Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,057
Siku zote, historia yako, ndiyo hutoa imani kwa watu wengine.
Hivi ni tangu lini anayejulikana ni mwizi na fisadi, mtu akasema amemwona anaiba, taarifa ikatolewa kwa jamii inayomzunguka, mwizi huyo akasema siyo yeye aliyeiba, halafu jamii ikaiamini kauli yake ya kukanusha bila vielelezo? Kiuhalisia, ni rahisi kuaminika raia aliyetoa taarifa ya wizi uliofanywa na mwizi mzoefu, hata bila ya vielelezo kuliko mwizi mzoefu kujitetea bila ya vielelezo.
Amesikika msemaji wa Bunge akieleza kuwa kauli ya Mbowe kuwa wabunge wale batili, wevi wa kura, Rais Samia amewaongezea mshahara toka shilingi milioni 13 hadi milioni 18, siyo ya kweli. Lakini hakuweza hata kusema ukweli ni upi. Wala hakutoa kielelezo chochote kuuonesha uwongo wa Mbowe.
Lakini tunajua kuwa Bunge, CCM na Serikali, wote wana historia mbaya ya uwongo, ufisadi na wizi. Na vithibitisho ni vingi.
Hawa watu waliojazana bungeni ni wezi wa kura na wezi waporaji wa mamlaka ya wananchi katika kuwapata viongozi.
Baadhi yao wamejazana Bungeni bila kupata kura ya mtu yeyote bali kwa kutangazwa tu na vibaraka wao wa wizi wa kura kuwa ndio washindi.
Viongozi wa chama hiki ndio wanaoongoza serikali ya watu waongo walioweza kufikia hatua mpaka ya kutamka Hayati Magufuli alikuwa anachapa kazi ikulu, wameongea naye kwa simu na anawasalimia sana wananchi, wakati Hayati alikuwa dakika za mwisho za kuyaaga maisha ya Duniani.
Walioiba kura, walioiba maamuzi ya wananchi, hawawezi kushindwa kuiba pesa za umma kwa kupitia njia mbalimbali, ikiwemo hiyo ya kujirundikia mshahara wa sh 18m na posho ya sh milioni 8, total 26m.
Lakini ukiona watu wachache wanafanya uchafu kama huu, ujue umma ndio uliobweteka.
Siku wananchi watakapoweza kunena kwa kauli na dhamira kuwa sisi wananchi ndio wenye maamuzi ya mwisho, ndipo hawa waovu watakapokoma kuyatenda mambo ya ajabu ya kuzinufanisha nafsi zao kwa gharama ya umma wa Watanzania.