Hii ndio picha halisi ya Yesu

Hii ndio picha halisi ya Yesu

Watu wengi hutamani kumuona Yesu. Wanajiuliza, “Alikuwa na sura gani? Alionekana vipi? Alikuwa mtu wa namna gani?” Wengine hujaribu kutengeneza picha kwa mawazo, ndoto au sanaa. Lakini kuna njia moja ya uhakika ya kumuona Yesu kwa macho ya kweli ya rohoni kupitia Neno lake.

Ni kama vile unavyosoma riwaya nzuri: kadri unavyosoma, unamjengea mhusika sura kichwani mwako. Unaweza kumjua tabia yake, namna anavyotembea, anavyocheka, anavyopenda au kuchukia yote haya yanajitokeza kupitia maneno.

Hali ni hiyo hiyo kwa Yesu.

Ukisoma Biblia kwa moyo wa kujifunza na kuelewa, utamwona Yesu ndani ya kila ukurasa. Si kwa macho ya nyama, bali kwa macho ya roho. Utaanza kuona:

1. Yesu mwenye huruma kwa walioteseka

2. Yesu mwenye msamaha kwa waliomkosea

3. Yesu mwenye nguvu dhidi ya dhambi na kifo

4. Yesu mwaminifu, mpole, na mwenye mamlaka

Na mwisho wa yote, picha hiyo itaanza kuchorwa pia ndani ya moyo wako.

Yesu si simulizi tu, ni Neno hai. Ukisoma Biblia, si tu unamjua bali unamwona, unamgusa kwa imani, na maisha yako hubadilika milele.

“Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu...” (Yohana 1:14)

Leo, chukua muda wako. Fungua Biblia. Mkaribishe Roho Mtakatifu. Na utamwona Yesu sura yake, tabia yake, na upendo wake.

Picha ya Yesu haijachorwa kwa mikono ya binadamu, bali ndani ya Neno la Mungu.
Ubarikiwe 🙏

Picha ya Yesu imefutwa tusiione wanadamu Katika macho ya nyama, Bali Katika Roho.

Sura ya Yesu ni Sura ya Mungu mwenyewe!
 
Upo nyuma kimaendeleo. Kwa mara ya kwanza nilimsoma Yesu kwenye kitabu ya Historia cha form five na six. Kitabu kiliezea matukio yote ya historia mpaka vita ya pili ya dunia.
Kusoma kitu kwenye kitabu haimaanishi kwamba kitu hicho kina exist kwenye uhalisia.

Hata Dragons 🐉 watemao moto midomoni mwao tuliwasoma kwenye vitabu, lakini hawapo kwenye uhalisia.

Hata Vampires tunawasoma kwenye vitabu ila kwenye uhalisia hawapo.

Vivyo hivyo, Huyo Yesu wako ni fictional character wa vitabuni tu. Hayupo kwenye uhalisia.

Yesu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.
 
Ukifikiria Kwa undani hutapata picha.
ILa amini kwamba hakuna mtu mwili aliepata mateso ndani ya masaa kumi na mbili Hadi kifo kama yeye YESU .Na hatokuja atokee Hadi mwisho wa dahari,
Tumsifu yesu kristu
 
Kusoma kitu kwenye kitabu haimaanishi kwamba kitu hicho kina exist kwenye uhalisia.

Hata Dragons 🐉 watemao moto midomoni mwao tuliwasoma kwenye vitabu, lakini hawapo kwenye uhalisia.

Hata Vampires tunawasoma kwenye vitabu ila kwenye uhalisia hawapo.

Vivyo hivyo, Huyo Yesu wako ni fictional character wa vitabuni tu. Hayupo kwenye uhalisia.

Yesu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.
Ukitaka kuelewa Dragon nenda kawaulize wachina ndio wanaelewa kuhusu dragon ukiangalia kwenye movie utadanganyika. Dragon yupo kwenye tamaduni za wachina.
 
Yesu hajawahi kuwepo hayupo na hatakaa awepo.

Yesu ni fictional character. Ndio maana hakuna picha halisi ya Yesu.

Kuna picha za waigizaji wa Uingereza Brian Deacon na Robert Powell walio igiza filamu ya Yesu kuhadaa wajinga.

Hakuna Yesu.

Hakuna Mungu.
FB_IMG_1743227021303.jpg
 
Ukitaka kuelewa Dragon nenda kawaulize wachina ndio wanaelewa kuhusu dragon ukiangalia kwenye movie utadanganyika. Dragon yupo kwenye tamaduni za wachina.
Kwenye tamaduni wapi?

Sehemu gani?

Hakuna Dragons 🐉 kwenye uhalisia. Dragons wapo vitabuni tu.

Dragon 🐲 ni myths tu.

Vivyo hivyo, Huyo Yesu wenu ni myths tu wa kwenye vitabu.

Yesu hajawahi kuwepo na hayupo.
 
Yesu hajawahi kuwepo hayupo na hatakaa awepo.

Yesu ni fictional character. Ndio maana hakuna picha halisi ya Yesu.

Kuna picha za waigizaji wa Uingereza Brian Deacon na Robert Powell walio igiza filamu ya Yesu kuhadaa wajinga.

Hakuna Yesu.

Hakuna Mungu.
View attachment 3309852
Chukua biblia yako anza kusoma utakutana na Yesu wala usiangaike.
 
Yesu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Huyo Yesu ni sawa na Abunuwasi wa kwenye hekaya.

Hekaya za Biblia= Hekaya za Abunuwasi.

Yesu= Abunuwasi.

Fictional characters.

Imaginations just an illusion.
Kabisa hizi hadithi za mtu kuzaliwa na bikira na kufa siku ya tatu kufufuka ni hadithi za abunuasi ambazo misri ya kale , Greek , mesapotania , na India zilikuwepo tangu kale mno , Constantine wa roma ya kale aliwaweza kweli
 
Back
Top Bottom