Hii ndio Passport ya Afrika iliyozinduliwa Rwanda

Wadau kwa heshima na taadhima naombeni nijuzwe na wengine wenye uelewa wa kariba kama yangu;

1. Nini hasa hii passport ya Africa
2. Ni lini nchi wanachama walikaa hasa mabunge ya Africa kama wawakilishi wa watu
wao kuidhinisha uanzishwaji wa passport.


3. Manufaa husika
4. Vipi mambo mengine mtambuka kama usalama wa nchi husika
5. hii ina maana kwa passport hii naweza hamia Burundi ( kwa mfano) na nikaishi huko bila bugudha


Ni wengi hatukufuatilia uanzishwaji wake naomba nifahamishwe na kwa kupigitia kwangu wapo wengi watanufaika na majibu yenu adhimu enyi wajuvi wa mambo ya Kiplomasia
 
Ni jambo jema ijapokuwa bado kuna changamoto nyingi sana hasa ukienda nchi nyingine maeneo ya boda
 
Mgirik, post: 16881331, member: 139246"]Inamaana walibya, wamisri,wasomali,wasudan kusini, wote waingie Tz? Mmh! Tutaumia
hiyo ni pasi tu. Lazima mtu apate viza. Hapo ndo control itakapokuwepo.
 
Wanaoshupalia hilo ni zile nchi ambazo unaweza kuzizunguka kwa baiskeli kwa nusu saa tu kwa sababu wanajua raia wao hawana ardhi ya kufanya chughuli za kilimo, ufugaji na ujenzi wa nyumba za makazi na viwanda.

Wewe nchi yako yenye mapori kila pahala mmeweza kuitumia hiyo ardhi? Uoga unalimaliza hili taifa
 
160717145245_au_passport_cu_549x549_bbc.jpg

Image captionBara la Afrika limezindua rasmi cheti chake cha kusafiria!

Je unamiliki cheti cha kusafiria cha taifa lako?

Hivi Karibuni, itakuwa hauhitaji cheti hicho madamu wewe ni mwafrika !

Kisa na maana ,,,, Bara la Afrika limezindua rasmi cheti chake cha kusafiria!

Madhumuni ya AU umoja wa Afrika kuzindua cheti hicho ni kuvunja mipaka iliyowekwa na mkoloni alipoigawanya Afrika ilikuitawala katika karne iliyopita.

160717143700_au_passport_512x288_bbc_nocredit.jpg

Image captionViongozi wa kwanza kupewa cheti hicho ni rais mwenyeji wa kongamano hilo Paul Kagame wa Rwanda na mwenzake wa Chad rais Idris Deby.
Viongozi wa kiafrika wamezindua cheti hicho maalum mjini Kigali Rwanda katika kongamano la viongozi wa Afrika.

Wakwanza kupewa cheti hicho watakuwa ni viongozi wenye hadhi ya kupewa vyeti vya kidiplomasia.

Viongozi wa kwanza kupewa cheti hicho ni rais mwenyeji wa kongamano hilo Paul Kagame wa Rwanda na mwenzake wa Chad rais Idris Deby.

160717145512_au_passport_cu_624x415_bbc.jpg

Image captionMadhumuni ya AU umoja wa Afrika kuzindua cheti hicho ni kuvunja mipaka iliyowekwa na mkoloni alipoigawanya Afrika ilikuitawala katika karne iliyopita.
Marais wote waliohudhuria kongamano hilo watapewa cheti hicho cha AU kabla ya kukamilika kwa mkutano huo.

Mawaziri wa maswala ya kigeni na viongozi wakuu katika umoja wa Afrika pia wanatarajiwa kufaidi cheti hicho cha kusafiria.

Umoja wa Afrika unatarajia kuwa mataifa ya kiafrika yataanza kutoa vyeti hivyo vipya vya usafiri kufikia mwaka wa 2018.

Hivi ile passport ya East Africa bado inatumika??? Mimi ninayo ila sijawahi kuitumia...
 
Kwa ukiwa na passport hiyo hahuitaji viza kuingiaaa kwenye nchi ambayo unatarajia kwendaa?au
 
Back
Top Bottom