GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,736
- 109,328
Kuna Mjumbe wangu wa Nyumba Kumi Kumi muda si mrefu kaniambia kuwa niende Ofisi za Serikali ya Mitaa ili nikajiandikishe nisubirie Mkopo. Nilipoenda kweli nikapokelewa kwa 'Bashasha' zote na kuambiwa tuwe 'Njemba' Kumi ( 10 ) kisha twende na tutapewa Tsh 500,000/= ( Shilingi Laki Tano ) ambapo kila Mtu atapewa Tsh 50,000/= ( Shilingi Elfu Hamsini ) kama Mtaji wake.
Ni Jambo jema ila kilichonishangaza tukaulizwa kama tuna Kadi za Kupigia Kura hasa kwa Uchaguzi Mkuu huu ujao wa 2020 ambapo karibia Wote tukasema tunazo na Kuulizwa pia kama tuna Kadi ya Chama Kimoja ( nakihifadhi ) tukasema tunazo japo wengine wakasema hawana. Na 'Mkopo' wenyewe tumeambiwa tukipewa tuna Uhuru wa Kurudisha au hata Kutourudisha vile vile.
GENTAMYCINE siyo 'Financial Guru' ila nawaombeni 'Wadau' hapa 'mnielimishe' je, aina hii ya 'Mkopo' unaitwaje na kwanini itolewe Kipindi hiki tu?