Hii ndio Passport ya Afrika iliyozinduliwa Rwanda

160717145245_au_passport_cu_549x549_bbc.jpg

Image captionBara la Afrika limezindua rasmi cheti chake cha kusafiria!

Je unamiliki cheti cha kusafiria cha taifa lako?

Hivi Karibuni, itakuwa hauhitaji cheti hicho madamu wewe ni mwafrika !

Kisa na maana ,,,, Bara la Afrika limezindua rasmi cheti chake cha kusafiria!

Madhumuni ya AU umoja wa Afrika kuzindua cheti hicho ni kuvunja mipaka iliyowekwa na mkoloni alipoigawanya Afrika ilikuitawala katika karne iliyopita.

160717143700_au_passport_512x288_bbc_nocredit.jpg

Image captionViongozi wa kwanza kupewa cheti hicho ni rais mwenyeji wa kongamano hilo Paul Kagame wa Rwanda na mwenzake wa Chad rais Idris Deby.
Viongozi wa kiafrika wamezindua cheti hicho maalum mjini Kigali Rwanda katika kongamano la viongozi wa Afrika.

Wakwanza kupewa cheti hicho watakuwa ni viongozi wenye hadhi ya kupewa vyeti vya kidiplomasia.

Viongozi wa kwanza kupewa cheti hicho ni rais mwenyeji wa kongamano hilo Paul Kagame wa Rwanda na mwenzake wa Chad rais Idris Deby.

160717145512_au_passport_cu_624x415_bbc.jpg

Image captionMadhumuni ya AU umoja wa Afrika kuzindua cheti hicho ni kuvunja mipaka iliyowekwa na mkoloni alipoigawanya Afrika ilikuitawala katika karne iliyopita.
Marais wote waliohudhuria kongamano hilo watapewa cheti hicho cha AU kabla ya kukamilika kwa mkutano huo.

Mawaziri wa maswala ya kigeni na viongozi wakuu katika umoja wa Afrika pia wanatarajiwa kufaidi cheti hicho cha kusafiria.

Umoja wa Afrika unatarajia kuwa mataifa ya kiafrika yataanza kutoa vyeti hivyo vipya vya usafiri kufikia mwaka wa 2018.

Nonsense tatizo la africa si passport, these fictators are funny
 
Waafrika tukikomaa wenyewe tunaweza jitoa, ila i dont see this happening in anyway. Viongozi walio hungry na power Africa ni wengi mno, kila moja ananifikiria mwenyewe tu. Hata hii passport hiyo 2018 ikifika hawajavunja agreement ni bahati sana.
 
Waafrika tukikomaa wenyewe tunaweza jitoa, ila i dont see this happening in anyway. Viongozi walio hungry na power Africa ni wengi mno, kila moja ananifikiria mwenyewe tu. Hata hii passport hiyo 2018 ikifika hawajavunja agreement ni bahati sana.
Usisahau kuna passport ya EAC.
 
="Abdulhalim, post: 16881610, member: 16155"]Hawawezi kuja kama serikali yetu tukufu haijaridhia. It is commonsense.[/QUOTE]
Kwanza Mtanzania jiulize je ruhusa ya kusafiri nje utaipata wapi? Kwa jinsi hali ilivyo hii pasi haina faida kwetu.
 
Back
Top Bottom