Kwenye suala la uteuzi kisa Udini, Ponda umechemsha. Siungi mkono maana waislam kielimu wapo nyuma sana!

Status
Not open for further replies.

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
3,764
2,000
KWENYE HILI SHEKHE WANGU PONDA UMECHEMSHA!

Kwanza nikiri kwamba mimi ni muislam tena nimetokea kwenye familia ya watu wanaoijua dini,kuanzia wazee wetu na babu yangu alikua sheikh wa Bakwata wilaya nisiende sana huko

Mimi sijaelewa ..point za msingi ni zipi sisi waislam apo kwenye teuzi? Zipi sifa za teuzi za nafasi za ajira kama hizo za serikali? Unaangaliwa udini au elimu na sifa nyingine? Je sisi waislam tupo wangapi wenye elimu ya kushika nafasi hizo waliopo serikalini? Lazima tukubali wenzetu wapo wengi waliosoma zaidi na weredi wa kazi kutuzidi sisi..lazima kila eneo tuwe wachache...ili kulibadilisha hili tusomeshe watoto wetu wapate elimu bora ..hasa za vyuo vikuu..ipo siku tutakua sawa au kuwazidi...au Ponda alitaka 50/50 kwenye teuzi ?

Kama sasa waislam waliopo serikali wenye sifa Za kuteuliwa wapo wachache?...au atolee mfano Tu yeye Ponda kama ana mtoto au ndugu aliachwa kuteuliwa serikalini kisa uislam Wake na sifa anazo? Ebu azungumzie basi sekta binafsi..aende Kampuni ya Azam akaangalie ajira kati ya waislam na wakristo aone tofauti..inawezekana kuwa waislam as 98% ,wakristo 2%, aache kulalamika pasipo ushahidi wa uhakika...

Mfano mdogo sisi waislam kielimu tupo nyuma sana tungekua angalau sawa kielimu na ndugu zetu wakristo tungeenda sawa

Mfano mdogo tu wa kielimu na uteuzi ni wachaga waislam wachaga waislam 98% ni wasomi na wameenda shule kweli kweli na wapo vitengoni na wameajiriwa vizuri tu serikalini na wizarani bila tatizo lolote wala ubaguzi wowote sasa hapo ndo utaamini wanacholalamika kina ponda hakina mantiki yoyote

Waislam wa Tanzania wajitahidi wawekeze kwenye elimu kama wakristo au hata waislam wenzao wa kule uchagani na upareni mfano huko Machame na masama waone kama wataachwa kwenye hizo nafasi au lah mimi nachoongea nakielewa nimetokea huko Moshi, ukoo wetu ni wasomi sana na hakuna aliyeachwa wengine ni maprofessa vyuo vikuu, wengine wapo huko nchi za kigeni wengine wameshika nafasi nyeti wizarani

Kwa hili ponda sikuungi mkono kabisa mimi mwenyewe ni muislam lakini kwa hili la kusema eti kuna udini kwenye teuzi sikuungi mkono kabisa!
 

Truth Matters

JF-Expert Member
Apr 12, 2013
1,230
2,000
Kikwete aliwapata wapi wasomi Waislam mpaka Maaskofu wakalalamika kwa nyaraka kila uchao? Au wamekufa wote?
 

Kinjeketile

JF-Expert Member
Dec 24, 2013
967
1,000
Kila kundi Duniani linaingia kwenye uchaguzi kimkakati huku likiwa na agenda zake. Kwenye waraka kuna agenda za Waislamu kwenye uchaguzi huu,sasa wewe na wenzako leteni agenda zenu kwenye uchaguzi huu.
 

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
4,591
2,000
Mimi ni Mkristo lakini mtu anapoishusha dini nyingine naona ananishusha na mimi pia. Amani yetu inategemea co-existence ya dini zote. Kusema kuwa Waislam hawajasoma sana ni kuwatukana Waislam. Kama una uhakika na kile unachokisema, weka hapa takwimu.
 

Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
23,737
2,000
Hata Wachaga zamani walikuwa watu wakihoji Ukabila TRA na BOT walikuwa wanasema nafasi zinaangalia vigezo, sasa hv wameelewa kilio cha wenzao

Hata Wasukuma hawawezi kuelewa kwa sasa
 

Flano

JF-Expert Member
Aug 7, 2019
562
1,000
Sijui hata kwa nini hawa ndugu zetu wanajitahidi sana kuwaaminisha watu kua waislamu hawajasoma.
Kweli yaliyojificha ndani ya mioyo yao ni makubwa kuliko wanayo yadhihirisha, yaani ni chuki, chuki chuki bila hata ya sababu.
 

Johnson Fundi

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
892
1,000
huo ndio ukweli halisi mleta kasema ukweli. kama unapinga leta takwimu hapa idadi ya shule za seminary za kikristo ufaulu wao n.k. kuanzia miaka ya nyuma kabisa. kuna baadhi ya waislamu walipeleka watoto wao kwenye shule za misheni waliona mbali. Wamisionary walipoingia kila walipojenga kanisa walijenga shule na kituo cha afya, waarabu walipoingia walijenga msikiti na madrasa, halafu leo unataka ulingane na mtu aliyewekeza kwenye elimu kwa kiasi kile.
 

Johnson Fundi

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
892
1,000
Sijui hata kwa nini hawa ndugu zetu wanajitahidi sana kuwaaminisha watu kua waislamu hawajasoma.
Kweli yaliyojificha ndani ya mioyo yao ni makubwa kuliko wanayo yadhihirisha, yaani ni chuki, chuki chuki bila hata ya sababu.
hakuna chuki hapa wewe ndio una chuki. si uje na takwimu ya idadi za shule zinazomilikiwa na mashirika ya kikristo na viwango vyao vya ufaulu, pia uje na takwimu za ufaulu kwenda vyuo vya elimu ya juu, anzia miaka ya nyuma. kusoma au kutosoma si hoja sana hapa, hoja ni idadi ya wasomi kutoka kila upande.
 

ligend

JF-Expert Member
Oct 14, 2019
431
1,000
we mdada unakwama wapi embu jiulize mbona ktk nafasi ya urais hiyo kesi yako haipo na tena inajulikana kabisa akitoka jakaya anakuja magufuli
 

NAWATAFUNA

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
8,290
2,000
Uzuri nchi yetu inadhibiti mapema sana misimamo ya kidini.angeachwa mpaka sasa hata sijui kama tungepata nafasi ya kuchati kama sio kufa kabisa.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom