Hii ndoa inanivunja moyo, najuta kwanini nilimuoa huyu mwanamke

Mkuu umeongelea ishu ya mkeo kuripoti matatizo yenu kwa wazazi wake na wa kwako. Nadhani kitu ambacho umeficha ni kwamba wewe hujatulia, either ni kicheche au kwa ujumla umempa mashaka kuhusu uaminifu wako katika ndoa na ndio maana reaction yake imekua ya namna hiyo. Na pia ndio sababu anatabia ya kuripoti matatizo kwa wazazi wenu.
 
Pole kwanza kwa kuchezea makofi mawili matatu maana najua hayo huwezi kuhadithia. Halafu wanaume wenzako moto ukiwaka huwa hawajifungii ndani bali wanatoka nje.
Pili japo mkeo aliover react lakini wewe mwanaume jiweke kwenye nafasi yake sasa ndio kapiwa simu halafu akaenda barazani na mwanaume tu anayefahamiana naye akawa anambembeleza amkopeshe halafu ukawa umesikia. Mkeo huyo wa ndoa wamsiki jamaa anabembeleza akopeshwe na jamaa wala humjui. Hapo mkuu ulifanya makosa sana. Simu kama hizo ungeenda kuongelea mbali huko. Alichofanya cha kuibamiza simu kwa hasira ni justifiable given that hata wewe ungeweza kufanya kama hivyo. Kumpiga mke vibao ni makosa japo nikiri hasira ndio zinaponza lkn ni kosa.
Jambo la kuogofya ni mkeo kukushikia kisu na mtwangio. Hii kwa kweli haikubaliki maana mfano angekukuta umegeukia upande ambao haujamuona angekudhuru. Hili sio jambo dogo. Kuna binti hapa mumewe alimpiga makofi mchana. sasa mwenyewe akafuga hasıra weee usıku wakatı wa kulala jamaa kaanza kukoroma. binti kaamka akachukua kigogo cha kusukumia chapati akampiga kimoja tu kwenye upara. Jamaa alishonwa nyuzi za kutosha na ndoa ikaishia hapo maana mke pia alikimbia japo mume alimbembeleza sana warudiane. Hapo kwenye silaha ni hatari. Ingekuwa ni huku kwetu uchagani huyo mwanamke msamaha wake lazima aje na sale pamoja na mbuzi.
Mkae na wazazi muyajenge. Binaadamu wana mapungufu mengi sana na msingi wa ndoa ni kuvumilia. Tabia ya uandishi wa habari waambie pia kwenye kikao kuwa huipendi yeye ameshaolewa na anatakiwa ayahifadhi ya nyumbani kwake na sio kila kitu kuhadithia.
mkuu umenipa ushauri mzuri sana, ntaufanyia kazi...hahahaaaa, ila makofi mawili matatu sikuchezea
 
upo sahihi mkuu, lakini elewa kwamba, mimi najitambua, ningekuwa sijamheshimu ningeongelea hili suala mbele yake kule chumbani. Yeye ndo alinyata kunifuata kunisikiliza naongea nini na nan? lakini hakuwa na subira, angekuwa na busara angesubiri nimueleze pia ningempa aongee na yule dada
Kama huyo dada sio mchepuko wako kwa nini ulipoona text kwamba umpigie ulienda kumpigia sebuleni na si hapo hapo chumbani? ulitaka kuficha nini?

Binafsi sioni kosa la mkeo bali wewe ndio kimeo.
 
Sa mbona unaongea kwa mahisia
yani hapa nahisi sijafit the way jamaa alivyokuwa ananihadithia, maana nilimuona ana jeraha ndio akanipa full stori, akanitaka na ushauri. Alikuwa ana hisia kali sana, utamuonea huruma. Na mimi nimeamini kweli hakuwa na kosa, maana nilimbana sana akasema hajawahi msaliti mkewe tangu afunge ndoa
 
Wanawake wazuri waadilifi hamtuoi mnaenda kuowa wauaji mwanamke unashikaje kisu huyo mwangalie sana pole mwaya
kweli mkuu, ila suala la kumpata mwenzi NDOA sometimes ni kama kucheza BIKO tu. Maana ni ngumu kujua kama mtu unaendana nae
 
Umesema huyo dada anaebleed ni Nani yako?
Huyo dada ni rafiki wa muda mrefu kabla hata hajamjua mke wa ndoa. Na hakuwa wazi kutaja ugonjwa wake, jamaa ndio alimhoji sana na kumwambia mficha maradhi kifo kitamuumbua, ndio akafunguka kuwa ana bleed mfululizo
 
inabidi wanandoa wachunguzane childhood zao zilikuwaje.

Some kids have been traumatized and they have walked around with these loads into adulthood without knowing they have them or even how to let go.

Matokeo yake ndo kama haya.
 
hizo ndundi zenu aisee
Pole sana mkuu Mungu akutie nguvu.
Oeni wanawake wenye busara jamani ili kuepukana na ndundi zisizo na Ring
wakati mwingine huwa najiuliza ninapokua na mwanaume amenikosea wakati mwingine unaona kabisa 90% ni makosa
Lakini naamua kumpa nafasi ya kujitetea maana wakati mwingine makosa ni misunderstanding tu ..unaweza kuona kitu kumbe sivyo kilivyo.
Je kukaa na kuzungumza nae ni busara au ni ujinga kumpa nafasi ajitetee kwanza kabla sijafanya maamuzi magumu.
Kama ndio ivyo mkuu wangu bora hizi busara zangu aisee, na huyo mkeo katia fora na mavisu na michi ya kutwangia hivi hakuogopi mimi nnavyoogopa kuchafuliwa sura yangu au mwili aisee siwezi kuanzisha beef hata siku1
 
Mtwangio na kisu...shemeji alipitia jkt nini..

Turudi upande wako unamskia mke wako anaongea na simu na mwanaume alafu mwanaume anamwambia kuwa mboo yake inasimama usiku kucha amkopeshe hela aende hospital ungejiskiaje mkuu ??

Tena wewe ulivyomkorofi nahisi ungemuangushia ukuta ili afe kabisa..
Hapo kuwa mwanaume tumia akili mshape mke wako acha kumsingizia kuwa ni reporter sana hiyo ndio asili yao wanawake hawana koromeo.
Mwanaume hakimbii nyumba rudi nyumbani kaa na mkeo vizuri mpe maneno matamu tamu ye mwenyewe atapiga simu kwa mama ake na kumwambia mama nilikua nakutania.

Ungekua daktari na huyo dada ni mgonjwa wako kusingekuwa na shida
nmecheka mno
 
Aisee mm bado cjaoa hapo cna ushauri ila nimependa ulivosimulia mlivokuwa mnagombana pls unaweza endeleza story

İla pole sana ndugu
 
Back
Top Bottom