Ni miezi kama miwili imepita tangu nimalize chuo na kurudi nyumbani.....lakini hata hivyo nilikuwa narudi kipindi cha likizo kuonana na familia.
Kwanza niseme tu wazi,,,sina desturi ya kukagua simu ya mkewangu lakini baada ya kumtilia mashaka ilibidi nifanye hivyo.
Nikweli nilichokikuta inbox ya Facebook ni hiyo conversation kati ya wife(chati ya bluu)
na jamaa ambae namjua na ni mfanyakazi mwenzangu pia na nlikuwa namheshim sana.
Hiyo conversation inaonesha watu hawa ni wapenzi wala haihitaji nguvu ya ziada kugundua hilo.
Wadau hii kitu nilikuwa nasikia tu kwa watu kumbe ni kweli aisee inauma sana usiombe yakukute....
Imagine mtu tuko nae over ten years sasa pamoja na watoto wawili Leo hii ananifanyia hichi kitu..
Afadhali hata ningekuwa na tabia ya kuchepuka nisingeumia sana.....ningejisemea tu moyoni kwamba malipo ni hapahapa duniani , muosha huoshwa.
Lakini kinachoniuma Mimi nimekuwa mwaminifu tangu nilipomuoa sijawahi msaliti hata Siku moja.
Wakuu embu nisaidieni experience kwa wale mliopata maswahibu kama haya au hata kama hayajakupata nishauri tu kabla sijaharibu Niko na hasira sio ya kawaida ingawa sijionyeshi kwake.....
View attachment 897325