Hii ndio Iringa halisi na watu wake

Hii ndio Iringa halisi na watu wake

mkuu naona unamwita ngosha aje kuvuruga....😀😀😀😀
Hehehehehe nyuzi kama hizi havurugi.. Yeye chuki yake ni kwa wakaskazini pekee..

Hapa nimemwita makusudi nione kama atasema lolote..
 
Mkuu nina takriban miaka 5 sijafika iringa..
Vipi yale matangazo ya kukata mkono wa sweta… yapo bado??
 
Love Iringa! Ni makazi yangu sasa,nmezaliwa Iringa,University nimesoma Iringa,kazi Iringa,though miye Msukuma,but mji ni mzuri sana,hasa hali ya hewa iko saafi,fursa za kimaendeleo zipo nyingi pia. Lov t
 
Mkuu ile redio nyenza na ebony fm (hot fm) ilisizi nini.. Siioni hapo kwenye list
 
Love Iringa! Ni makazi yangu sasa,nmezaliwa Iringa,University nimesoma Iringa,kazi Iringa,though miye Msukuma,but mji ni mzuri sana,hasa hali ya hewa iko saafi,fursa za kimaendeleo zipo nyingi pia. Lov t
Mimi pia ni makazi yangu sasa nina miaka 2...aaaah,I just love this town. Wakati nahamia huku kutoka dar nilipatwa na mawazo sana,sikujua kama ntaweza kuuzoea hii mji. Iringa kuzuri...karibuni sana ambao hamjawahi kufika ..
 
Kwa kweli iringa sitapasahau. My favourite town.mara ya kwanza ilikua 79 nilipita na mdingi pale ni kakatwa kuingia kwenye bus la railway.sijui dingi hakulipa tkt sielewi. Nikapitishwa dirishani,82 nilifika kwa mjomba pale mkwawa chuoni nikiwa mdogo kabisa.then nikapita tena 88 nikielekea Singida,92 nikapita tena nikienda Mbeya. Hapo bado mdogo ndo teenager age. nikapita ya mwisho 93-94.halafu basi king kross la Boda mtera halikutokea , sijui lilikwama wapi.tumekaa siku 2 pale stand.ndio shala wambe akatukodisha bus tufike mtera. Siku 2 hizo ilikua ni kubwia ulanzi kwa kwenda mberee.nilikua na 1700 enzi hizo iliisha.hadi nauli nililipa ya kuunga unga.
 
Habari za jioni mabibi kwa mabwana,
Bila kupoteza wakati, hebu Leo tutembelee mkoa wa iringa.

Kwa ufupi,
Jina iringa linatokana na neno lilinga, (which means fort) au boma kwa kiswahili.
Mkoa wa iringa una wilaya nne, ambazo ni Iringa manispaa, Iringa vijijini, Kilolo na Mufindi,

Katika elimu, mkoa wa iringa una shule nyingi za sekondari (ni nyingi kuzitaja) na vyuo vikuu vitatu,
Ambavyo ni
Chuo kikuu cha Mkwawa
Chuo kikuu cha Iringa
Chuo kikuu cha Ruaha
Pamoja na taasisi nyingine za elimu ya juu zikiwemo chuo cha ustawi wa jamii na chuo cha mafunzo ya Ualimu cha Kleruu.

Shughuli za maendeleo,
Shughuli za maendeleo katika mkoa wa iringa ni kilimo, ufugaji, usindikaji na biashara,.

Kilimo ndio inayochukua nafasi kubwa, hasa katika mazao ya nafaka, mbao, mazao ya biashara kama chai, mazao ya mbogamboga n.k
Bado kuna fursa nyingi hasa katika kilimo cha misitu ya mbao katika wilaya za kilolo na Mufindi, ambazo hali ya hewa inafaa sana kwa makuzi ya misitu ya mbao. (Fursa hii vijana watz changamkieni),

Mpaka sasa mkoa wa iringa una TV station moja (IMTV) na fm Radio Stations 7
Ambazo ni
Trap Gang Radio
Ebony FM
Country FM
Nuru FM
Kibla ten FM
Furaha FM
Overcomers FM

Hivi karibuni iringa imekuwa ni manispaa ya kuvutia sana kuanzia huduma za jamii (umeme, maji, afya na elimu), miundombinu, mazingira na ujenzi wa mji unaokuwa kwa kasi ,
hali hii pia imechochewa na kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya lami inayounganisha Dodoma na iringa,
Ambapo kwa sasa kanda ya ziwa na kaskazini zimeunganishwa na nyanda za huu kusini na kupelekea kufunguka fursa zaidi za kibiashara.
Kwa sasa Iringa ni HUB.

Pamoja na mengine mengi,

Nihitimishe kwa kupongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na pia Hongera sana ndugu zangu wana iringa, ongezeni juhudi,

Asanteni sana.

Iringa town,
View attachment 399626View attachment 399627

View attachment 399628View attachment 399629View attachment 399630

View attachment 399632

View attachment 399634

View attachment 399635

View attachment 399636

View attachment 399637View attachment 399638View attachment 399639View attachment 399640

Iringa Down-town/Central business district/town centre/high street a.k.a Mjini Kati kuna muonekano wa usafi, mpangilio mzuri na hakuna vumbi. Safi sana na pongezi kwa Halmashauri ya Mji wa Iringa, Tanzania.
 
Habari za jioni mabibi kwa mabwana,
Bila kupoteza wakati, hebu Leo tutembelee mkoa wa iringa.

Kwa ufupi,
Jina iringa linatokana na neno lilinga, (which means fort) au boma kwa kiswahili.
Mkoa wa iringa una wilaya nne, ambazo ni Iringa manispaa, Iringa vijijini, Kilolo na Mufindi,

Katika elimu, mkoa wa iringa una shule nyingi za sekondari (ni nyingi kuzitaja) na vyuo vikuu vitatu,
Ambavyo ni
Chuo kikuu cha Mkwawa
Chuo kikuu cha Iringa
Chuo kikuu cha Ruaha
Pamoja na taasisi nyingine za elimu ya juu zikiwemo chuo cha ustawi wa jamii na chuo cha mafunzo ya Ualimu cha Kleruu.

Shughuli za maendeleo,
Shughuli za maendeleo katika mkoa wa iringa ni kilimo, ufugaji, usindikaji na biashara,.

Kilimo ndio inayochukua nafasi kubwa, hasa katika mazao ya nafaka, mbao, mazao ya biashara kama chai, mazao ya mbogamboga n.k
Bado kuna fursa nyingi hasa katika kilimo cha misitu ya mbao katika wilaya za kilolo na Mufindi, ambazo hali ya hewa inafaa sana kwa makuzi ya misitu ya mbao. (Fursa hii vijana watz changamkieni),

Mpaka sasa mkoa wa iringa una TV station moja (IMTV) na fm Radio Stations 7
Ambazo ni
Trap Gang Radio
Ebony FM
Country FM
Nuru FM
Kibla ten FM
Furaha FM
Overcomers FM

Hivi karibuni iringa imekuwa ni manispaa ya kuvutia sana kuanzia huduma za jamii (umeme, maji, afya na elimu), miundombinu, mazingira na ujenzi wa mji unaokuwa kwa kasi ,
hali hii pia imechochewa na kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya lami inayounganisha Dodoma na iringa,
Ambapo kwa sasa kanda ya ziwa na kaskazini zimeunganishwa na nyanda za huu kusini na kupelekea kufunguka fursa zaidi za kibiashara.
Kwa sasa Iringa ni HUB.

Pamoja na mengine mengi,

Nihitimishe kwa kupongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na pia Hongera sana ndugu zangu wana iringa, ongezeni juhudi,

Asanteni sana.

Iringa town,
View attachment 399626View attachment 399627

View attachment 399628View attachment 399629View attachment 399630

View attachment 399632

View attachment 399634

View attachment 399635

View attachment 399636

View attachment 399637View attachment 399638View attachment 399639View attachment 399640
dah umenitia huzuni sana...nateseka dar wakat kukae kuzuri tuu...bora niludi gangilonga kwetu
 
Back
Top Bottom