Tutafika
JF-Expert Member
- Nov 4, 2009
- 1,443
- 631
Mara kwa mara kumekuwa na mijadala inayohusisha udini sijaelewa nani ana agenda ya kuleta balaa tanzania kama ilivyo nigeria na ivory cost!
Nimesoma mjadala uliochangiwa sana humu kuhusu kitabu kinachohusu maisha ya Sykes nimeona watu wanajaribu kuhakikisha kila kitu kinachofanywa na mtu basi sifa au lawama wapewe wote wa dini yake kupitia mgongo wa dini husika! Yaani eti mkatoliki akiua muislam wanasema wakatoliki wauaji wa uislam! Au eti mwalim muislam akimchapa mwanafunzi mkatoliki wanasema waislam hawataki wakatoliki wasome! Hivi hatuna utaifa?, mnapeleka wapi jamii?
Inafikia mtu anahoji eti mbona wabunge wengi ni waislam/wakristo utadhani uchaguzi unafanyika msikitini/kanisani?
Mbona kama dini zimeturoga tunasahau kama zilitukuta hapa hapa na Tz yetu?
Mi nadhani tu muda ni sasa wa kuhubiri utaifa na utu wetu! Kamwe tusikubali utaifa/Utu wetu kubadilishwa kuwa udini!
Kama ni njama za wakoloni (waarabu na wazungu) tusimame tuwazomee na ikibidi tuwatake wasitutembelee!
Mungu wabariki watanzania wasibaguane kama usivyowabagua unapogawa neema ya mvua!
Wote sema AMEN