaambiwa ni pressure.

Mwaka 2021 napata ajali mbaya ya gari maeneo ya igawa mkoa wa Mbeya hivyo kupelekea kupata madhala zaidi maeneo ya mgongoni na kiunoni?
Mpaka kusafirishwa kuletwa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Nilitibiwa kwa muda wa miezi Saba, tumshukuru Mungu Leo naweza kutembea, nisisahau na hili kipindi chote hicho familia ya mke wangu hawakuwahi kuja kunitembelea hospitali Wala kunijulia hari kwenye simu?
Ni binti pekee na ndugu zangu ndio wanahangaika.

Uhamisho wa ajabu ajabu kwenda maporini zaidi toka mjini?

Vifo vya Babu yangu na bibi yangu ndani ya vipindi vifupi vinavyofuatana?

Jamani haya mambo ni Laana ya asili au Kuna mkono wa mtu?
Maana Kuna matukio mengi yananiandama mengine sijayaandika mpaka ya kukimbizwa na Nyuki

Mwisho
 
Hakuna laanaa bali ndivyo dunia ilivyo, si kila siku uwe Mtu wa furaha tu bali zipo nyakati za huzuni.

Soma BIBLIA "MUHUBIRI 3:1-15."
 
aliyemuelewa mleta uzi namna alivyoeleza kwenye paragraph ya pili kutoka mwisho, naomba anieleweshe na mimi.
giphy.gif
Ana rips nzuri kweli aisee
 
Nilioa mnamo mwishoni mwa 2020 kwa ndoa ya kulazimisha.
Kifupi ndoa hii haikuidhinishwa kwa moyo mmoja na wazazi wake,
isipokuwa Babu yake na bibi yake ndio waliisimamia kidete, na kunisapoti nimuoe mjukuu wao.

Wazazi wake waliapa kuwa hawatoshiriki kwenye hii ndoa, hivyo ikabidi ifungwe nyumbani kwa Babu yake.

Sherehe kubwa ilifanyika kwao na kwetu, kabla ya kuelekea ukumbini siku ya jumapili ila wazazi wake hawakuhudhuria zaidi ya bibi na babu yake na ndugu wengine.

Mtu niliyemuoa hakuwa mpya kwenye maisha yangu, kwani nilianza nae mahusiano nikiwa kidato Cha sita wakati yeye akiwa form III.

Hivyo mwaka 2012 wakati yupo kidato Cha nne, alijigundua ni mjamzito kipindi wanajiandaa na mtihani wa Taifa.

Akaja kwangu akiomba pesa atoe, nami nikamkatalia nikimwambia akitoa ajue Mapenzi yetu yameishia hapo, ila kabinti kakang'ang'ania Kutoa hivyo kuachana bila kukubaliana.

Mimi nilikuwa kwenye kipindi Cha kujiandaa ili nikajiunge chuo kcmc Kilimanjaro.
Ila baada ya Ile Taarifa ikabidi nikamshirikishe baba yangu mzazi anipe ABC nini Cha kufanya.

Mzee akanambia tunabadilisha program Yale masuala ya chuo weka kando, nenda kajiunge kule kunakoogopwa na wengi, ili uweze kumlea mwanao halafu baada ya miaka mitatu nitakufanyia mpango uludi chuo.

Hivyo basi kupotea mtaani ila kosa nililofanya kutomuaga bibie na Mimi kutojuwa msimamo wake kama atatoa au atalea.
Huu uzi umejipost mana ujafika mwisho
 
Inaendelea.................
Kifupi nikapat taarifa tena, yule jamaa kapeleka barua ya posa hivyo inasubiriwa kujibiwa?

Mimi nilichokifanya ni kusafiri usiku usiku, kutoka mkoani kumbuka ni zaidi ya kilomita 950 mpaka dar,
Yule mzazi wake wa kike akawa anatamba mtaani kwamba Binti yake hawezi kuolewa na familia ya watu wagumu, kwa sababu yeye ni mzaramo.

Yule jamaa ni mtu wa Tanga aliyetoa posa lakini kubwa kuliko akaapa hata wafanyeje mtoto wao ataolewa na huyo.

Nilivyofika dar, Moja kwa Moja home, huku nikijiuliza nichukue atua gani?
Nibebe Mwanangu maana niliapa mtoto wangu hawezi kulelewa na baba wa kambo nikiwa hai au nibebe mama mtu ili kukata ngebe za yule bi mkubwa?

Naomba ifahamike mpaka muda huo, hizi familia hazipikiki chungu kimoja ila binti hakuwa na shida binafsi ila mama yake mswahili kinyama.

Yule jamaa huduma kazidisha na kazi yake ni mjeda sometime anakuja na gwanda zake kitaa.
Vijana mtaani wakawa wanamwogopa fulani hivi ila nikasema huyu hanijui Mimi sio Mandonga [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38].

Nikampigia simu mama mtoto nikimtaka kesho tuonane, hivyo aje nyumbani huku akiwa na sauti ya kiuoga uoga akidhani nimeshagundua Janja yao.

Binti akafika kesho yake, tukajadili ishu ya yeye kutolewa posa, kakajitetea mama yake ndio kalazimisha na mahari ishatolewa, sijui naeleweka?

Yaani wakati Wana hisi mtaa kumbe tayari, hapo ni mchumba wa mtu, halafu katoto kangu kanamwita anko.

Nilichomwambia kesho tunaondoka wote na Leo hapa nyumbani hutoki, mwache baba yako aje?….....…
Ngoja kwanza ! Kwani we mandonga umemjua lini na story ni ya lini .
 
Chukua wanao wakiwakatalia WAAACHIE

Wakiwa wakubwa watakufuata tu
 
Wewe si mgumu Sasa unalialia Nini, nani alikwambia laana inawapata wagumu mabaunsa majakicheni, komaaa tu hivyo hivyo bana. Uliona wapi swazniga analia ?
 
Inaendelea...............
Basi baada ya mtoto wa pili, taratibu za ndoa zikaanza baada ya yeye kurudi toka Dar alikoenda kusalimia na kupeleka mtoto.

Na kama nilivyowadokeza wazazi wake hawakuwa radhi basi ikabidi mipango ifanyike kwa Babu na Bibi yake.

Ila kila mkipanga linatokea tatizo ambalo mtafanya muhairishe kwa mwaka husika.

Mara ya kwanza aliumwa baba yangu mkubwa mpaka akafariki ikabidi tuhairishe.

Mara ya pili aliumwa Mama yangu mzazi, chuou chupu kumpoteza.

Hatimaye ndoa ikafungwa kwa mara ya tatu ambapo wazazi wake hawakuhudhuria ila ikapita pita kibingwa na zawadi zao walipelekewa huko huko majumbani.

Baada ya Ndoa

Kupita ndani ya ule mwezi anafaliki baba yangu, tunaenda kumfanyia postmortem tunaambiwa ni pressure.

Mwaka 2021 napata ajali mbaya ya gari maeneo ya igawa mkoa wa Mbeya hivyo kupelekea kupata madhala zaidi maeneo ya mgongoni na kiunoni?
Mpaka kusafirishwa kuletwa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Nilitibiwa kwa muda wa miezi Saba, tumshukuru Mungu Leo naweza kutembea, nisisahau na hili kipindi chote hicho familia ya mke wangu hawakuwahi kuja kunitembelea hospitali Wala kunijulia hari kwenye simu?
Ni binti pekee na ndugu zangu ndio wanahangaika.

Uhamisho wa ajabu ajabu kwenda maporini zaidi toka mjini?

Vifo vya Babu yangu na bibi yangu ndani ya vipindi vifupi vinavyofuatana?

Jamani haya mambo ni Laana ya asili au Kuna mkono wa mtu?
Maana Kuna matukio mengi yananiandama mengine sijayaandika mpaka ya kukimbizwa na Nyuki

Mwisho
Mwanajeshi kachomoa betri hyo wengine hawapendi ujinga haya mambo haya unaweza ukapigwa misumari mpaka ukakimbia huko kusikojulikana.
 
Wewe si mgumu Sasa unalialia Nini, nani alikwambia laana inawapata wagumu mabaunsa majakicheni, komaaa tu hivyo hivyo bana. Uliona wapi swazniga analia ?
Issue najiuliza haya mambo ni asili au mkono wa mtu?
 
Mwanajeshi kachomoa betri hyo wengine hawapendi ujinga haya mambo haya unaweza ukapigwa misumari mpaka ukakimbia huko kusikojulikana.
Hapo tulikuwa tunatunishiana misuli ila haya mambo yananielemea
 
Back
Top Bottom