Uchaguzi 2020 Hii 'Mikopo' ya aina hii kwanini huwa 'inatolewa' tu Kipindi hiki cha 'Kampeni' halafu haina hata 'Riba' yoyote ile?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,485
108,609
Kuna Mjumbe wangu wa Nyumba Kumi Kumi muda si mrefu kaniambia kuwa niende Ofisi za Serikali ya Mitaa ili nikajiandikishe nisubirie Mkopo. Nilipoenda kweli nikapokelewa kwa 'Bashasha' zote na kuambiwa tuwe 'Njemba' Kumi ( 10 ) kisha twende na tutapewa Tsh 500,000/= ( Shilingi Laki Tano ) ambapo kila Mtu atapewa Tsh 50,000/= ( Shilingi Elfu Hamsini ) kama Mtaji wake.

Ni Jambo jema ila kilichonishangaza tukaulizwa kama tuna Kadi za Kupigia Kura hasa kwa Uchaguzi Mkuu huu ujao wa 2020 ambapo karibia Wote tukasema tunazo na Kuulizwa pia kama tuna Kadi ya Chama Kimoja ( nakihifadhi ) tukasema tunazo japo wengine wakasema hawana. Na 'Mkopo' wenyewe tumeambiwa tukipewa tuna Uhuru wa Kurudisha au hata Kutourudisha vile vile.

GENTAMYCINE siyo 'Financial Guru' ila nawaombeni 'Wadau' hapa 'mnielimishe' je, aina hii ya 'Mkopo' unaitwaje na kwanini itolewe Kipindi hiki tu?
 
Haina tofauti sana na hizi ahadi za Magufuli kwenye kampeni halafu hapo hapo anawaamuru watendaji wa serikali waanze mara moja kuzitekeleza, kisha anawauliza wananchi kama watampa kura.
Ndio CCM hiyo.
 
Mkuu kwani na Wewe siyo 'Financial Guru' labda uweze 'Kunielemisha' na Mimi 'Ngumbaru' wa Masuala ya 'Fedha' na 'Mikopo' hasa Kipindi hiki tu?
Mkuu Rais Magufuli aliahidi kutoka 50,000,000 kwa kila kijiji, wewe ni kati ya wale watu 100 mliobahatika kupewa hiyo hela. Hata usitegemee kudaiwa, Tumetekeleza Matokeo Chanya +
download.png
 
Mrejesho wake ujitowe akili utupe huko Lumumba uanze kusifia kila jambo ata ukila chakula usiku useme kama sio awamu ya tano nisingekula leo kama sio awamu ya 5 nisenge pewa mechi na wife leo!
 
Alafu pale TAKUKURU kuna brigedia generali anafuga tu tumbo na mashavu. Kazi kubambikia mahasimu wa Jiwe kesi na kuwanyang’anya hela zao tu!!
 
Alafu pale TAKUKURU kuna brigedia generali anafuga tu tumbo na mashavu. Kazi kubambikia mahasimu wa Jiwe kesi na kuwanyang’anya hela zao tu!!

Hili siwezi Kulisemea kwani sina uhakika nalo hasa ukizingatia 'Mhusika' Mkuu huyo kutoka 'JWTZ' namjua alivyo Makini, Imara na Mweledi mno tu.
 
Chukua, tumia. Kupiga kura ni siri yako. Hata kadi utapewa hela ukakate kama huna.
 
Back
Top Bottom