Hii ndiyo hasa tafsiri ya Nabii Katika Agano Jipya

Hii ndiyo hasa tafsiri ya Nabii Katika Agano Jipya

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,938
Reaction score
41,098
Salaam, Shalom!

Palikuwepo manabii wengi Katika agano la kale, mfano Adam, Nuhu, Musa, Elia, Nehemiah, Daniel nk nk.

NABII katika Agano la kale na kuishia kwa Yohana Mbatizaji,waliishi maporini kujitenga na UOVU kuepuka kuona, kusikia UOVU Katika mikusanyiko ya watu, ingawa SI wote, manabii hawakuoa ingawa baadhi walioa, hawakujenga au kuanzisha makanisa kama sasa, ukiona mtu anajenga nyumba ya ibada na kuhudumia watu, huyo ni mchungaji mwenye karama ya unabii, Mungu akimwita nabii akafungue kanisa, huyo ni mchungaji lakini ndani ana karama ya unabii.

TAFSIRI YA NABII.

Nabii ni mtu aliyeteuliwa na Mungu , mtu huyo, kinywa chake, Mungu hukitumia kunena yatokayo kwa Mungu, kuelekea nchi na JAMII husika.

Nabii Musa kwa Mfano, aliongea na Mungu direct, au kwa maono au kupitia ndoto Kisha akaja kuleta ujumbe wa Mungu kwa watu wa Mungu.

Uandishi pia wa Biblia, wote, ni manabii walipokea neno kwa njia ya kusikia,maono au ndoto Kisha wakaandika walichosikia Katika gombo na vitabu mbalimbali ambavyo ndivyo vilivyokusanywa kupata Biblia.

NABII WA MWISHO NI NANI.

Yesu Kristo ameweka wazi, nabii wa Mwisho ni Elia/ Yohana Mbatizaji, na hakuna mwingine baada yake kwa sababu baada ya Yesu kuja, akazaliwa, kufa na kufufuka, hapatatokea nabii mwingine yoyote atakayeleta unabii wowote kinyume na INJILI YA AGANO JIPYA YA KUZALIWA ,KUFA, KUZIKWA NA KUFUFUKA KWAKE YESU KRISTO.

Hivyo ukisikia nabii mwingine yeyote amekuja na kuleta habari tofauti na injili ya ufalme ya YESU KRISTO aliyezaliwa,aliyekufa,akazikwa na kufufuka, huyo ni nabii wa uongo aongozwaye na Roho ya mpinga Kristo.

TAFSIRI YA NABII KATIKA AGANO JIPYA.

Nabii katika Agano jipya ni mtumishi wa Mungu anayehubiri Neno la Mungu kwa nguvu za Roho mtakatifu. Ni aliletaye neno kutoka kuandikika, likatamkika na kuwa hai na kuleta matokeo halisi.

Nabii katika Agano jipya ni yule anayeliamini neno na kuhubiri injili kwa Imani na watu wanaamini na kupokea nguvu na neema ya wokovu.

Kwa Tafsiri hiyo, nabii anaweza kuwa Mchungaji kwa maana, kuhubiri injili kwa kuongozwa na Roho mtakatifu ni sharti kwanza usikie sauti iliyo ndani ya neno la Mungu lililoandikwa, Kisha uipokee Katika Roho Kisha uilete kuwa neno ambalo utalitamka kwa kinywa Kisha likasikiwa na watu kwa sikio la Roho na likapokelewa kwa Imani.

Nabii na unabii Katika Agano jipya ni mtu ndani ya kanisa aliye chini ya mchungaji aliyepewa karama ya unabii, na kama nilivyoeleza hapo juu,

Nabii mwenye karama ya unabii( prophecy) ataena kwa lugha, Mungu atatumia kinywa chake kunena injili na ufunuo juu ya Injili, Kisha atatafsiri alichokisema kwa lugha aliyonena kama ni lugha ya malaika au lugha za wanadamu Ili kulijenga kanisa.

TAFSIRI POTOFU YA NABII KATIKA AGANO JIPYA.

Kuna watu wanapotosha nabii na tafsiri ya Nabii kwa kuchanganya na kitu kiitwacho " Jicho/mwonaji" au "macho ya kinabii/ mwonaji".

Ukisikia mtu anawaambia watu akiwaambia Jana ulikula Nini, au kesho utaenda wapi, au ulizaliwa sehemu Fulani, Umesoma Shule Fulani, au jina la mama yako ni Fulani bila kumwambia, huyo SI nabii, ni sehemu tu ya office ya unabii iitwayo uonaji./ Mwonaji./ Macho ya Roho, sasa huyo SI nabii kamili.

PROPHECY:Is to preach the Gospel with power of The Holly spirit/ spirit of JESUS.

Note: WEWE pia unisomaye Katika thread hii ni nabii ikiwa tu Umeokoka, unaye Roho mtakatifu,na unahubiri injili kwa nguvu za Roho mtakatifu.

Mungu awabariki.

Ikiwa hujampa Yesu maisha Yako fuatisha sala hii:

Ee Mungu katika jina la Yesu Kristo, nina kukiri wewe kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yangu, ninatubu dhambi zangu zote, ninaomba unisamehe, ulifute jina langu katika kitabu cha hukumu, uliandike jina langu katika kitabu cha uzima, nipe uwezo wa kuishi maisha matakatifu, dhambi isinishinde, uovu usinishinde, ulevi usinishinde, uzinzi usinishinde, uchawi usinishinde, ninaomba hayo kupitia jina la Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi wa maisha yangu. Aamin
 
Nabii Nuhu:

Mwanzo 6:13,14.....)

13:Mungu akamwambia Nuhu, mwisho wa Kila mwenye mwili imekuja mbele ZANGU...

14: Ujifanyie safina ya mti wa mvinje.

... Mwisho wa kunukuu...

Hapo unaona nabii Nuhu anaongea na Mungu wakiwa pekeao faraghani, anaambiwa ujumbe unaoingia KUPITIA sikio, anatunza moyoni, Kisha anaulleta kwa watu kuwashauri kujenga safina.

Tunaona hapo Nabii hazungumzi jambo la mtu mmoja, nabii huzungumza mambo mkubwa Katika level ya nchi kidunia au ujumbe wa kujenga kanisa zima utikao kwa Mungu au maonyo ya Mungu kwa wananchi wakaao duniani au nchini au Katika kanisa au ibadani.
 
NABII MUSA.

(Kutoka 3:2-10)

Mungu anamtokea Musa KUPITIA malaika aliyejigeuza kuwa kijiti kiwakacho moto na hakiteketei,

Mungu anasema na NABII MUSA kumwambia aende kwa Mfalme Farao Ili awatoe taifa lake Israel kutoka utumwani Misri.

Hapo utaona, nabii anatumwa Katika level ya Taifa, SI kwa mtu mmoja pekee.
 
Sawa. Hapo umeeleza kwa sehemu tu maana huwezi kufahamu kila kitu. Kuna tofauti ya Nabii na Unabii.
Nabii na unabii.

Prophet na Prophecy.

Nabii ni mtu,

Unabii ni kile kitokacho Katika kinywa Cha Mungu KUPITIA kinywa Cha nabii.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Tofauti kati ya NABII NA MWONAJI.

MWONAJI: (1 Samwel 9:1-10)

Sauli anapoteza punda wa kuazima, wanatafuta Hadi wanachoka, wanaafikiana kwenda kwa Mwonaji( mtu wa Mungu).

9: Hapo zamani Katika Israel,mtu alipokwenda kuuliza neno kwa Mungu, husema hivi, Haya! Twende kwa Mwonaji; maana mtu aitwaye sasa Nabii hapo zamani aliitwa mwonaji.

NB: SI Kila Nabii ni mwonaji, na SI Kila mwonaji ni nabii, ila Mwonaji anaweza pia kuwa nabii wakati huo huo.

Kuna mwonaji pia Katika ufalme wa Giza( sangoma).

Pia Pana mwonaji ufalme wa Mungu ( nabii ndani ya kanisa).

Karama ya unabii wana wa Mungu waombe na watapewa Ili kulijenga kanisa.

Aamen
 
Mwonaji Katika ufalme wa Giza.

(Matendo ya mitume 16:17)

16: Kijakazi mmoja alikuwa na Pepo wa uaguzi,akatukuta, aliyewapatia BWANA zake faida nyingi kwa kuagua.

Alipomwona Paulo,akawatambua kuwa ni watumishi wa Mungu aliye juu.

Sasa wana wa Mungu, ni marufuku kwenda kuchumgulia hatma zao kwa waonaji walio Katika ufalme wa Giza.
 
Mtu yeyote anayehubiri NENO ni Nabii.
Ndio ni nabii,

Ikiwa tu anahubiri kwa kusoma na kuusikia sauti iliyo ndani ya neno llililoandikwa ( Biblia). Na awe amejazwa Roho mtakatifu amsaidiaye kuhubiri kwa nguvu ilitayo mvuto Katika MAISHA ya watu watubu DHAMBI na kuokolewa. Huyo ni nabii.

Aamin
 
Ameen.
 
Ukisikia mtu anakusanya watu, anamwita mmoja au anapokea simu na kuanza kukwambia ukweli wote kuhusu MAISHA Yako huyo SI nabii,

Huyo ni mwonaji, mwenye jicho la Roho.

Na jicho Hilo Katika ulimwengu wa Nuru haliendani na kutoza watu pesa Ili akwambie mambo yako au akusaidie.

Mtu abayetoza pesa ni mganga wa kienyeji ,mwonaji wa Giza.

Karama za Mungu hutolewa Bure, hazilipiwi pesa, kwamba mwenye milioni moja aje ofisini nimtabirie, mwenye elfu kumi ataandika kwenye notebook na kutupia kwenye kasha la maombezi, hii SI sawa, na huo SI unabii sawasawa na neno la Mungu
 
Unabii mkubwa kuliko wote agano jipya ni kuvua Roho za waliopotea na kuwaleta kwa Kristo Yesu.

Hawa matapeli wanaoita watu na kuwapuna pesa zao ni manabii feki, ni fake sababu hauwezi kuwasikia wakiwaita watu kuacha DHAMBI, kuokoka na kuacha UOVU Ili wazaliwe upya.

Nabii wa kweli Katika Agano jipya ni yule amalizapo kuhubiri au kuhutubu, Kisha akawaita watu wapya waje kuokoka au waliookoka kuja kutengeneza na Mungu wao.

Hapo ni rahisi sasa kumjua nabii ni nani na ukimtifautisha na mganga mvaa suti.
 
Mwalimu na Nabii Mathanzua kazi yako ya kufundisha na kuhubiri injili Mungu anaithamini sana.

Ubarikiwe
 
Yesu Kristo ameweka wazi, nabii wa Mwisho ni Elia/ Yohana Mbatizaji, na hakuna mwingine baada yake
Kuna manabii wakubwa na manabii wadogo. Manabii wadogo kadhaa waliendelea kuwepo hata baada ya Yohana Mbatizaji..

Mfano:
Matendo ya Mitume 21:
10 Basi tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Uyahudi.

11 Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa.
 
Nakubaliana nawe maana umequote neno la Mungu.

Manabii wapo hata Leo, ila hawawezi kuja na unabii tofauti na kuzaliwa,kufa na kufufuka kwa Yesu.

Lazima manabii hao ikiwa ni wa kweli, watoe unabii wa kumtukuza Yesu na kumkiri kuwa ni Mungu aliyekuja Katika mwili wa Mwanadamu.

Na unabii wao ulenge kulijenga kanisa. SI kulenga maslah binafsi kwa kulipisha watu pesa Katika kuwahudumia.
 
Mathayo 23:33-34
[33]Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehanum?

[34]Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji;
Salaam, Shalom!

Palikuwepo manabii wengi Katika agano la kale, mfano Adam, Nuhu, Musa, Elia, Nehemiah, Daniel nk nk.

NABII katika Agano la kale na kuishia kwa Yohana Mbatizaji,waliishi maporini kujitenga na UOVU kuepuka kuona, kusikia UOVU Katika mikusanyiko ya watu, manabii hawakuoa, hawakujenga au kuanzisha makanisa kama sasa, ukiona mtu anajenga nyumba ya ibada na kuhudumia watu, huyo ni mchungaji mwenye karama ya unabii, Mungu akimwita nabii akafungue kanisa, huyo ni mchungaji lakini ndani ana karama ya unabii.

TAFSIRI YA NABII.

Nabii ni mtu aliyeteuliwa na Mungu , mtu huyo, kinywa chake, Mungu hukitumia kunena yatokayo kwa Mungu, kuelekea nchi na JAMII husika.

Nabii Musa kwa Mfano, aliongea na Mungu direct, au kwa maono Kisha akaja kuleta ujumbe wa Mungu kwa watu wa Mungu.

Uandishi pia wa Biblia, wote, ni manabii walipokea neno kwa njia ya kusikia, Kisha wakaandika walichosikia Katika gombo na vitabu mbalimbali ambavyo ndivyo vilivyokusanywa kupata Biblia.

NABII WA MWISHO NI NANI.

Yesu Kristo ameweka wazi, nabii wa Mwisho ni Elia/ Yohana Mbatizaji, na hakuna mwingine baada yake kwa sababu baada ya Yesu kuja, akazaliwa, kufa na kufufuka, hapatatokea nabii mwingine yoyote atakayeleta unabii wowote kinyume na INJILI YA AGANO JIPYA YA KUZALIWA ,KUFA, KUZIKWA NA KUFUFUKA KWAKE YESU KRISTO.

Hivyo ukisikia nabii mwingine yeyote amekuja na kuleta habari tofauti na injili ya ufalme ya YESU KRISTO aliyezaliwa,aliyekufa,akazikwa na kufufuka, huyo ni nabii wa uongo aongozwaye na Roho ya mpinga Kristo.

TAFSIRI YA NABII KATIKA AGANO JIPYA.

Nabii katika Agano jipya ni mtumishi wa Mungu anayehubiri Neno la Mungu kwa nguvu za Roho mtakatifu.

Nabii katika Agano jipya ni yule anayeliamini neno na kuhubiri injili kwa Imani na watu wanaamini na kupokea nguvu na neema ya wokovu.

Kwa Tafsiri hiyo, nabii anaweza kuwa Mchungaji kwa maana, kuhubiri injili kwa kuongozwa na Roho mtakatifu ni sharti kwanza usikie sauti iliyo ndani ya neno la Mungu lililoandikwa, Kisha uipokee Katika Roho Kisha uilete kuwa neno ambalo utalitamka kwa kinywa Kisha likasikiwa na watu kwa sikio la Roho na likapokelewa kwa Imani.

Nabii na unabii Katika Agano jipya ni mtu ndani ya kanisa aliye chini ya mchungaji aliyepewa karama ya unabii, na kama nilivyoeleza hapo juu,

Nabii mwenye karama ya unabii( prophecy) ataena kwa lugha, Mungu atatumia kinywa chake kunena injili na ufunuo juu ya Injili, Kisha atatafsiri alichokisema kwa lugha aliyonena kama ni lugha ya malaika au lugha za wanadamu Ili kulijenga kanisa.

TAFSIRI POTOFU YA NABII KATIKA AGANO JIPYA.

Kuna watu wanapotosha nabii na tafsiri ya Nabii kwa kuchanganya na kitu kiitwacho " Jicho/mwonaji" au "macho ya kinabii/ mwonaji".

Ukisikia mtu anawaambia watu akiwaambia Jana ulikula Nini, au kesho utaenda wapi, au ulizaliwa sehemu Fulani, Umesoma Shule Fulani, au jina la mama yako ni Fulani bila kumwambia, huyo SI nabii, ni sehemu tu ya office ya unabii iitwayo uonaji./ Mwonaji./ Macho ya Roho, sasa huyo SI nabii kamili.

PROPHECY:Is to preach the Gospel with power of The Holly spirit/ spirit of JESUS.

Note: WEWE pia unisomaye Katika thread hii ni nabii ikiwa tu Umeokoka, unaye Roho mtakatifu,na unahubiri injili kwa nguvu za Roho mtakatifu.

Mungu awabariki.

Ikiwa hujampa Yesu maisha Yako fuatisha sala hii:

Ee Mungu katika jina la Yesu Kristo, nina kukiri wewe kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yangu, ninatubu dhambi zangu zote, ninaomba unisamehe, ulifute jina langu katika kitabu cha hukumu, uliandike jina langu katika kitabu cha uzima, nipe uwezo wa kuishi maisha matakatifu, dhambi isinishinde, uovu usinishinde, ulevi usinishinde, uzinzi usinishinde, uchawi usinishinde, ninaomba hayo kupitia jina la Yesu Kristo aliye Bwana na Mwokozi wa maisha yangu. Aamin

Kama Mungu hataleta nabii ili atupe mwanga hukumu haitakuwa ya haki kwa sababu wengine aliwatumia watu wakuwaongoza.
Uzuri Mungu alimtuma yohana wa kizazi hiki ( William Marion Branham)
 
Back
Top Bottom