Uchaguzi 2020 Hii ndio orodha ya watu watakaompigia kura Magufuli

Habari za leo watanzania wenzangu, Natumai mu wazima wa afya njema.

Leo nitatoa orodha ya watanzania watakao mpigia kura Magufuli siku ya oktoba 28. Naomba ufuatane na mimi ili upate kuelewa vizuri kama hujui. Basi yafuatayo ndio makundi ya watu hao.

1. Watu wenye akili timamu, wanaojua kutafakari na kupambanua mambo. Hawa lazima wampigie kura Magufuli.

2. Watu wanaopenda kuona haki zikitendeka mahakamani, makazini na maeneo mbalimbali. Hawa lazima watampigia kura.

3. Watu wanyonge wanaojua akiwepo Magufuli ataweza kuondoa unyonge wao. Hapa kuna makundi mbalimbali. Hawa lazima watampigia kura.

4. Watu wanaopenda maendeleo na wanapenda kufanya kazi kwa bidii. Hawa lazima watampigia kura.

5. Watu wasiopenda ufisadi na mafisadi. Watu wasiopenda kusikia watu wanaiba pesa zetu huko mabandarini, TRA, na kwenye mataasisi yetu mbalimbali. Hawa lazima watampigia kura.

6. Watu wasiopenda rushwa. Hapa kuna makundi mbalimbali kuna wasiopenda kutoa rushwa na wasiopenda kupokea rushwa. Nina asilimia mia hawa lazima watampigia kura.

7. Wacha Mungu wote hawa lazima watampigia kura zote. Aliwaongoza kwenye maombi kipindi cha korona. Wala hakuruhusu makanisa yafungwe. Alisisitiza waendelee kumwomba Mungu na kufanya kazi. Hawa lazima watampigia kura Magufuli. Watu wote wanaompenda Mungu ndani yao hawa sina shaka nina asilimia mia watampigia kura Magufuli. Hivyo kusanya makanisa yote na misikiti yote hao lazima watampigia kura Magufuli.

8. Watu wasio wavivu na wanaopenda kufanya kazi kwa bidii kwa kiingereza tunasema non lazy people. Hawa lazima watampigia kura hawategemei serikali iwalishe wao wanajua kujituma kwaajili ya kufanya uzalishaji ndani ya taifa ni wajibu wa raia na sio kulala tu ukitegemea serikali ukuletee chakula.

9. Watu wanaopenda maadili mazuri kazini. Hawa lazima watampigia kura Magufuli.

10. Wanaopenda Tanzania iwe kama ulaya. Ukienda ulaya utaona jinsi mawasiliano yalivyo raisishwa. Kuna mabarabara ya juu, matren ya umeme na umeme wa uhakika. Hawa lazima watampigia kura Magufuli. Watu wanaopenda kuona wagonjwa wote hata viongozi wanatibiwa hapahapa Tanzania kwenye hospitali zetu.

11. Watu wanaopenda serikali inayowajibika kwaajili ya wananchi wake. Hawa lazima watampigia kura Magufuli.

12. Watu wanaopenda kuona haki ikitendeka kila maeneo. Hapa kuna wakinanamama, akina baba, vijana, n. k. Na sote tuliona jinsi alivyo kuwa akiwatetea watu mbalimbali katika mikoa mbalimbali kila mikoa ya Tanzania. Wajane walipata faraja, waliozulumiwa walirudishiwa faraja iliyopotea kwa muda mrefu, walionyanyaswa walipata tiba, walio teseka kwaajili ya watu fulani wote hao walipata faraja. Makundi ya watu hawa wote sote tunayajua na nina uhakika asilimia mia watu hawa watampigia kura Magufuli.

13. Watu wanaopenda kuona serikali inayo ajiri kwa kufuata uwezo wa mtu na elimu aliyo nayo. Na sio kuajiri hovyohovyo hata kama mtu hana elimu na uwezo wa kufanya kazi hiyo au kuajiri kwa kufuata undugu. Kundi la watu hawa lazima limpigie kura Magufuli maana ndio mkombozi wao. Katika awamu ya Magufuli hata mtoto wa mkulima ameajiriwa TANESCO, TRA, EWURA, TBS, TBA n. k. Watoto wa wakulima wote ambao hawana connection Magufuli ndio mkombozi wao katika kupata ajira lazima wampigie kura Magufuli.

14. Watu wanaopenda rasilimali zetu zisiibiwe na mabeberu. Tanzania ni nchi yenye rasilimali za kutosha madini kila mkoa na wilaya. Tukiwa na Rais asiye na msimamo kwa mabeberu. Mabeberu wataiba madini na gesi yetu yote. Hivyo kinda lisilopenda haya kutokea nina asilimia Mia lazima limpigie kura Magufuli.

15. Watu wasiopenda kuonewa na mtu yeyote. Na wanajua kwamba wakimfuata Magufuli atawasaidia kukamata wale wanao waonea. Kundi hili nina asilimia mia lazima limpigie kura Magufuli.

Nimemaliza wakuu.
Na Ellyskywilly

Mimi ni mwananchi wa kawaida kabisa mtanzania kijana nisiyependa uvivu wala mchezomchezo katika kazi. Nipo kwaajili ya maendeleo ya taifa langu, sipo hapa kwaajili ya kuomba cheo.

Nipo kwaajili ya kuongea ukweli, ukweli tu ndio utakao waweka huru watanzania.
Mbona umesahau
1 Akina Bashite
2 Pornstars
3 wanaharamu wenye funguo za hazina wanaodaiwa watoto wa dadake DOTTO
4 wauaji wanaojulikana kama "watu wasiojulikana
5 wapenda fiests
6 mayanga construction na wafanya Kazi weke
7 baraza la wanafiki wa kiislamu BAKWATA
8 Wahutu kutoka burundi
9 kiwanja cha chato
10 hekta 25000 kule karagwe
11waliokula pesa za wahanga wa majanga
12 Mdogo wake first Lady wa kigamboni ambae anamtoto yet another mwana haram
13 vimada mbali mbali baadhi wapo serikalini

Muda hautoshi kweli CCM tuna wapiga kura wengi
Yaani Hao wanaharamu na vijumba vidogo vingi Sana
 
Umewasahau waliodhulumiwa korosho zao, waliobomolewa nyumba, wafanyabiashara wanaonyanyaswa na TRA, wafanyakazi wanaokatwa 15% bodi ya mikopo, wale wanaolia na fao la kujitoa, ambao hawajaongezewa mishahara wala kupandishwa vyeo, walioliwa rambirambi zao pamoja na pesa za tetemeko, bila kusahau waliochomewa nyavu zao, waliotumbuliwa bila sababu, waliofukuzwa kazi kwa tuhuma za uongo, kundi la wale wa vyeti feki na familia zao, wananchi wa hali ya chini wanaokabiliana na maisha magumu na wanaotukanwa na Rais wao kila kukicha, wanaobaguliwa kwa fhana ya ukanda na kwa sababu hawakumpigia mwenyekiti kura, kwa kweli watapiga kura kwa wingi sana

Tukutane 28
Tumechoka kutawaliwa kidikteta na Familia moja
We can't breathe
 
Back
Top Bottom