Hii ni kupeana hasara tu.

Hii ni kupeana hasara tu.

Kyenju

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2012
Posts
5,143
Reaction score
2,547
Fikiria umempeleka mtu hotelini/mgahawa, ukamwambia aagize anachokitaka, akaagiza sahani ya chips, kuku nusu na soda, alafu katika vyote hivyo kila kimoja anatumia nusu nusu anaacha.

Hii tabia huwa inanikera sana, sijui wewe unasemaje kuhusu tabia hii.
 
Hiyo inaudhi sana niliwaikumpeleka dada mmoja hotelini(jina ninalo)aliagiza mambo kama hayo kisha akaonja na kuacha gharama ilikuwa 8500/tsh ndio si kubwa lakini iliuma sana
 
hahahahaha.......mabepari utawajua tu.
 
Hiyo inaudhi sana niliwaikumpeleka dada mmoja hotelini(jina ninalo)aliagiza mambo kama hayo kisha akaonja na kuacha gharama ilikuwa 8500/tsh ndio si kubwa lakini iliuma sana

kwako wewe ni ndogo, ila kwetu sisi ni hela mingi sana!
 
Hiyo inaudhi sana niliwaikumpeleka dada mmoja hotelini(jina ninalo)aliagiza mambo kama hayo kisha akaonja na kuacha gharama ilikuwa 8500/tsh ndio si kubwa lakini iliuma sana

Tatizo siyo gharama, ni vyema ukaagiza chakula utakacho kimaliza, hata kama utaagiza chakula cha 25,000 ukakila chote kwangu siyo tatizo.
 
Na ni ustaarabu sana kula chote ulichoagiza.... Hii inaonyesha unajifahamu kuanzia njaa yako na ulaji wako. kuna mijitu kuacha msosi ndo inadhani ni usasa, kumbe ujinga mtupu....
 
ha ha ha poleni sana anaagiza henken anakunywa robo nyingine anamwaga ha ha ha
 
majuzi nilifunga chips kuku zaidi ya nusu sahani iliyomshinda mtu!!!!japo yeye alionesha kunishangaa,ila niliondoka nayo!ni kweli inakeraaa!!!
 
Hiyo inaudhi sana niliwaikumpeleka dada mmoja hotelini(jina ninalo)aliagiza mambo kama hayo kisha akaonja na kuacha gharama ilikuwa 8500/tsh ndio si kubwa lakini iliuma sana

Alitambua kwamba imekuuma????
 
Tatizo siyo gharama, ni vyema ukaagiza chakula utakacho kimaliza, hata kama utaagiza chakula cha 25,000 ukakila chote kwangu siyo tatizo.

Mbaya zaidi unakuta kuku anaila kwa kunyofoafoa tu na mlipaji siyo yeye, sijui njaa inakua haiumi!!!
 
inaboa aisee mi mpenzi wangu akiagiza chakula wakileta kingi huwa ananipunguzia kabla hata hajaanza kula anabakisha kinachomtosheleza
 
majuzi nilifunga chips kuku zaidi ya nusu sahani iliyomshinda mtu!!!!japo yeye alionesha kunishangaa,ila niliondoka nayo!ni kweli inakeraaa!!!

Hiyo safi, hela utafute wewe mwingine aje kuifanyia maozoezi ya kuipoteza! Alafu kwanini tabia hizi wadada hawaziachi!
 
Fikiria umempeleka mtu hotelini/mgahawa, ukamwambia aagize anachokitaka, akaagiza sahani ya chips, kuku nusu na soda, alafu katika vyote hivyo kila kimoja anatumia nusu nusu anaacha.

Hii tabia huwa inanikera sana, sijui wewe unasemaje kuhusu tabia hii.

.
Uswahilini kwetu kuliko akieche hata kama kashiba atakiombea rambo ya kukibeba.
Huko kwa wanaojifanya watoto wa getini ndio wana kasumba hiyo ya kujifanya hawana njaa. Baazi yao hufa na tai shingoni.
.
 
Tatizo siyo gharama, ni vyema ukaagiza chakula utakacho kimaliza, hata kama utaagiza chakula cha 25,000 ukakila chote kwangu siyo tatizo.
Sure. Bora mtu ale amalize, kuliko kula robo ilhali yeye ndo kaomba outing ili akale! Pole bro. Mwingine kaja juzi na thread kama hii, ila ya mavazi. Kajipinda na kumnunulia wake wa ubani nguo nzuri za gharama kutoka Uchina, kaambiwa na binti kuwa hizo hazitakiwi, anataka designer clothing za Italy na France tu. Asssume ndo ww umejipinda na kinusu mshahara chako, utajisikiaje?
 
Wanaume tunakubana na mengi, katika hili suala la mapenzi.
 
Hiyo inaudhi sana niliwaikumpeleka dada mmoja hotelini(jina ninalo)aliagiza mambo kama hayo kisha akaonja na kuacha gharama ilikuwa 8500/tsh ndio si kubwa lakini iliuma sana

sasa ataonekanaje kuwa ni demu wa kishua (sisteri du) kama atakomba chakula chote? akilamba chote si utasema 'duu..demu huyu anafukia! ka dumuzi..'
 
Sure. Bora mtu ale amalize, kuliko kula robo ilhali yeye ndo kaomba outing ili akale! Pole bro. Mwingine kaja juzi na thread kama hii, ila ya mavazi. Kajipinda na kumnunulia wake wa ubani nguo nzuri za gharama kutoka Uchina, kaambiwa na binti kuwa hizo hazitakiwi, anataka designer clothing za Italy na France tu. Asssume ndo ww umejipinda na kinusu mshahara chako, utajisikiaje?

hatapata zawadi kutoka kwangu tenaaaaaaaaaaaaaa
eboooooooooo
 
lakini mmewazoesha mashauzi toka mnakutana. eti mnawavumilia
mapozi kama hayo hayawezi kuzuka ghafla tu katika chakula lazima kuna mambo mengi pia huwa wanafanya kisista duuu
simu atataka blackbel wakati mwanzo hakuwa na hata nokia tochi au alikuwa na nokia tochi, outing atataka sehemu za juu, kutoka kununua mitumba atataka nguo za butiki ataacha kuagiza chakula na kula nusu?

muwe mnawambia wawe wenyewe sio kujifanya wa juuu kumbe wakawaidaaaa
 
Back
Top Bottom