Morogoro Enzi Hizo: Hii ndio Morogoro bwana!

Moro mmeipamba vya kutosha,Ni kweli ni mkoa mzuri sana na binafsi nimebahatika kuishi hapo kama miaka miwili hivi ila kuna mambo mawili naomba niwakosoe kidogo wenyeji wa mkoa huu.
1. Mkoa wa moro umejaa "majungu na umbea sana" hasa vijana? yan ukibahatika kukaa vijiwe vya watoto wa moro utashangaa maneno yanayoshushwa hapo.kazi yao kubwa ni "kusifia matajiri matajiri tu" hasa matajiri wa kiarabu....Utakuta mtu wa kijiwe A anamchambua tajiri fulani "kiundani" na kiuhakika yan mpaka wewe msikilizaji unajiuliza hivi huyu mzungumzaji ana undugu na huyo tajiri?hizi habari anazipata wapi? lakini pia habari zile ulizoziskia kijiwe A unaweza kukutana nazo kijiwe B na ukaziskia vilevile kama alivyohadithia wa kijiwe A.
2.Watu wa moro akitaja jina la mtu fulani analazimisha wewe mskilizaji umjue,au anamtaja huyo mtu kana kwamba wewe mskilizaji unamfahamu aliyetajwa? mfano unamuuliza mtu aisee hizi simu zinauzwa wapi? utaskia "nenda kwa dula zipo kibao tu".....yan kamaliza hapo,hakwambii "dula" gani na duka lake lipo mtaa gani.
3.Pia moro kumejaa matapeli sana yaani hii mpaka wazee....tatizo ni lilelile kupenda kitonga na uvivu.
4.Ndo mkoa pekee ambao ugonjwa wa typhod ndo nyumbani. yan hili lipo wazi kila mtu anajua na sababu hata hazijulikani kwanini ugonjwa huu ni rahisi sana kuupata ukiwa moro kuliko mkoa wowote ule tz.
5.Vijana wengi moro shule hawana....hili nalo ni shida.ukikuta kijana amesoma ujue mgeni huyo na si mkazi.
6.Moro Ni watu flani hv wanapenda sana kulalamika kuliko kutafuta solution.
7. Wakazi wa moro wanapenda sana kuongea lafudhi/sauti moja ya yenye mahadhi ya kiluguru.....cha ajabu "sauti" hii hata wasio waluguru nao wanafanya hivyo.hapa wengi mtanielewa....yan hii si watoto si wakubwa.
8.Abood ndiyo kampuni pekee ya mabasi inayokubalika na watu wa moro kuliko kampuni yeyote ya mabasi,japo hali hii inaanza kupungua kwa siku hizi za karibuni.Pia ukitaka uifahamu vizuri familia ya abood haina haja ya kwenda wikipedia,wewe mkamate mtu yeyote wa morogoro akuhadithie Abood ni nani?Utashushiwa nondo hapo mpk utatamani uzibe masikio.....ukweli,uongo,majungu vinamixiwa humohumo ili uchambue mwenyewe....


Yapo mengi ila kiufupi haya ndo yaliyonikera nilipokuwa moro.ila yote kwa yote Moro ni mkoa mzuri sana kuishi hasa unapokuwa na vyanzo vya pesa vya uhakika...ni pazuri sana kiukweli.
Katika muda niliokaa Moro hayo uliyosema ni kweli tupu nineobserve mwenyewe.Halafu kinachoniudhi Kwa Moro vijana wa Moro ni Wapiga mzinga balaa.Unaenda Bar mtu yupo bar lkn unashangaa unaanza kukupiga mzinga,huwa najiuliza kaja bar kufanya nini ilihali hela hana
 
Ha ha ha noma sana,kuna jamaa walikuwa wanajitega kabisa njia nnayopitia kurudi home mida ya kurudi tu utakuta wapo njiani Broo nipe ya fegi au msosi kumbe mwingine anaunga unga hela ya Bangi au hela ya kwendea Kahumba
 
Ha ha ha noma sana,kuna jamaa walikuwa wanajitega kabisa njia nnayopitia kurudi home mida ya kurudi tu utakuta wapo njiani Broo nipe ya fegi au msosi kumbe mwingine anaunga unga hela ya Bangi au hela ya kwendea Kahumba
Hv kahumba bado ipo active ?
 
ROmbo resort bado ipo?! Umenikumbusha maeneo ya Madizini, kwa mnyonge, kilakala, Kigurunyembe, Nyumba za Polyster. Hivi yule dereva wa mabasi maarafu kwa jina la makata bado yupo?!
 
Unaweza kwenda kingstone kama unaenda 8 8
Moro kubwa mno.. Al saed, Islam ndo mabus ya zaman, ukija pale KILOSA, mtaa wa uhindini.. disko la babilon... Dumila hapo ndo usiseme, enzi hzo mahindi ya kuchoma duu, Ukija pale mkongeni Dakawa, nilikuwa nakwenda kila jmos kula nyama baada ya msuli wa Dumila Sec...
 
Kuna sehemu ilikuwa inaitwa Masika, una kaa hapo kusikiliza muziki huku unakunywa soda
 
Naizungumzia zaidi Moro ya kipindi cha nyuma kidogo ya miaka ya 90 hadi 2000 mwanzoni... Hii town ya wajanja , vijana wanaojua kuvaa,wenye exposure, wapenda burudani na utafutaji... Ni mji uliofikia kuitwa jiji kasoro bahari kutokana na upatikanaji wa kila kitu kinachotakiwa... Kulikuwa na shule kubwa mbili Forest Hill na Kigurunyembe ambapo Forest ilikuwa ya watoto wa kishua na Kigurunyembe ilikuwa ya watoto wa kihuni... Mitaa maarufu ilikuwa ya kishua ni Forest, Liti, Sua na Rock garden... Mitaa maarufu ya ushenzini kulikuwa na Mji mpya, Kichangani, Mafiga.

Watu wa Moro ni wapenzi sana wa burudani haswa muziki na soka.... Kulikuwa na timu ya mji maarufu Reli kiboko ya vigogo hii ilikuwa daraja la kwanza alikuwa akija Simba au Yanga atoki.. Hiyo Reli naizugumzia ya kina Duncan Butinini, David Mihambo, Fikiri Magoso, Mohamed Mtono hapo kuna mshangiliaji maarufu sana wa kuitwa Ya mungu ambae ndio shabiki wa kwanza mtanzania kujichora mwilini... Licha ya Reli mtaani kulikuwa na team nyingi sana za mchangani kama chama langu Jamaica, kulikuwa na Black Viba, Small boys, Zaragoza baadae ikawa Moro United, Uruguay, Burkina Fasso, Rhino nk mtaani ilikuwa ni hatari.

Kwenye muziki Moro ina historia ndefu kidogo siwezi kuzungumzia enzi za kina Mbaraka Mwishehe kwa kuwa sikuwepo mimi nilikuwepo enzi za shimoni Morogoro Hotel na Rock Garden na maonyesho ya Forest Hill... Hapa kuna mtu anaitwa Dj Sweet Coffee alikuwa pale mtaa wa Konga ndio alomfundisha Udijei John Dilinga enzi hizo akiitwa John Mkimbizi sababu baba yake alikuwa mkimbizi kambi ya Solomon Mahlangu.. Disco lilikuwa linapigwa shimoni na mara nyingi alikuwa anakuja Dj Joseph Kusaga akimfundisha kazi Dj Peter Moe.

Watu wa Moro najua mpo wengi umu Jf naomba tukumbashane mawili matatu matukio, maujanja na mazuri ya Moro Town.

Moro Town ulikuwa pia mji wa kibabe.. Kulikuwa na watemi wa mji kina Slim mtoto wa sheikh mkuu, Matata, Gamba mcheza judo, vijana wa siafu toka mji mpya nk

Unaikumbuka Miss Morogoro? Unamkumbuka Alex Nictas?

Unawakumbuka mabingwa wa kudansi kitaifa? Kina Askofu, Bob Tigger, Super Ngedere nk

Unakumbuka mashindano ya magari? Unawakumbuka wakimbiza magari maarufu kina Collen, Steve, Pat, Kararambe, Shanto, De Santos nk

Unakumbuka wagiriki na bata zao kwa Mama Perina na Acropol? Unakumbuka masista duu na mabraza meni wa mitaa ya Forest?

Unakumbuka enzi za Mnet inaingia mjini? Moro mji wote ulikuwa na access ya kuona dstv bure.

Unakumbuka heka heka za ligi za mbuzi uwanja wa shujaa, makaburini kilakara na kikundi?

Unakumbuka Fete Fete? Unakumbuka Shan cinema? Unakumbuka swimming pool ya rock garden?

Unamkumbuka Mzee Mkwidu na Patel wakuu wa shule maarufu KG & Forest?

Unamkumbuka Maneno Big G rip? Unamkumbuka Mnambo wauza ngada maarufu?

Unamkumbuka Ndanje jambazi aliyetikisa mji? Unakumbuka ishu yake ya silaha na February Ma rope?

Unamkumbuka toz wa kipindi hicho Puzzo na kundi lake la kurap Watukutu akiwa na Sallam meneja wa Diamond sasa hivi? Unawakumbuka Gangster Family? Unawakumbuka Ze domp?

Unamkumbuka Achimpota? Unaikumbuka bus la Chambo?

Unakumbuka ule upepo uliokuja wa watu kuzamia Sauz na ulaya?

Umeishi mtaa gani Mafisa, Msufini, Kilakara, Ngoto, Kingo, Mlapakoro, Boma road, Sua, Vibandani, Relwe magorofani, Kigurunyembe, Madizini? Au wapi Umeishi?

Kuna watu maarufu wengi sana DSM ambao maujanja yao wamejifunzia Moro Town... Hakika Morogoro ni jiji kasoro bahari.

WATOTO WA MOROGORO MIKONO JUU.
Siku Ndanje anapigwa risasi alitokea Kahumba na alikuwa amelewa sana na alishindwa kudhibiti akili na mwili wake. Ila kulikuwa na demu aliyekuwa naye kwenye tukio alifanya makeke ya ajabu
 
Mji kasoro bahari,.Nyumbani ni nyumbani na iko siku nitarudi nyumbani..kuna mengi sana moro ambayo yamekuwa istoria,.kulikuwa na midundiko yakutosha tu kama kisamango,kudawimbe ambao ulikuwa unaongozwa na mzungu lakini mwishoni wakasema alikuwa jasusi..camp scout tunajitia Bahati camp,yaani kujiachia na girl guide adi raha.ukija viwanja vya usiku usiongee,tunaanzi shimoni,tunaoitia bwalo la umwema,tunamalizia na mango park uwanja wa nyumbani..chama langu la mpira pia jamaica(jamaica maridadi mwendo wake sua sua.yaani machizi kibao ndani ya jamaica,maskani ya timu Princeses hotel opp na ilipokuwa stendi ya kitambo,kwa kina mwamadi rasam kaka yake na fauz..kipindi icho jamaica haishikiki ndani ya moro,kuna shanto golini,wako mapacha wa msikit mkuu pale,yuko mwana mudi kibakuli,sentaafu kuna mwana kutoka 7 saba wa kuitwa kalonga,hassani bantu alikuwa kama kiongozi,yaaani machizi kibao..ukija fujo za mjini usiongee mkuu wa polisi moro yaani ASP alikuwa mzee mmoja wa kuitwa Sadam,alikuwa mtata kinoma.jumamosi tunaenda kuongesha mbwa mati,tukimaliza njiani pale shule ya mbuyuni tunapiganisha mbwa,ilikuwa noma si mchezo.maswala picknic tunajitia zetu rock garden,au morning site,tukiona uzushi tujitia tangeni..kipindi icho mkundi mashamba,lukobe kote mashaba..soccar uwanja shujaa,uwanja saba saba kitaa. Kigurunyembe ulikuwa utuambii kitu uwanja wa nyumbani,hosteli kwa brother john,Brass bend ya father kanuti,muuza miogo wa kuitwa economi,na chizi we kitaa kile losi buka..Yaani naimiss moro kinoma,tukitoka shule nakatiza kwa makaburi ya sultani kingo kisebengo.. unaikumbuka taxi maaruf moro?taxi no 20 ya refarii nyamwela?unamjuwa chizi maarufu kibedui?anakumbuka ajali za coaster kipindi lakshari tumepoteza washkaji kibao.unakumbuka majina ya zile coaster kama el sakrani,kuchaluga,mwadila,ez come az go,second george likopero na nyingine nyingi..ikifika ijumaa washkaji kibao wanatoka dar wanakuja moro kuruka nyoka..Sema ndiyo hivyo hakuna lililo na mwanzo likakosa mwisho.
 
hahaaa
piga kiwi lakini ukitoka utafurahi ..hahaaa
sasa wakaumbuka Kile kipindi cha picnic ..vipi kuhusu Yale mabomu ya mungu mmoja teehhh enzi hizo mkuu wa police SADAMU ..ikifika msimu wa baridi kuamka kwenda shule watafakuri..baridi lamaana ukiongea mdomo watoa moshi..
huku milima ya nawiri na kuzidi kuvutia kwaajili ya uoto wa asili maji yanatiririka milimani tena waiona vizuri kabisa water falls hats ukiwa nyumbani kwenu. .
Siku hizi waterfalls hatuzioni tena mkuu..waluguru wamesafisha mlima kwa kukata miti na mashindano ya kuchoma moto mlima...ile scenic beauty haipo tena
 
Moro mmeipamba vya kutosha,Ni kweli ni mkoa mzuri sana na binafsi nimebahatika kuishi hapo kama miaka miwili hivi ila kuna mambo mawili naomba niwakosoe kidogo wenyeji wa mkoa huu.
1. Mkoa wa moro umejaa "majungu na umbea sana" hasa vijana? yan ukibahatika kukaa vijiwe vya watoto wa moro utashangaa maneno yanayoshushwa hapo.kazi yao kubwa ni "kusifia matajiri matajiri tu" hasa matajiri wa kiarabu....Utakuta mtu wa kijiwe A anamchambua tajiri fulani "kiundani" na kiuhakika yan mpaka wewe msikilizaji unajiuliza hivi huyu mzungumzaji ana undugu na huyo tajiri?hizi habari anazipata wapi? lakini pia habari zile ulizoziskia kijiwe A unaweza kukutana nazo kijiwe B na ukaziskia vilevile kama alivyohadithia wa kijiwe A.
2.Watu wa moro akitaja jina la mtu fulani analazimisha wewe mskilizaji umjue,au anamtaja huyo mtu kana kwamba wewe mskilizaji unamfahamu aliyetajwa? mfano unamuuliza mtu aisee hizi simu zinauzwa wapi? utaskia "nenda kwa dula zipo kibao tu".....yan kamaliza hapo,hakwambii "dula" gani na duka lake lipo mtaa gani.
3.Pia moro kumejaa matapeli sana yaani hii mpaka wazee....tatizo ni lilelile kupenda kitonga na uvivu.
4.Ndo mkoa pekee ambao ugonjwa wa typhod ndo nyumbani. yan hili lipo wazi kila mtu anajua na sababu hata hazijulikani kwanini ugonjwa huu ni rahisi sana kuupata ukiwa moro kuliko mkoa wowote ule tz.
5.Vijana wengi moro shule hawana....hili nalo ni shida.ukikuta kijana amesoma ujue mgeni huyo na si mkazi.
6."Mizinga"....daah yan hili ndo gonjwa la pili linalofuata baada ya typhod.Vijana wa moro mnapenda sana kuomba omba vihela vidogo vidogo...afu hawataki kuamini utakapomwambia "sina" yan atakuona mbaya sana....mnapenda sana mteremko vijana wa moro hebu badilikeni.
7.Moro Ni watu flani hv wanapenda sana kulalamika kuliko kutafuta solution.
8. Wakazi wa moro wanapenda sana kuongea lafudhi/sauti moja ya yenye mahadhi ya kiluguru.....cha ajabu "sauti" hii hata wasio waluguru nao wanafanya hivyo.hapa wengi mtanielewa....yan hii si watoto si wakubwa.
9.Abood ndiyo kampuni pekee ya mabasi inayokubalika na watu wa moro kuliko kampuni yeyote ya mabasi,japo hali hii inaanza kupungua kwa siku hizi za karibuni.Pia ukitaka uifahamu vizuri familia ya abood haina haja ya kwenda wikipedia,wewe mkamate mtu yeyote wa morogoro akuhadithie Abood ni nani?Utashushiwa nondo hapo mpk utatamani uzibe masikio.....ukweli,uongo,majungu vinamixiwa humohumo ili uchambue mwenyewe....


Yapo mengi ila kiufupi haya ndo yaliyonikera nilipokuwa moro.ila yote kwa yote Moro ni mkoa mzuri sana kuishi hasa unapokuwa na vyanzo vya pesa vya uhakika...ni pazuri sana kiukweli.
Kila eneo lina ustarabu wake, Ukiwa Njombe/Iringa watu wa kule hawapendi makabira mengine, hawakupi ushirikiano huwo ndio ustarabu wao, Ukizungimzia typhoid ni kweli ipo ndio maana Wafaransa waliboresha ziwa Mindu kwasababu ya huo ugonjwa na kichocho, Je Njombe/Iringa/Mbeya si ndio ukimwi umetamaraki?. Mji unapokua lazima kuwe na Wavivu, pia Moro sio wote Waluguru isolation, wengi pale walikuja, waha, wasagara, wanyamwezi, wagogo, wasukuma n.k, ila ukiwauliza watakwambia wao ni waluguru, kasoro zipo kwa kila Kabira. Unaposema Shule, Waluguru wengi wa Moro mjini wanasoma Dar, familia zipo uko, Moro wamejaa wageni ndio maana pamechangamka. Pole kwa kunyimwa penzi na toto ya Kiluguru, punguza povu.
 
Back
Top Bottom