Hii ni hatari sana, tanzania tumechoka amani?

Tutafika

JF-Expert Member
Nov 4, 2009
1,443
631
Mara kwa mara kumekuwa na mijadala inayohusisha udini sijaelewa nani ana agenda ya kuleta balaa tanzania kama ilivyo nigeria na ivory cost!

Nimesoma mjadala uliochangiwa sana humu kuhusu kitabu kinachohusu maisha ya Sykes nimeona watu wanajaribu kuhakikisha kila kitu kinachofanywa na mtu basi sifa au lawama wapewe wote wa dini yake kupitia mgongo wa dini husika! Yaani eti mkatoliki akiua muislam wanasema wakatoliki wauaji wa uislam! Au eti mwalim muislam akimchapa mwanafunzi mkatoliki wanasema waislam hawataki wakatoliki wasome! Hivi hatuna utaifa?, mnapeleka wapi jamii?

Inafikia mtu anahoji eti mbona wabunge wengi ni waislam/wakristo utadhani uchaguzi unafanyika msikitini/kanisani?

Mbona kama dini zimeturoga tunasahau kama zilitukuta hapa hapa na Tz yetu?

Mi nadhani tu muda ni sasa wa kuhubiri utaifa na utu wetu! Kamwe tusikubali utaifa/Utu wetu kubadilishwa kuwa udini!

Kama ni njama za wakoloni (waarabu na wazungu) tusimame tuwazomee na ikibidi tuwatake wasitutembelee!

Mungu wabariki watanzania wasibaguane kama usivyowabagua unapogawa neema ya mvua!

Wote sema AMEN
 
Jomba una akili sana.
Shida ya dini inapandikizwa taratibu nchini, zaid kwa haja za kisiasa za watu wachache.
Baada ya ya maneno na chokochoko hizi kuna hatari ya kufuatiwa na vitendo, kama vya huko mto wa mbu.
TUKUMBUKE kuwa hakuna mateso makubwa chini ya jua kama kuikimbia nchi yako na kupiga hodi kwa majirani.
 
upande mmoja utakuelewa, mwingine hautakuelewa
 
Hii ingependeza akasukumiwa mkulu; yeye amelalamika mara nyingi kuwa kuna nyufa hizo za kidini. Yeye akiwa mwajiri no 1 ameshindwa kuwataja wahusika hadharani wala kuamuru akina Shimbo kuwashughulikiwa hao wanaoeneza udini, unafikiri ni nani mwingine wa kumfunga paka kengele!
Ktk karne hii wapo wachahe wanaoabudu mawe, mibuyu nk. Lakini inapokuja kwenye kuhitaji maji safi, elimu bora, huduma safi za afya, umeme wa kutosheleza nk hili halibagui mtu kwa dini yake.
Taifa lirejee kwenye misingi ya kutenda haki, na viongozi waoneshe kule wanakotaka kuwapeleka wananchi, ili wananchi watoe ushirikiano wa 100%, wasitende dhambi ya kuwagawa kwa faida zao za kisiasa.
 
Tz ha2na udini bali tuna ufisadi unaojengewa ukuta wa udini Ukiwalinda mafisad kwa kutugawa ktk iman zetu huku 2kisahaulishwa kuoji mambo ya msingi
 
Hii inatokana na kukosa uongozi wenye hekima na utashi wa kuongoza! Raisi wetu alipokosa kuza alizotegemea kupata lalamiko la kwanza ni kwamba amenyimwa kura kwa sababu yeye sio mkristo!
 
tutajikuta tunakua wakimbizi au tunaishi uhamishoni kenya msumbiji burundi rwanda na kongo hapo sasa sijui itakuweje
Jomba una akili sana.
Shida ya dini inapandikizwa taratibu nchini, zaid kwa haja za kisiasa za watu wachache.
Baada ya ya maneno na chokochoko hizi kuna hatari ya kufuatiwa na vitendo, kama vya huko mto wa mbu.
TUKUMBUKE kuwa hakuna mateso makubwa chini ya jua kama kuikimbia nchi yako na kupiga hodi kwa majirani.
 
Misingi ya taifa letu haina udini hata kidogo. Mawazo potofu ya wanasiasa walio madarakani, kwa sababu zao tu za kipuuzi wanazozijua wenyewe wameanza kuingiza udini katika maneno yao na labda hata matendo.
Kibaya zaidi wanaoeneza haya ni viongozi wa juu kabisa ambao hawakutegemewa kueneza maneno kama haya ambayo yanajenga mgawanyiko wa hatari kwa jamii wanayoiongoza.
Hakuna uthibitisho wa udini kwa wananchi walio wengi ila kwa wanasisa na viongozi uthibitisho ni maneno yao wenyewe kupitia hotuba zao.
Watanzania wanatakiwa kupuuza mawazo potofu yanayoweza kuangamiza taifa ya viongozi hao.
 
Bahati mbaya wanaolipalilia hili wapo na ndo wenye makoromeo makubwa kupiga kelele kwa faida yao. Bahati mbaya tena kwamba raia wengi wa nchi hii hawataki kusumbua akili kutafakari yanayosemwa zaidi ya kuyabeba yalivyo! Nway, kichwa kikiwa kibovu, basi hata sehemu zingine za mwili zina matatizo.
 
Hii inatokana na kukosa uongozi wenye hekima na utashi wa kuongoza! Raisi wetu alipokosa kuza alizotegemea kupata lalamiko la kwanza ni kwamba amenyimwa kura kwa sababu yeye sio mkristo!

Sijui anafanya maksudi au anafanya bila kujua? Yaani pamoja na ugumu wa maisha uliopo sasa lakini hili linaniuma sana!, sijui nitapaza vip sauti watanzania wote wanielewe na kubadilika!!
 
udini tz hauwezi kuisha ni chuki iliyopandikizwa na bado inapandikizwa,wakristo waligomea kukipigia kura chama cha cuf kwa kudhani ni chama cha mujahidina na waislamu hawakipigii kura chadema kwa kudhani ni wakatoliki
 
TUKUMBUKE kuwa hakuna mateso makubwa chini ya jua kama kuikimbia nchi yako na kupiga hodi kwa majirani.

Nilishuhudia warundi wakikimbia na nilishuhudia kwa macho yangu maiti za wanyarwanda zikizagaa mtoni, mamba wakiwa wamekula mpaka wamechoka!,

Nilishuhudia mama wa kirundi akijifungulia njiani pasipo na msaada wowote!, yaani ni kati ya matukio ya mwaka 1993/4 ambayo sitasahau kamwe!, sasa nikiona tz nayo tunanyemelewa nahisi matumbo yanatetemeka!
 
Nitajie viongozi wote wa juu wa serikali ya Kikwete then niambie anayewaza udini ni Watanzani ama ni Viongozi?
 
Una akili sana.
Hawa wakuu wanajaribu kutugawa makundi, tujenge chuki ili wale vizuri.
Ukabila wanashindwa maana tz tuna makabila kibao.
Tukemeeni.
 
Una akili sana.
Hawa wakuu wanajaribu kutugawa makundi, tujenge chuki ili wale vizuri.
Ukabila wanashindwa maana tz tuna makabila kibao.
Tukemeeni.

Hapa ni kuwaambia tu hata kama wanatufunga basi potelea mbali!, mi nataka nichukue hatua badala ya kuendelea kuumia!,

Kwa kuanzia nitakua nafuatilia hotuba zao halafu nawaandika kwa magazeti kwa kuwataja majina na hotuba zao za uchochezi wa udini!, ikibidi nitaanzisha taasisi binafsi ya kuwakemea kama hakielimu wanavyofanya kwenye sekta elimu!,

Vip nitapata support au ndio wataniua kama walivyopanga kuwafanya kina Slaa na Mwakyembe? Au ndio nitakua nau-promote?
 
Vip nitapata support au ndio wataniua kama walivyopanga kuwafanya kina Slaa na Mwakyembe? Au ndio nitakua nau-promote?

kwenye mapambano hutakiwi kuwa muoga.
Unapopambana unatakiwa uweke nafsi za wengine mbele.
Yaani unafight kwa ajili ya watu wako au kizazi kijacho.
Watu walikubali kwenda jela kwa ajili ya watu na wengine wamekufa kwenye mapambano.
Hakuna binadamu anaweza kumuua binadamu mwenzake.
Ni mungu tu na kila mtu atakufa siku yake ikifika.
Unatakiwa kuwa na msimamo na ujasiri. Ukisimamie unachotaka kufanya na ukielewe vizuri.
Wapo wengi tutaosupport kwa namna moja au nyingine.
 
Jomba una akili sana.
Shida ya dini inapandikizwa taratibu nchini, zaid kwa haja za kisiasa za watu wachache.
Baada ya ya maneno na chokochoko hizi kuna hatari ya kufuatiwa na vitendo, kama vya huko mto wa mbu.
TUKUMBUKE kuwa hakuna mateso makubwa chini ya jua kama kuikimbia nchi yako na kupiga hodi kwa majirani.

Unaweza kunipatia habari za hapo kwenye red? ni kama nilizipata shallow.
 
Nilikwishaandika siku za nyuma kuwa kuna sasa hivi kuna kampeni kubwa zinafanyika misiktin na kwenye mihadhara ya kidini za kujenga chuki kati ya waislamu na wakristo.Hii kitu huwa inanihuzunisha sana.Watu wa usalamu wameacha hali hii iendelee bila kukemea wanaofanya hivyo.

Nashindwa kuelewa kwanini wakristo wamekaa kimya wakati kampeni zinaendelea kila kukicha misikitini.Wakati umefika kwa UWT wakristo kulishughulikia hilo suala bila kushirikiana na uongozi wa juu wa nchi ambao unaonekana ndio unashabikia hali hii.Viongozi wote wa serikali ambao ni wakristo sasa wajue kuwa kuna hatari inayowkabili wao pia hivyo waache kushirikiana na kina Rostamu ambao ndio wafadhili wakuu wa mpango huu kupitia serikali ya Iran.Waandishi wa habari wakristo wanaotumiwa na RA wajue kuwa nao hawatakuwa salama mambo yakiharibika.Wanasheria wote wanatumiwa pia wakati umefika waseme sasa basi kwani nao pia wanamsaliti kristo.

Sioni ni namna gani hili suala litaisha kwani ni too late na sumu ya kutosha imeshamwagwa misikitini.Nina wasiwasi huenda hata silaha zimeshaanza kuingia kutokea arabuni.

Nimefanya utafiti wa kutosha na umeonyesha kuwa sumu imeingia barabara kwa ndugu zetu.
 
Ajbu ni kuwa wako viongozi waandamizi ndani ya serikali na CCM walio wakatoliki wasio kosa kanisani lakini ndio wako mstari wa mbele kudai CHADEMA ni ya wakatoliki
 
Udini na Ukabila ni sumu mbaya sana katika maisha ya mwanadamu.

Angalia nchi nyingi zilizomo kwenye misukosuko mpaka hivi sasa utagundua chanzo ni Udini au Ukabila
 
Back
Top Bottom