Hii ndio Iringa halisi na watu wake

Hii ndio Iringa halisi na watu wake

Mtaa wa uhindini, Manispaa ya Iringa.
IRINGA+TOWN+TANZANIA.jpg
 
Picha zaidi, the Beauty of Iringa Town., the beautiful Tanzania
8007960_orig.jpg
2462685_orig.jpg
iringa_12.jpg
Photo+Dec+4%2C+2012+2-23+PM.jpg
5059718992_b2d51056a3_o.jpg
 
Habari za jioni mabibi kwa mabwana,

Bila kupoteza wakati, hebu Leo tutembelee mkoa wa Iringa.

Kwa ufupi,

Jina iringa linatokana na neno lilinga, (which means fort) au boma kwa kiswahili. Mkoa wa Iringa una wilaya nne, ambazo ni Iringa Manispaa, Iringa Vijijini, Kilolo na Mufindi.

Katika elimu, mkoa wa Iringa una shule nyingi za sekondari (ni nyingi kuzitaja) na vyuo vikuu vitatu ambavyo ni;
Chuo kikuu cha Mkwawa
Chuo kikuu cha Iringa
Chuo kikuu cha Ruaha
Pamoja na taasisi nyingine za elimu ya juu zikiwemo chuo cha ustawi wa jamii na chuo cha mafunzo ya Ualimu cha Kleruu.

Shughuli za maendeleo, shughuli za maendeleo katika mkoa wa iringa ni kilimo, ufugaji, usindikaji na biashara.

Kilimo ndio inayochukua nafasi kubwa, hasa katika mazao ya nafaka, mbao, mazao ya biashara kama chai, mazao ya mbogamboga n.k. Bado kuna fursa nyingi hasa katika kilimo cha misitu ya mbao katika wilaya za Kilolo na Mufindi, ambazo hali ya hewa inafaa sana kwa makuzi ya misitu ya mbao. (Fursa hii vijana watanzania changamkieni)

Mpaka sasa mkoa wa Iringa una TV station moja (IMTV) na fm Radio Stations 7
Ambazo ni;
Trap Gang Radio
Ebony FM
Country FM
Nuru FM
Kibla ten FM
Furaha FM
Overcomers FM

Hivi karibuni Iringa imekuwa ni manispaa ya kuvutia sana kuanzia huduma za jamii (umeme, maji, afya na elimu), miundombinu, mazingira na ujenzi wa mji unaokuwa kwa kasi, hali hii pia imechochewa na kukamilika kwa ujenzi wa barabara ya lami inayounganisha Dodoma na iringa, ambapo kwa sasa Kanda ya Ziwa na kaskazini zimeunganishwa na nyanda za huu kusini na kupelekea kufunguka fursa zaidi za kibiashara.
Kwa sasa Iringa ni HUB.

Pamoja na mengine mengi.

Nihitimishe kwa kupongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na pia hongera sana ndugu zangu wana Iringa, ongezeni juhudi.

Asanteni sana.

Iringa town,
View attachment 399626View attachment 399627

View attachment 399628View attachment 399629View attachment 399630

View attachment 399632

View attachment 399634

View attachment 399635

View attachment 399636

View attachment 399637View attachment 399638View attachment 399639View attachment 399640
Daaah iringa mzunguko wa biashara mdogo snaa
 
Naipenda Iringa, ndiyo mji mzuri na niupendao kuliko yote Tanzania, umesahau jiwe la Gangilonga nilishapanda mara nyingi tu hadi juu!

One love kwa masela wote pale Shooters downtown tulikuwa tunacheza billiards (polltables) na kushushia na bia bariiidi!

Long live Iringa, my home of Choice, Nitarudi Iringa Mungu akipenda!


1280px-Iringa.JPG

jiwe la gangilonga hata mie nimepanda, na kupiga mapicha kibao. shida la hilo jiwe ni wakati wa kushuka lazma uone manyotanyota.
 
Mkuu naomba sifau au mapungufu ya wanawake wa kihehe maana naona 98% nahisi nitakuja kuoa mhehe
Wanawake wa iringa kwanza kabisa
+altitudes
1. Wafanyakazi haswaaa
2. Wepesi wa kushaulika
3. Hawana makuu sana.
4. Wavumilivu sana
5. Wana upendo wa dhati
-altitudes
1. Hasira ipo karibu sana
2. Wivu wa mapenzi
3. Wanapenda pombe baada ya kazi
2.
 
Ni kweli, kama kigezo ni biashara sio sahihi kulinganisha mbeya na Iringa.
Lakini naijua mbeya in and out. Kuna mengi mazuri, na mabaya pia yapo ambayo yanahitaji marekebisho..(another topic though)
 
Duuuhhh iringa kuzuri kiasi hicho !!natamani maisha yangu yahamie iringa kwanza kuna watt wazuri mnoo
 
Hujakosea kabisa. Watoto wa iringa tupo vizuri na uchapa kazi ni sehemu ya maisha yetu.
Dah.... Alama pekee ya kumtambulisha mtoto wa Iringa ni Ile urembo pembeni ya macho... Wenyewe wanaita 11....kama huna basi wewe ni sawa mzaramo aliyekimbia joto la Dar na kuja kujificha Iringa
 
Back
Top Bottom