Hii ni kwa hustlers/wapambanaji wote

Hii ni kwa hustlers/wapambanaji wote

Kwa mama ntilie nauziwa chakula 2000. Naomba mchanganuo wa kujipikia kwa sh 2000. Yaan hyo elfu 2 itoshe kununua gas, unga, mboga, mafta, chumvi, maji, viungo+muda naotumia kupika+kuosha vyombo.
Vuta kiti kaa nikupe madini Mzee.

Hiyo buku 2 huwezi kununua vitu vyote ulivyo ainisha hapo juu. Ila buku mbili unayoila kwa mlo mmoja unaweza kula hata milo miwili ilokamilika sio hivyo vibakuli vya mama ntilie.
Sijajua hesabu zako umepigaje ulipotaka buku mbili inunue mazaga yote mfano unga, gas, mchele, mboga, n. Umeandika kama mtu akinunua Gas basi anapika pishi moja inaisha,mboga na unga atapika mlo mmoja vikaisha. Kitu ambacho si sahihi.

1: MAFUTA YA KULA

Dumu la mafuta lita 3 huku nanunua 9,500 kama dumu ninalo,nikiwa sina dumu ni 12. Mafuta ambayo kwa matumizi yangu huwa natumia kwa miezi mitatu.

2: MCHELE
Kuna mchele wa kuanzia 1,700-3,000 per kg. Nunua hata wa 2,500 kwa kg 5 ni 12,500. Huu utaula zaidi ya mwezi kwasababu hutokula wali mara kwa mara.

3: UNGA
1KG ni 1,700 kwa kg 10 ni 17,000. Kg 10 ni nyingi sana utakula hata miezi mitatu na zaidi.

4: GESI
Hapa kuna mitungi ya 40k-50k kwa mitungi midogo,huo ni mpya. Tuassume kujaza ni 18k mpaka 25,000. Gas ambayo unatumia zaidi ya miezi miwili.

5: SUKARI
1kg ni 1,8000 ile ya packet. Hiyo kg moja inatosha kwa more than two weeks kama uko peke yako. Na ni siku 8 mpaka 9 kama mko wawili.

6: MAZAGA ZAGA MENGINEYO
Hapa nazungumzia nyanya,bamia,nyanya chungu karoti,hoho,vitunguu maji,vitunguu swaumu,nazi,n.k

Ambapo mazaga ya msingi zaidi kama nyanya za buku unapikia mboga tatu,kitunguu cha 1,000 unatumia kwa mboga hata 5-6,vile vile kwa karoti za buku ni siku 5-6. Kwasababu haya mazaga yote kuna mafungu kuanzia jero,n.k. Hoho la jero linatoa mboga hata tatu.

Ukipiga hesabu hapo unapata TSH 73,000/= ambayo ni bejeti ya kuanzia miezi miwili na kuendelea. Ukiwa unanunua mboga za hapa na pale waweza kufika walau 150,000/= kwa miezi mitatu na zaidi.

Sasa wewe mlo wako mmoja tu wa 2,000 kwa mwezi ni 60,000/=,kwa milo miwili inakua ni 120,000/= hapo bado huli chakula bora,unakula tu kujaza tumbo.

Tunaposema kujipikia ghetto ni bora kuliko kununua tunamaanisha kwamba mazaga ya msingi kama Gas,Chumvi,Sukari,Mafuta, Mchele unavyo so sana sana huwa ni mboga tu ambayo si gharama kubwa. Pia waweza kuamua leo ule nini kwasababu chakula si ugali,pilau na wali tu kama mnavyojaza matumbo huko kwa mama Ntilie
 
kuna mwanangu ni mpambanaji sana ila misingi ya wapambanaji hafuati, akipata 20K halali kwake anarudi asubuhi na hang over za pombe hana hata mia. Yeye ni pombe na pisi akiwa hana hela utamuonea huruma anakula viapo vyote kuwa hatorudia ila akipata hela kidogo mambo ni yale yale.
Huyo inabidi asaidiwe mapema kabla hajakutana na tatizo kubwa zaidi. Fanyeni mpango mpaka atamani mafanikio yenu na kuona kama mtungi unampotezea muda. Hapa namaanisha wekeni mafanikio yenu hata kama ni madogo mbele yake,hii itasaidia kujiona anakosea .
 
Wanangu sana.
Msiache kuishi katika misingi yetu hii.
 
Back
Top Bottom