Hii ndoa inanivunja moyo, najuta kwanini nilimuoa huyu mwanamke

radicals

radicals

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Messages
3,679
Points
2,000
radicals

radicals

JF-Expert Member
Joined Nov 7, 2016
3,679 2,000
Habari wanajamvi, naombeni tumshauri huyu mwenzetu, kanisimulia mkasa wake mimi kama rafiki yake wa karibu sana. Ila nimeona nishare nanyi ili tupate mawazo murua. Nitasimama katika huu uzi kwa niaba yake. Mtanisamehe kwa maelezo haya mengi, ila ili umshauri ni vema usome uzi huu wote.

NB. For great thinkers only, if you are a small thinker stay away from this thread.

ILIPOANZIA JANA 12/09/2019
Alfajiri nimeamka nikakuta sms katika simu yangu. Ujumbe ulisomeka hivi "habari, sorry ukiwa free na ukiiona sms hii naomba unipigie, ni muhimu sana".

Ni dada ambaye ninafahamiana nae sana (long time back). Nikachukua simu, fasta nikaenda sebuleni ili nimpigie nijue kuna tatizo gani. Kumbee! mimi bila kujua, mke wangu ambaye nilidhani amelala usingizi, akanyata kimya kimya kunifuata nyuma....

Nikampigia simu yule dada, akanambia anaumwa sana, nimkopeshe fedha ili akapate matibabu. Katika kumuuliza sana unaumwa nini!,. akanambia anahisi ni amechezewa na waswahili maana ni miezi miwili mfululizo anableed!

Nikamhoji, kwa nini anahisi kachezewa! akanijibu, anajua fika atakuwa amechezewa maana kuna siku alianika nguo zake nje, mda wa kuja kuzichukua alibaini nguo zake mbili tu za ndani hazipo (zimeibiwa).

Ghafla bin vuu! hata sijamaliza kuongea nae, WIFE kapokonya simu huku kafura kwa hasira na maneno yakimtoka ."malay* mkubwa weeee, yan unaongea na demu wako kuhusu MP huoni hata aibu, mseng* mmoja wee".

Nikamfuata ili nichukue simu niikate(ilikuwa hewani bado) afu nimuelezee hali halisi, akaibamiza chini, PAAAAAH.........Busara niliweka kando, nilimpa kerubu mbili matata,(nakiri sijawahi kumpiga kabla)........Nae akanivamia, nikamsukumia kwenye sofa nikaokota simu kwa hasira nikaenda chumbani kujifungia.

Punde si punde, yupo mlangoni..."KAMA WEWE MWANAUME KWELI FUNGUA MLANGO"...mh, nikaona hii dharau sasa, huyu anajiamini nn!!!!.....Nimeanza kufungua mlango tu, aaahmad!!!!, kabeba mtwangio wa kinu na KISU.

Nikataka nipush mlango ili niubane tena, akanisogezea knife, akanichana kwenye mkono(my arm).

Nilipata hasira sana yani sana.....nikampa kibao kizito cha shavuni, alitoka ndukiii akasahau hadi zana zake....breki ya kwanza jikoni.....

Sikumfuata, fasta nikatafuta leso ili nijifunge jeraha(maana damu ilikuwa inamwagika).


MUDA SI MUDA, karudi tena hadi mlangoni, akanifungia kwa funguo kwa nje. "Leo hutoki kabisa, utakaa humo humo ndani, NI NANI ALIYEKWAMBIA MWANAMKE ANAPIGWAA" . Aliendelea kupayuka pale nje, maneno yote yalimtoka.
Alivyoona simjibu , akaenda nje, akafunga geti, akarudi sebuleni, akajifungia kwa ndani.

Nilikaa takribani nusu saa nikimsihi anifungulie ili nijiandae niwahi kazini, KIMYAA!!!!.

Nikachukua simu yangu ndogo, nikampigia boda boda aje na fundi seremala na zana zote za kuvunjia vitasa. Nikapaki baadhi ya nguo katika begi langu la mgongoni (nilijiapia sirudi home).
Fundi alipofika, nilimpa maelekezo, akaruka uzio. akatindua kitasa.....nikamalizana nae pamoja na boda boda.


Nilijiandaa, nikabeba na begi.. nikazunguka dirishani nikamwambia mke wangu *"NAONDOKA, SITARUDI KWA SABABU UMENISHIKIA KISU UNA LENGO LA KUNIUA".
huyooo, nikaepa..

Muda wa mchana alinipigia simu sikupokea maana ilikuwa kwa fundi inatengenezwa. Akaja kazini kwangu(nimejiajiri) hakunikuta. Akawapa maagizo wafanyakazi wangu nikifika wanipe taarifa kuwa yeye alifika pale kuniulizia. Kwa kweli sikumtafuta kabisa hiyo jana, na home sikurudi, nililala kwenye chumba nilichompangia mfanyakazi wangu wa kiume.


LEO ILIPOFIKIA 13/09/2019
Simu za wana ndugu zimefululiza hapa na sijapokea, nimepokea ya mama tu. Akanambia amepokea malalamiko kuwa nimempiga mwenzangu, na nimehama na nyumba.!!!!!!!
Nimemwomba mama nimpigie badae jioni kwa sababu asubuhi nilikuwa nimetingwa nahudumia wateja(ila pia nilikuwa sijaona nimweleze nini)

MAELEZO YA ZIADA
I. Huyu mke wangu ni reporter sana yaani nahisi hata wanandugu washaanza kumchoka, ugomvi kidogo tu, atasimulia home kwangu na kwao.
Pia ifahamike kwamba yeye pia ni binadamu, huwa ananikosea lakini mimi huwa namchukulia the way alivyo.

II. Huyu ni mke wangu wa ndoa katoliki , ndoa ni ya mwaka mmoja sasa


HAYA WANAJAMVI
ungekuwa wewe ungemshauri nini huyu ndugu?

pia wewe great thinker una maoni gani kuhusu changamoto hii aliyoshare nawe?
 
radicals

radicals

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Messages
3,679
Points
2,000
radicals

radicals

JF-Expert Member
Joined Nov 7, 2016
3,679 2,000
DAAAH MKUU POLE SANA HIZO NI CHANGAMOTO ZA NDOA.CHA MUHIMU MKAE CHINI UMUULIZE VEMA KWANINI ALIAMUA KUHAMAKI NAMNA ILE BILA KUWA NA USHAHIDI??!!
Huyu ndio tabia yake, anapenda sana kufuatilia simu yangu. Wakati mwingine anaiba simu yangu anachukua namba, anaanza kuwapigia watu anaoona calls zimeingia sana. Ana wivu wa kitoto sana
 
Kamwene kamwene

Kamwene kamwene

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2019
Messages
752
Points
1,000
Kamwene kamwene

Kamwene kamwene

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2019
752 1,000
Mtwangio na kisu...shemeji alipitia jkt nini😁😁..

Turudi upande wako unamskia mke wako anaongea na simu na mwanaume alafu mwanaume anamwambia kuwa mboo yake inasimama usiku kucha amkopeshe hela aende hospital ungejiskiaje mkuu ??

Tena wewe ulivyomkorofi nahisi ungemuangushia ukuta ili afe kabisa..
Hapo kuwa mwanaume tumia akili mshape mke wako acha kumsingizia kuwa ni reporter sana hiyo ndio asili yao wanawake hawana koromeo.
Mwanaume hakimbii nyumba rudi nyumbani kaa na mkeo vizuri mpe maneno matamu tamu ye mwenyewe atapiga simu kwa mama ake na kumwambia mama nilikua nakutania.

Ungekua daktari na huyo dada ni mgonjwa wako kusingekuwa na shida
 
radicals

radicals

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Messages
3,679
Points
2,000
radicals

radicals

JF-Expert Member
Joined Nov 7, 2016
3,679 2,000
Pole Sana Kwa Changamoto
Rudi Home Haya Yanazungumzika Vizuri Sana
mkuu, mimi binafsi akili inanambia nijipe likizo wiki mbili hivi ndio nirudi home. Ningekuwa nilimtoa kwao ningemrudisha, tatzo tulifahamiana mjini na nilimkuta kaajiriwa mjini. So it is better niondoke mimi
 
Jane Msowoya

Jane Msowoya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2017
Messages
2,038
Points
2,000
Jane Msowoya

Jane Msowoya

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2017
2,038 2,000
Kuna muda ndoa hugeuka gunia la misumari, unahangaika kulitua huwezi

Ushauri wangu, wakae wayaongee na wakubaliane mfumo mzima wakuishi Maana ndoa ni mkataba wa hiyari
 
radicals

radicals

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Messages
3,679
Points
2,000
radicals

radicals

JF-Expert Member
Joined Nov 7, 2016
3,679 2,000
Mtwangio na kisu...shemeji alipitia jkt nini..

Turudi upande wako unamskia mke wako anaongea na simu na mwanaume alafu mwanaume anamwambia kuwa mboo yake inasimama usiku kucha amkopeshe hela aende hospital ungejiskiaje mkuu ??

Tena wewe ulivyomkorofi nahisi ungemuangushia ukuta ili afe kabisa..
Hapo kuwa mwanaume tumia akili mshape mke wako acha kumsingizia kuwa ni reporter sana hiyo ndio asili yao wanawake hawana koromeo.
Mwanaume hakimbii nyumba rudi nyumbani kaa na mkeo vizuri mpe maneno matamu tamu ye mwenyewe atapiga simu kwa mama ake na kumwambia mama nilikua nakutania.

Ungekua daktari na huyo dada ni mgonjwa wako kusingekuwa na shida
upo sahihi mkuu, lakini elewa kwamba, mimi najitambua, ningekuwa sijamheshimu ningeongelea hili suala mbele yake kule chumbani. Yeye ndo alinyata kunifuata kunisikiliza naongea nini na nan? lakini hakuwa na subira, angekuwa na busara angesubiri nimueleze pia ningempa aongee na yule dada
 
M

maloloo

Senior Member
Joined
May 26, 2019
Messages
182
Points
250
M

maloloo

Senior Member
Joined May 26, 2019
182 250
Mtakuja kuuwana huyo hatobadilika ni tabia yake! Muwacheeeeeeeee
 
radicals

radicals

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Messages
3,679
Points
2,000
radicals

radicals

JF-Expert Member
Joined Nov 7, 2016
3,679 2,000
Kuna muda ndoa hugeuka gunia la misumari, unahangaika kulitua huwezi

Ushauri wangu, wakae wayaongee na wakubaliane mfumo mzima wakuishi Maana ndoa ni mkataba wa hiyari
kweli mkuu, asante kwa ushauri wako. ngoja upepo huu wa hasira upite ndipo wazungumze
 

Forum statistics

Threads 1,335,546
Members 512,359
Posts 32,509,312
Top