Hii ni Familia ya Kanali Hans Pope

Serikali kwenye corona mnaionea. Sisi wenyewe ndio hatutaki kukubali huu ugonjwa upo sasa serikali ifanyeje?

Serikali iliwaaminisha watu kuwa ugonjwa haupo. Ikawa brainwash sawa sawa hasa machinga, boda boda, wapiga debe, vibaka vibaka, mama lishe, uswahilini nk:

Madhara ya Awamu ya Tano yanayofumbiwa Macho

IMG-20210725-WA0007.jpg

Mabingwa wa brainwashing hizo wangalipo serikalini leo wakichapia chapia kivingine kuhusiana na ugonjwa huo huo.

Wameshauriwa wafanye nini kitalaamu wao kama serikali bado hawazingatii. Wako busy wakisimamisha chumi zao binafsi kwanza.

Ziko wapi takwimu au taarifa sahihi za ugonjwa huu? Kwa serikali bado Corona ni taboo. Iko kama vile kuugua au kufa kwa Corona si sahihi kuongelewa.

Karibu mwezi sasa takwimu zilizoahidiwa kuandaliwa zingali zikipikwa:

#COVID19 - Waziri Gwajima, takwimu za Covid-19 mnaandaa au mnapika?

Kimsingi kwa serikali hii ugonjwa huu haupo. Ungali labda ni vita vya kiuchumi dhidi ya Tanzania kama tulivyo aminishwa awamu ile.

Kwa serikali hii waliougua na labda hata kufa kwa Corona Tanzania ni kaka yake Mbowe na waziri Mramba peke yao ambao familia zao zilitangazo hivyo.

Kwamba serikali haihusiki?

"Ni kweli kabisa kuwa haihusiki. Ndiyo maana wahanga wa ugonjwa huu wanajigharimia wenyewe matibabu, kodi na tozo juu, mikusanyiko yote hata isiyokuwa na tija inaendelea na pasipo na tahadhari zozote."

IMG_20210911_000004_180.jpg

Pole Tanzania ambako hata mtu nyuma ya dereva anaweza kulisukuma ndinga kama anavyotaka na bado maisha yakaendelea.

Cc: Jumbe Brown
 
Acha kupotosha nyau wewe ,Hans alikuwa hajachanja na mzigo alitoka nao huko Kigoma kama Mwalim Kashasha.unapotosha ili upate faida gani wakati mtu na familia yake nzima inateketea 😏😏😏
Asa unabisha kama nani?
Acha mihemko ya kijinga
 
Ni Baba yao ndio alikuwa Mjerumani, Aliwahi kuwa RPC kagera miaka ya nyuma Sana, Mwanzoni mwa Vita ya kagera alikamatwa na Wanajeshi wa IDD AMIN akauliwa vibaya IDD AMIN akatoa shutuma tuna mamluki kulingana na yule mzee alivyokuwa ila Mama yao alikuwa MHEHE kitu Kama hicho!!!
Wewe nawe.Babu yao si ndo alimzaa baba yao?Kusema babu yao ni mjerumani si ndo pope mwenyewe jamani.
 
Ni Baba yao ndio alikuwa Mjerumani, Aliwahi kuwa RPC kagera miaka ya nyuma Sana, Mwanzoni mwa Vita ya kagera alikamatwa na Wanajeshi wa IDD AMIN akauliwa vibaya IDD AMIN akatoa shutuma tuna mamluki kulingana na yule mzee alivyokuwa ila Mama yao alikuwa MHEHE kitu Kama hicho!!!
Huyu ndo baba yao

WhatsApp Image 2019-01-15 at 22.22.47.jpeg
 
Watu wanafikiri ukichanjwa basi ujiachie achie tu. Ukichanjwa endelea kuchukua tahadhari.
Kwa mazingira ya bongo hata ukivaa mask na ukajiweka lockdown masaa 24 hautaikwepa Corona. Njia pekee ni chanjo,wengi sana chanjo itawasaidia kutougua sana hadi kufa lakini wachache bado Corona itawaondoa.
 
Chanjo ni nini?
Chanjo ni kuutayarisha mwili wako kupambana na kimelea husika kutokana na chanjo uliyochanjwa .Mfano chanjo ya Covid inaufanya mwili wako uproduce antibodies against kimelea cha covid. Sasa ikitokea umepata maambukizi mwili unakuwa tayari una askari na wanaattack vimelea hivyo haviduplicate kwa wingi mpaka kukusababishia dalili mbaya hadi kifo.
 
Acha kupotosha nyau wewe ,Hans alikuwa hajachanja na mzigo alitoka nao huko Kigoma kama Mwalim Kashasha.unapotosha ili upate faida gani wakati mtu na familia yake nzima inateketea
Kumbe uviko sio tishio maana inafahamika ilipo yaani kigoma km ulivotuambia afu kumbe tunaishi nayo tu kwani kigoma katoka juzi kat hapo?
 
Ni pigo na ni Msiba mkubwa sana kutokea kwa mara Moja.

Kingine cha kukumbushana kuwa hawa waathirika walikuwa wameshachanjwa!
Usitoe taarifa ambazo wewe huna uhakika nazo kwa lengo la kupotosha mkuu
 
Chanjo ni kuutayarisha mwili wako kupambana na kimelea husika kutokana na chanjo uliyochanjwa .Mfano chanjo ya Covid inaufanya mwili wako uproduce antibodies against kimelea cha covid. Sasa ikitokea umepata maambukizi mwili unakuwa tayari una askari na wanaattack vimelea hivyo haviduplicate kwa wingi mpaka kukusababishia dalili mbaya hadi kifo.
Mtu aliyeugua Corona na kupona, ana tofauti na mtu aliechanjwa? Kwamba mwili umeshajifunza jinsi ya kupambana hivyo una kinga ya asili tayari..
 
Kingine cha kukumbushana kuwa hawa waathirika walikuwa wameshachanjwa!
Hii chanjo basically wataalamu wanasema haizuii aliyechanjwa kutopata ugonjwa kama atakuwa exposed kwemye mazingira hatarishi. Sasa ukishalikwaa lijidudu la COVID19, lolote linaweza kutokea kama tayari una magonjwa nyemelezi
 
Back
Top Bottom