Hii ndio shule yenye ada kubwa zaidi duniani

FM facts

Member
Mar 16, 2019
45
88
Inaitwa La Rosey
Shule hii ipo Rolle Kaskazini Mashariki mwa Switzerland Ilianzishwa Mwaka1880 na Mwanzikishi ni Paul-Emile Carnal, Ni shule yenye Wanafunzi 420 Kwasasa na Walimu Karibia 200. Inafundisha Kuanzia Elimu ya Shule ya Msingi, Elimu ya Sekondary na Diploma ya Masomo Mbalimbali.

Mmiliki wa Shule hii Wasasa ni Philippe Gudin, Mkuu wa Shule ni Michael Gray na Director ni Christophe Gudin.

Eneo la Shule lina Ukubwa wa Ekari 69 au 0.243 KM² Sawa na Ukubwa wa Nchi ya Vatican na Limegawanyika Katika Sehemu mbili, Upande wa Mabweni ya Wavulana na Upande wa Mabweni ya Wasichana na Inafundisha zaidi ya Lugha 30 katika Elimu ya Msingi na Baadae Unamua Uendelee na Lugha Zipi Mbili (Wengi Huchagua English na French).

Shule ina Vyumba vya Kulala 179 Vya Wanafunzi Vyenye Bafu ndani, Madarasa 53, Maabara 8 za Mazoezi na Nyingine 14 zenye Vifaa vya Kisayansi, Apartments 48 za Kuishi Walimu, Maktaba 2 zenye Zaidi ya Vitabu 30,000 na Vifaa vya Mazoezi Stadi, Kumbi 2 za Chakula na Kumbi 2 za Gym na Vifaa vingine vya Michezo na Kuna Vingine Vingi ambavyo Sijavitaja hapa.

Kuna Viwanja 10 vya Tennis, Mabwawa ya Kuogelea 25 ndani na 25 nje, Viwanja 3 vya Mpira wa Miguu N.K.
Kutoka Upande wa Wasichana Kwenda upande wa Wavulana Unapanda Treni la Shule.

Ada yake Kwa Ujumla ni Shs. Millions 368 za Tanzania (Dollar 157,000) kwa Mhula Mmoja (Nusu Mwaka), Hapo Ushalipia Tuition Pamoja na Vifaa vya Michezo e.t.c.

Sheria za Nchi hiyo Hazimruhuru Mwalimu/ Mfanyakazi yeyote Anaetoka Nje ya Ulaya Kuomba Kazi Katika Shule hii. Lazima uwe Mkazi wa Ulaya.

Website ya Shule Welcome to Le Rosey
SIMU: +41 21 822 55 00

Kama wewe ni Mwalimu na Huna Ajira, Omba kazi Katika Shule hii Hapa Employment... Na Utume Maombi yako Kwenda Kwa E-Mail hii job@rosey.ch

Kama Unahitaji Kwenda Kusoma Huko ingia Hapa How to ?
NB:Uwe na Umri wa Miaka 8-12, na Kama Umefika 15 basi Uwe Unajua Vizuri French na English.

Fomu ya Kujiunga Ipakue Hapa https://webdevsrv.rosey.ch/Ec2Inscrip?LNG=UK
Kuripoti Shuleni ni Mwezi wa 9-11.

HAYA JAMANI KAZI YANGU MIMI NIMEMALIZA, KAZI KWAKO!.

images-1.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1054529

Sent using Jamii Forums mobile app

kwakweli umemaliza.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ngoja nimuhamishie mwanangu huko,kumbe hapa IST kwenye tuada twa tumilioni 37 kwa mwaka ni cha mtoto,inaonekana hata elimu yao ni next level huko,akitoka atarusha ndege,ataendesha meli,atakuwa mtalaalam mbobez sana ktka masuala atakayoyasomea
 
Niliona documentary ya shule ya private Uingereza nimesahau jina. Ada ni £100,000 kwa mwaka. Watoto darasani ni 25, kipindi ni dakika 90 na kati kati ya kipindi mnapewa chai au kahawa na biscuti.
Mwalimu ana muda wa kukaa na kila mtoto kuangalia perfomance yake.

Breakfast unachagua, cooked breakfast yenye mayai, bacon, sausages au cornflakes.

Mchana ni three course meal pamoja na usiku.

Kuna walimu wa michezo, rugby, football, ni sehemu ya masomo

kulala ni wawili wawil kila chumba, mkiwa darasani ma haouse keeper wanakuja kutandika vitanda na kuosha vyumba, bafu na vyoo.
 
Nadhani mwanafunzi akihitimu hapo atakuwa anafahamu kila kitu kwenye ulimwengu huu....
 
Back
Top Bottom