Hii ni kwa hustlers/wapambanaji wote

Merchante

JF-Expert Member
May 9, 2017
1,293
2,680
Hii ni kwenu wanangu sana, wapambanaji & watafutaji wote. Haijalishi unatafuta katika mazingira gani, umezungukwa na nani, muda gani, mahala gani na kwa nani. Pambana mpaka tone la mwisho la jasho na damu yako.

Mpambanaji au mtafutaji hakati tamaa na kijitoa uhai(kujiua). Hustler akikata tamaa anazama chaka lolote lile kusaka Mabunda. Ila sio kuiba, kutapeli, n.k kwasababu wapambanaji wote tunaijua siri ya pesa, kwamba ukiipata katika njia ambazo si halali huwezi kuitumia katika matumizi halali na ikaleta matokea chanya ya kudumu.

Saka mabunda popote pale, usikae sehemu moja miaka kibao na hupigi hatua. Zone A pakikataa hama mpaka zone B,B ikigoma nenda C. Hapa namaanisha life likikataa Dar, nenda Mbeya, Mbeya likikataa nenda Kakonko, likigoma Kakonko nenda Dodoma, n.k.

Usiwe mtu wa kukaa na kujutia ya nyuma, hustler hajutii, analichukua litakalokuja kama lilivyo.

Chapa kazi! Haijalishi ni kazi gani, chapa kazi kwa bidii, halijalishi nani anakutazama wewe chapa kazi muhimu kono liende kinywani. UKIPATA KUMBUKA KUWEKA AKIBA, AKIBA HAIOZI. Akiba itakusaidia siku za baadae kama mchakato unaofanya ukibuma.

Ukiotea mabunda mengi nunua hata ardhi kadhaa, popote pale ambapo ni dili. Ardhi ni akiba nzuri sana kwa fighter yeyote yule.

MAMBO YA KUEPUKA

1: LUNDO LA MADEM

Hii ni kwa sisi wanaume,madem watakurudisha sana nyuma Mzee,utahisi unaenjoy kupewa papuchi ila kiuhalisia kwa ninja yoyote yule madem si kitu cha kukiweka karibu kipindi unajitafuta.

Kama utaweza achana kabisa na issue ya mahusiano, kipindi unajitafuta (wengi watapinga ila maninja wananielewa).

Kutokua na dem haimaanishi kwamba huli papuchi kabisa, kula inapobidi sana,sio kula kula tu hovyo hovyo. ZINGATIA: KULA PAPUCHI INAPOHITAJIKA SANA,(Zingatia neno "Sana")

2: MITUNGI
Hiki ndio kikwazo kwa wapambanaji wengi sana,unakuta mtu anajitafuta anapata labda buku 10 kwa siku ila 8k anaishia kula mtungi(huo ni mfano).

Jitahidi usiwe na uraibu na pombe,maisha yako yatakua ni kituko (ingawa ni maisha yako sisi hayatuhusu,ila ndo hivo wana lazima tusanuane)

Kama unakula mtungi jitahidi kubalance sana walau kwa week mara moja au kwa mwezi moja. Tena sio hiyo mara moja ndio unywe kama una beef na mitungi.

3: KUJILINGANISHA NA MTU
Oyaa! Hii kitu ndo huwafanya wengi wajikatie tamaa na kuona hakuna kitu wanafanya katika haya maisha. Kila mtu ana njia zake za utafutaji, so acha kujilinganisha na watu eti kisa ni mwanao au rika lako au umesoma nae.

Zingatia: Watu wametoboa kwa namna nyingi, nyingine ukielezwa huwezi kuzitamani. So fight katika zone yako na pambana na adui wa size yako.

4: KUCHAGUA KAZI
Achana na hizi mambo za kuchagua kazi,chapa kazi yoyote ile halali ambayo itakuingizia kipato halali. Unakuta kidume/beberu zima liko kwa maza linagombania vijiko vya ubwabwa, masufuria ya ukoko na madogo na Dada wa kazi kisa tu hataki kwenda street kupiga kazi fulani. Ukimuuliza anaona aibu au eti kazi sio hadhi yake, blad faken!!

5: MAKUNDI YA KIJINGA
Unakuta mwana katika circle yako wamejaa mabishoo wasio na michongo, walamba lips waomba hela za madem, wavivu, wapiga mizinga, mariooz, nk. Unadhani utakua na mentality za kujilipua machaka kusaka mabunda?

6: USIJIPE SANA THAMANI NA USIISHUSHE SANA THAMANI YAKO
Hili la kujiona wewe ni wa hadhi fulani kisa umesoma au umri wako,au mtoto wa family fulanj ndio hupelekea watu kukataa baadhi ya michongo. Kwa kifupi mnazingua,wewe chapa kazi, thamani na heshima yako itaonekana pale ukiwa na mabunda ya kutosha Mzee.

Pia usiishushe sana thamani yako, utanyanyaswa, utalipwa ujira kiduchu kwa kazi mlima. Kwa kifupi kuwa normal, tambua ni kipi unahitaji kwa wakati gani na mahali gani.

NAMALIZA NA HII KWA WANANGU WA GHETTO
Kanuni ni zile zile, chapa kazi,save mabunda kiasi, achana na mapenzi kabisa (ukiweza lakini), usisahau kujipikia unachotaka kwasababu kupika huokoa sana bajeti (mkibisha naweka mchanganuo hapa).

Kwa ambao hamjatoka kwenu pitia ule uzi wa "Ulianzaje kukaa ghetto"

NB: PIGA KAZI,PENDA KAZI YAKO.
Jah bless us

Nawasilisha,
MERCHANTE
 
makini sana hii,

nimependa hio usijilinganishe na wengine kisa ni marafiki, mpo rika moja, mmesoma wote, n.k.

Hata huku makazini mtu ana masters anaishia kukunja laki 8 lakini mtu ana diploma yake anakuja na subaru yake ukimwambia nipe mchongo anakupa juu juu tu hazami kwenye siri
 
makini sana hii,

nimependa hio usijilinganishe na wengine kisa ni marafiki, mpo rika moja, mmesoma wote, n.k.

Hata huku makazini mtu ana masters anaishia kukunja laki 8 lakini mtu ana diploma yake anakuja na subaru yake ukimwambia nipe mchongo anakupa juu juu tu hazami kwenye siri
Hali ndio kama hizo, mwingine akiona hivyo anapanic,kwamba why huyu wa Diploma asukume ndinga na yeye na Masters yake ana maliza viatu.
 
makini sana hii,

nimependa hio usijilinganishe na wengine kisa ni marafiki, mpo rika moja, mmesoma wote, n.k.

Hata huku makazini mtu ana masters anaishia kukunja laki 8 lakini mtu ana diploma yake anakuja na subaru yake ukimwambia nipe mchongo anakupa juu juu tu hazami kwenye siri
Watu wenye michuzi hawasemagi wanaipataje ..
 
Mademu + Mtungi
CB2FD03A-8B0D-4130-B4CC-B2779D0A388F.jpeg
 
Back
Top Bottom