Hii ndiyo hasa tafsiri ya Nabii Katika Agano Jipya

Mathayo 23:33-34
[33]Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?

[34]Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;

Kama Mungu hataleta nabii ili atupe mwanga hukumu haitakuwa ya haki kwa sababu wengine aliwatumia watu wakuwaongoza.
Uzuri Mungu alimtuma yohana wa kizazi hiki ( William Marion Branham)
Manabii wapo na watakuwepo,

Muhimu ni kuwa, unabii wao lazima ukiri kuwa YESU ndiye MUNGU aliyekuja Katika mwili wa Mwanadamu, akazaliwa,AKAFA, akazikwa na kufufuka siku ya tatu,

Na unabii wao, iwe ndani ya kanisa au Katika level ya nchi,iwe ni Katika kulijenga kanisa
 
Salaam, Shalom!

Palikuwepo manabii wengi Katika agano la kale, mfano Adam, Nuhu, Musa, Elia, Nehemiah, Daniel nk nk.

NABII katika Agano la kale na kuishia kwa Yohana Mbatizaji,waliishi maporini kujitenga na UOVU kuepuka kuona, kusikia UOVU Katika mikusanyiko ya watu, manabii hawakuoa, hawakujenga au kuanzisha makanisa kama sasa, ukiona mtu anajenga nyumba ya ibada na kuhudumia watu, huyo ni mchungaji mwenye karama ya unabii, Mungu akimwita nabii akafungue kanisa, huyo ni mchungaji lakini ndani ana karama ya unabii.

TAFSIRI YA NABII.

Nabii ni mtu aliyeteuliwa na Mungu , mtu huyo, kinywa chake, Mungu hukitumia kunena yatokayo kwa Mungu, kuelekea nchi na JAMII husika.

Nabii Musa kwa Mfano, aliongea na Mungu direct, au kwa maono Kisha akaja kuleta ujumbe wa Mungu kwa watu wa Mungu.

Uandishi pia wa Biblia, wote, ni manabii walipokea neno kwa njia ya kusikia, Kisha wakaandika walichosikia Katika gombo na vitabu mbalimbali ambavyo ndivyo vilivyokusanywa kupata Biblia.

NABII WA MWISHO NI NANI.

Yesu Kristo ameweka wazi, nabii wa Mwisho ni Elia/ Yohana Mbatizaji, na hakuna mwingine baada yake kwa sababu baada ya Yesu kuja, akazaliwa, kufa na kufufuka, hapatatokea nabii mwingine yoyote atakayeleta unabii wowote kinyume na INJILI YA AGANO JIPYA YA KUZALIWA ,KUFA, KUZIKWA NA KUFUFUKA KWAKE YESU KRISTO.

Hivyo ukisikia nabii mwingine yeyote amekuja na kuleta habari tofauti na injili ya ufalme ya YESU KRISTO aliyezaliwa,aliyekufa,akazikwa na kufufuka, huyo ni nabii wa uongo aongozwaye na Roho ya mpinga Kristo.

TAFSIRI YA NABII KATIKA AGANO JIPYA.

Nabii katika Agano jipya ni mtumishi wa Mungu anayehubiri Neno la Mungu kwa nguvu za Roho mtakatifu.

Nabii katika Agano jipya ni yule anayeliamini neno na kuhubiri injili kwa Imani na watu wanaamini na kupokea nguvu na neema ya wokovu.

Kwa Tafsiri hiyo, nabii anaweza kuwa Mchungaji kwa maana, kuhubiri injili kwa kuongozwa na Roho mtakatifu ni sharti kwanza usikie sauti iliyo ndani ya neno la Mungu lililoandikwa, Kisha uipokee Katika Roho Kisha uilete kuwa neno ambalo utalitamka kwa kinywa Kisha likasikiwa na watu kwa sikio la Roho na likapokelewa kwa Imani.

Nabii na unabii Katika Agano jipya ni mtu ndani ya kanisa aliye chini ya mchungaji aliyepewa karama ya unabii, na kama nilivyoeleza hapo juu,

Nabii mwenye karama ya unabii( prophecy) ataena kwa lugha, Mungu atatumia kinywa chake kunena injili na ufunuo juu ya Injili, Kisha atatafsiri alichokisema kwa lugha aliyonena kama ni lugha ya malaika au lugha za wanadamu Ili kulijenga kanisa.

TAFSIRI POTOFU YA NABII KATIKA AGANO JIPYA.

Kuna watu wanapotosha nabii na tafsiri ya Nabii kwa kuchanganya na kitu kiitwacho " Jicho/mwonaji" au "macho ya kinabii/ mwonaji".

Ukisikia mtu anawaambia watu akiwaambia Jana ulikula Nini, au kesho utaenda wapi, au ulizaliwa sehemu Fulani, Umesoma Shule Fulani, au jina la mama yako ni Fulani bila kumwambia, huyo SI nabii, ni sehemu tu ya office ya unabii iitwayo uonaji./ Mwonaji./ Macho ya Roho, sasa huyo SI nabii kamili.

PROPHECY:Is to preach the Gospel with power of The Holly spirit/ spirit of JESUS.

Note: WEWE pia unisomaye Katika thread hii ni nabii ikiwa tu Umeokoka, unaye Roho mtakatifu,na unahubiri injili kwa nguvu za Roho mtakatifu.

Mungu awabariki.

Ikiwa hujampa Yesu maisha Yako fuatisha sala hii:

Ee Mungu katika jina la Yesu Kristo, nina kukiri wewe kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yangu, ninatubu dhambi zangu zote, ninaomba unisamehe, ulifute jina langu katika kitabu cha hukumu, uliandike jina langu katika kitabu cha uzima, nipe uwezo wa kuishi maisha matakatifu, dhambi isinishinde, uovu usinishinde, ulevi usinishinde, uzinzi usinishinde, uchawi usinishinde, ninaomba hayo kupitia jina la Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi wa maisha yangu. Aamin
Baadhi walioa na baadhi Biblia haisemi kama walioa.
 
Ni kweli,

Lakini pia agano la kale, manabii hawakuanzisha au kuongoza hekaluni, walikaa maporini au kuwa watu tu wa kawaida,wanatoa unabii, Kisha kurudi Katika kazi zao
 
Hongera kwa jitihada unazofanya kuelewa haya mambo mkuu. Lakini jitahidi kwenda deep kidogo. Manabii hawakuishi porini na si wote walikuwa wanaishi maisha ya kawaida. Kilichowafanya waishi porini ni tishio la kuuwawa kutokana na ujumbe mzito wa hukumu waliotoa kwa watawala. Kuwa nabii haikuwa kazi rahisi.

Msome nabii Daniel hakuwa na maisha ya kawaida wakati wote. Kuna wakati alikuwa miongoni mwa wanaofanya kazi makao ya mfalme na washauri. Nabii Musa hakuwa na maisha ya kawaida na hata alioa huku kwetu Afrika.

Soma vizuri mkuu utawasilisha jambo lako kwa njia nzuri
 
Umenena vyema,

Umemsahau Yusufu,alikuwa nabii lakini pia Waziri Mkuu Misri. Kama tu Daniel.

Palikuwa na makuhani, lakini nabii hawakufungua makanisa kama hivi Leo.

Musa, Daniel pia hawakukusanya watu kwa ibada hekaluni, Bali walitokea angle ingine kusaidia watu.

Leo Hawa wanaofungua makanisa ni wachunggaji wenye kipawa Cha unabii ndani.
 
Nabii ilikuwa lazima aseme ujumbe aliopewa na Mungu kupitia maono ya moja kwa moja au ndoto. Hao wa sasa ndio wale Yesu alisema watatokea wanashughulika na matumbo yao.
 
Nabii ni yeyote ayaonayo na kuyatabiri yaliyofichwa kwa ajili ya wakati ujao.
 
Habari yako Mtumishi wa Mungu.
Yesu hakusema kwamba Yohana mbatizaji ndiye nabii wa mwisho, Nafikiri umeelewa vibaya ile Luka 7:27 — “Kwa kuwa huyu ndiye nabii aliyeandaliwa, na mimi kusema kweli, hakuna mwingine aliye kama yeye wa kuzaliwa na wanawake.”

Hii inamaanisha Yohana alikuwa nabii wa mwisho kabla ya kuanza kwa utume wa Yesu, lakini si nabii wa mwisho wa milele.

Yesu ndiye aliye mkuu katika unabii wa mwisho na wokovu.
Baada ya Yesu, Biblia inafundisha kwamba hakuna nabii mwingine aliye na mamlaka sawa ya kuokoa wanadamu (Mathayo 17:11–12, Luka 16:16).

Yesu alibainisha kwamba Yohana alikuwa mtangulizi wa Ufalme yaani alitengeneza njia kwa ajili ya Yesu.

Je, unafahamu kwamba Yesu alikuwa na karama zote?

Mwalimu – alifundisha kwa kutumia mifano na mifano ya maisha (Mathayo 7:28–29).

Nabii – alitabiri matukio, akifundisha unabii wa Ufalme wa Mungu (Luka 4:24; Mathayo 21:11).
Kama yeye alikuwa nabii pia, Si kwamba yeye ndiye nabii wa Mwisho?

Mponyaji – aliponya wagonjwa, vipofu, viziwi, na wenye pepo wachafu (Mathayo 9:35).

Mwokozi / Mkombozi – alikuja kuokoa wanadamu kutokana na dhambi na kifo (Yohana 3:16–17).

Mufufua wafu – aliamsha wafu, ikiwemo Lazaro (Yohana 11:43–44).

Mtendaji wa miujiza – miujiza mingi, ikiwemo kugawa mikate, kutembea juu ya maji (Mathayo 14:25–33).

Mlezi wa kiroho – aliweka mifumo ya kuishi kwa Roho, mafundisho ya Baba Yetu, matunda ya Roho (Luka 11; Wagalatia 5:22–23).

Yesu alikuja kutoa mfano wa Jinsi ya kuishi katika mapenzi yake kwa kila mwenye karama hiyo na kwa kupitia kauli yake kwenye Yohana.

“Mimi ndiyo njia, ukweli, na uzima; hakuna anayefika kwa Baba ila kwa mimi” (Yohana 14:6).

Tunajifunza ya kwamba Yesu kristo ndiye nabii wa Mwisho hakuna mwingine kwa maana yeye ndiye Njia, Kweli na Uzima.
 
Umenena vyema,

Umemsahau Yusufu,alikuwa nabii lakini pia Waziri Mkuu Misri. Kama tu Daniel.

Palikuwa na makuhani, lakini nabii hawakufungua makanisa kama hivi Leo.

Musa, Daniel pia hawakukusanya watu kwa ibada hekaluni, Bali walitokea angle ingine kusaidia watu.

Leo Hawa wanaofungua makanisa ni wachunggaji wenye kipawa Cha unabii ndani.
Nakutafuta ndugu Rabbon,
 
Habari yako Mtumishi wa Mungu.
Yesu hakusema kwamba Yohana mbatizaji ndiye nabii wa mwisho, Nafikiri umeelewa vibaya ile Luka 7:27 — “Kwa kuwa huyu ndiye nabii aliyeandaliwa, na mimi kusema kweli, hakuna mwingine aliye kama yeye wa kuzaliwa na wanawake.”

Hii inamaanisha Yohana alikuwa nabii wa mwisho kabla ya kuanza kwa utume wa Yesu, lakini si nabii wa mwisho wa milele.

Yesu ndiye aliye mkuu katika unabii wa mwisho na wokovu.
Baada ya Yesu, Biblia inafundisha kwamba hakuna nabii mwingine aliye na mamlaka sawa ya kuokoa wanadamu (Mathayo 17:11–12, Luka 16:16).

Yesu alibainisha kwamba Yohana alikuwa mtangulizi wa Ufalme yaani alitengeneza njia kwa ajili ya Yesu.

Je, unafahamu kwamba Yesu alikuwa na karama zote?

Mwalimu – alifundisha kwa kutumia mifano na mifano ya maisha (Mathayo 7:28–29).

Nabii – alitabiri matukio, akifundisha unabii wa Ufalme wa Mungu (Luka 4:24; Mathayo 21:11).
Kama yeye alikuwa nabii pia, Si kwamba yeye ndiye nabii wa Mwisho?

Mponyaji – aliponya wagonjwa, vipofu, viziwi, na wenye pepo wachafu (Mathayo 9:35).

Mwokozi / Mkombozi – alikuja kuokoa wanadamu kutokana na dhambi na kifo (Yohana 3:16–17).

Mufufua wafu – aliamsha wafu, ikiwemo Lazaro (Yohana 11:43–44).

Mtendaji wa miujiza – miujiza mingi, ikiwemo kugawa mikate, kutembea juu ya maji (Mathayo 14:25–33).

Mlezi wa kiroho – aliweka mifumo ya kuishi kwa Roho, mafundisho ya Baba Yetu, matunda ya Roho (Luka 11; Wagalatia 5:22–23).

Yesu alikuja kutoa mfano wa Jinsi ya kuishi katika mapenzi yake kwa kila mwenye karama hiyo na kwa kupitia kauli yake kwenye Yohana.

“Mimi ndiyo njia, ukweli, na uzima; hakuna anayefika kwa Baba ila kwa mimi” (Yohana 14:6).

Tunajifunza ya kwamba Yesu kristo ndiye nabii wa Mwisho hakuna mwingine kwa maana yeye ndiye Njia, Kweli na Uzima.
Yesu SI nabii.

Nabii wa mwisho ni Elia/Yohana Mbatizaji.

Yesu ni Mungu aliyekuja Katika mwili wa Mwanadamu, akazaliwa, AKAFA, akazikwa na kufufuka siku ya tatu.

Ndiye aketiye Katika kiti Cha Enzi.

Paulo alikutana naye akiwa Katika utukufu wake, akawa kipofu hapo hapo.

Soma kwa ufahamu ndugu.
 
Yesu ni Mungu.

Yesu anakuja duniani kama mwanadamu akiwa na karama zote ikiwemo karama ya Unabii.

Yesu ni nabii wa mwisho duniani kwasababu alikua na Sifa zote za kinabii.

Tatizo watu wengi wameathiriwa na ubishi wa kidini (Haswa waislamu wanaodai Yesu si Mungu bali ni nabii tu).

Yesu alikuja kama binadamu duniani akijinyenyekesha kama binadamu akiwa na karama zote za kibinadamu ikiwemo ya unabii.

Ukiachana na Uungu wake Yesu.
Yesu ni nabii pia kwasababu alitoa unabii ambao hata leo unatimia.
Yesu ni mtume pia.
Yesu ni mchungaji pia.
Yesu ni mwalimu pia.
Yesu ni mponyaji pia.
Yesu ni mkombozi.

Kila mtume, kila mchungaji na kila mwalimu lazima afuate mfano alioachiwa na Yesu katika kazi yake hiyo.
 
According to the scripture,

Nabii wa mwisho ni Elia/ Yohana Mbatizaji.

Yesu ni alfa na omega, mwanzo na mwisho Katika Kila kitu, unabii ,ualimu, ufalme,uongozi, karama, nk nk nk.

Mungu ni mmoja tu, na jina la Mungu huyo mmoja aliyekuja Katika mwili wa Mwanadamu ni Yesu Kristo/ Yeshua Hamashiach.

Aamin
 
Amefanya kazi za kinabii pia.
 
Amefanya kazi za kinabii pia.
Kufanya kazi ya kinabii SI kuwa nabii wa mwisho.

Yesu ndiye unabii wenyewe maana Yeye ndiye NENO. Unabii unatoka Katika kinywa Cha NENO, na NENO la Mungu ndiye Yesu .

Sasa kumwita Mungu nabii , SI sawa.
 
Mathayo 23:33-34
[33]Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?

[34]Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;

Kama Mungu hataleta nabii ili atupe mwanga hukumu haitakuwa ya haki kwa sababu wengine aliwatumia watu wakuwaongoza.
Uzuri Mungu alimtuma yohana wa kizazi hiki ( William Marion Branham)
Branham ni nabii wa uongo
 
Back
Top Bottom