Hii ni laana au kuna mkono wa mtu

Hii ni laana au kuna mkono wa mtu

MWANAHARAMU

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
5,171
Reaction score
13,231
Nilioa mnamo mwishoni mwa 2020 kwa ndoa ya kulazimisha.

Kifupi ndoa hii haikuidhinishwa kwa moyo mmoja na wazazi wake,
isipokuwa Babu yake na bibi yake ndio waliisimamia kidete, na kunisapoti nimuoe mjukuu wao.

Wazazi wake waliapa kuwa hawatoshiriki kwenye hii ndoa, hivyo ikabidi ifungwe nyumbani kwa Babu yake.

Sherehe kubwa ilifanyika kwao na kwetu, kabla ya kuelekea ukumbini siku ya jumapili ila wazazi wake hawakuhudhuria zaidi ya bibi na babu yake na ndugu wengine.

Mtu niliyemuoa hakuwa mpya kwenye maisha yangu, kwani nilianza nae mahusiano nikiwa kidato Cha sita wakati yeye akiwa form III.

Hivyo mwaka 2012 wakati yupo kidato Cha nne, alijigundua ni mjamzito kipindi wanajiandaa na mtihani wa Taifa.

Akaja kwangu akiomba pesa atoe, nami nikamkatalia nikimwambia akitoa ajue Mapenzi yetu yameishia hapo, ila kabinti kakang'ang'ania Kutoa hivyo kuachana bila kukubaliana.

Mimi nilikuwa kwenye kipindi Cha kujiandaa ili nikajiunge chuo kcmc Kilimanjaro.
Ila baada ya Ile Taarifa ikabidi nikamshirikishe baba yangu mzazi anipe ABC nini Cha kufanya.

Mzee akanambia tunabadilisha program Yale masuala ya chuo weka kando, nenda kajiunge kule kunakoogopwa na wengi, ili uweze kumlea mwanao halafu baada ya miaka mitatu nitakufanyia mpango uludi chuo.

Hivyo basi kupotea mtaani ila kosa nililofanya kutomuaga bibie na Mimi kutojuwa msimamo wake kama atatoa au atalea.
 
Inaendelea...........
Nilivyorudi baada ya mwaka.

Ilikuwa siku ya jumamosi nimetulia nyumbani Sina hili wala Lile nikashangaa katoto kanaletwa na dada yangu.
Kalikuwa na jinsia ya kike, hivyo kupata shauku ya kutaka nijue!

Kumtazama hakukuwa na haja hata ya kupima vinasaba, nikimtazama mzee anatabasamu wakati ni mtu seriously sana.

Baba akasema nimeamua kumpa jina la mama yangu yaani bibi yako hivyo kwa sababu umerudi salama tufanye utaratibu wa kwenda kumkomboa.

Kumbuka kule kwao, wazazi wake bado wamefura,
Walivyouliza tabia zangu mtaani wakaambiwa jamaa hana shida, ila ni mtu mkimya sana na ana misimamo.

Jioni ya siku hiyo Mama mtoto akaja kunitembelea na kumfata mtoto maana ilikuwa jioni ili arudi nae.

Kesho Wazee wakatumwa ili kujadili gharama za kumgomboa, na Ile familia ikataja kiwango kikubwa Cha pesa kinachozidi Milioni Moja, wanasema kuwakomoa.

Ikabidi nilipe na Wala sikuwa na shida.
Walivyouliza nichague mtoto akae wapi, nikasema akae kwa mama yake ili kakue vizuri.

Baada ya matukio hayo nikapotelea zangu mkoani kwenda kupiga kazi, huku tukiwa na mawasiliano mazuri na mama mtoto.
 
aliyemuelewa mleta uzi namna alivyoeleza kwenye paragraph ya pili kutoka mwisho, naomba anieleweshe na mimi.
giphy.gif
 
Inaendelea...............
Basi wakati nipo mkoani, Kuna jamaa yangu hapo kalibu na Mitaa ya Wailes Temeke akanipigia simu.

Kunieleza kuwa Kuna movement za jamaa mmoja na mama mtoto hazielewi na jamaa anaonyesha kashaiteka Ile familia.
Kifupi jamaa anakubalika na mama mkwe hatari.

Mwamba full kupeleka mazawadi, mama zake wadogo wanaoga fedha kwa maelezo ya jamaa, hivyo jamaa akawa anajipigia kimasikhara, huku Mimi nikikabwa matunzo ya mtoto.

Nikamwambia jamaa Asante kwa taarifa, hivyo ilivyofika muda wa likizo nikarudi kitaa.
Nikafanya Juhudi aletwe mtoto kumuona kimya haletwi, nikimtuma dada yangu wanasema mtoto anaumwa, kumbe mama mkwe ndiye anayepiga biti mtoto asiletwe.

Nikakaa kimya baada ya wiki nikamvutia waya mama mtoto akasema bibi yake ndiyo hataki. Nikauchuna

Jioni wakati natoka mazoezini, Kuna mzee akanisimamisha na kujitambulisha kwamba yeye ndio Babu yake mama mtoto, hivyo akaomba nimetembelea kwake, sijui Kuna nini?

Baada ya siku mbili nikaenda, wao kwa maelezo yao, walisema wanataka wanifahamu tukaongea na kucheka, kumbuka hiyo nyumba naifahamu.
 
We jamaa kama bando limekata sema tukuunge! Kwann unaleta story nusu nusu kama goli la nyeto, unatupandisha stimu lkn hamu haikati [emoji35][emoji35][emoji35]
Mimi nime-skrinishoti kabisa kesho namtumia Nape Nnauye na TCRA yake waone wananchi tunavyoteseka. Hata aniporomoshee matusi kama ilivyo kawaida yake potelea mbali [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Inaendelea.................
Kifupi nikapat taarifa tena, yule jamaa kapeleka barua ya posa hivyo inasubiriwa kujibiwa?

Mimi nilichokifanya ni kusafiri usiku usiku, kutoka mkoani kumbuka ni zaidi ya kilomita 950 mpaka dar,
Yule mzazi wake wa kike akawa anatamba mtaani kwamba Binti yake hawezi kuolewa na familia ya watu wagumu, kwa sababu yeye ni mzaramo.

Yule jamaa ni mtu wa Tanga aliyetoa posa lakini kubwa kuliko akaapa hata wafanyeje mtoto wao ataolewa na huyo.

Nilivyofika dar, Moja kwa Moja home, huku nikijiuliza nichukue atua gani?
Nibebe Mwanangu maana niliapa mtoto wangu hawezi kulelewa na baba wa kambo nikiwa hai au nibebe mama mtu ili kukata ngebe za yule bi mkubwa?

Naomba ifahamike mpaka muda huo, hizi familia hazipikiki chungu kimoja ila binti hakuwa na shida binafsi ila mama yake mswahili kinyama.

Yule jamaa huduma kazidisha na kazi yake ni mjeda sometime anakuja na gwanda zake kitaa.
Vijana mtaani wakawa wanamwogopa fulani hivi ila nikasema huyu hanijui Mimi sio Mandonga [emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38].

Nikampigia simu mama mtoto nikimtaka kesho tuonane, hivyo aje nyumbani huku akiwa na sauti ya kiuoga uoga akidhani nimeshagundua Janja yao.

Binti akafika kesho yake, tukajadili ishu ya yeye kutolewa posa, kakajitetea mama yake ndio kalazimisha na mahari ishatolewa, sijui naeleweka?

Yaani wakati Wana hisi mtaa kumbe tayari, hapo ni mchumba wa mtu, halafu katoto kangu kanamwita anko.

Nilichomwambia kesho tunaondoka wote na Leo hapa nyumbani hutoki, mwache baba yako aje?….....…
 
Inaendelea.....................
Kama waswahili wasemavyo usiku wa deni haukawii kukucha.
Kesho yake alfajiri hao ubungo, safari kuelekea mkoani ikaanza, huku nikimwambia amjulishe babu yake?

Kipindi hiki nilikuwa tayari nimesharudi chuo ila sikuendelea na taaluma za sayansi bali vitu vingine hivyo mipango yangu na baba ilikuwa inakwenda kama ilivyopangwa.

Baada ya safari ya kutwa nzima, tukafika salama huku maisha mengine yakiendelea ila kwao walibaki na aibu kubwa hasa mama yake.
Hapa unajifunza usijaribu kuwatenganisha watu wapendanao.

Ili kuwakata kilimi limi, baada ya miezi miwili akabeba tena ujauzito na kuendelea kuishi kwa upendo, huku Mimi nikimalizia shahada yangu ya kwanza.

Nikimalizia pia ujenzi wangu wa Nyumba ya kwanza kule Msongola, yaani kinaweza kuwa ni kipindi bora kwenye maisha yangu.

Kakazaliwa katoto ka pili, haka Sasa kalikuwa ka kiume na kuamua kumpa jina la baba yangu.

Na Binti alitakiwa aende dar kupeleka mtoto kwa wazazi wangu na nduguze.
 
Back
Top Bottom