Hii mboga inaliwa? Msaada wenu!

BlackPanther

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
9,020
8,480
Mchicha pori mwekundu je! Unaliwa ama sumu?

Na upandaji wake ni kama mchicha tuliouzoea?

Hivyo nikisema nijaribu kuupanda unakubali kwa all season kwa maana kiangazi na masika?

Mchicha pori nimetokea kuupenda sana sana, ila huu mwekundu unanipa mashaka kama unaliwa.
IMG_1525-e1599567686711.jpg
full_449_2__amarant-vishnevyy-dzhem.jpg

Msaada wenu wanajamvi.

Herbalist Dr MziziMkavu n.k
 
Mchicha pori mwekundu je! Unaliwa ama sumu?

Na upandaji wake ni kama mchicha tuliouzoea?

Hivyo nikisema nijaribu kuupanda unakubali kwa all season kwa maana kiangazi na masika?

Mchicha pori nimetokea kuupenda sana sana, ila huu mwekundu unanipa mashaka kama unaliwa.
View attachment 2934369View attachment 2934370

Msaada wenu wanajamvi.

Herbalist Dr MziziMkavu n.k
Ukisikia mchicha pori orijino ndiyo huu sasa. Majani yake yana faida lukuki ikiwemo kuongeza nguvu za kiume, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa sumu mwilini, kupunguza cholesterol, kuimarisha uoni wa macho na faida nyingi nyingine.

Hizo mbegu huwa zinavunwa na kusagwa na huuzwa ghali sana. Huwa zinachanganywa na ulezi pamoja na unga kidogo wa mbegu za maboga kupikia uji ambao unasemekana unafanya kazi vizuri zaidi kuliko viagra!
 
Kula majani hayo ni mboga safi sana na salama. Kuuogopa ni sawa na kuogopa mtama mwekundu kwa rangi yake hali mababu zetu huko Kishapu, Bariai, Maswa, Igunga n.k wamekula na walikuwa imara zaidi ya wala mahindi ya panna, zam seed n.k
 
Ukisikia mgagani orijino ndiyo huu sasa. Majani yake yana faida lukuki ikiwemo kuongeza nguvu za kiume, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa sumu mwilini, kupunguza cholesterol, kuimarisha uoni wa macho na faida nyingi nyingine.

Hizo mbegu huwa zinavunwa na kusagwa na huuzwa ghali sana. Huwa zinachanganywa na ulezi pamoja na unga kidogo wa mbegu za mabogq kupikia uji ambao unasemekana unafanya kazi vizuri zaidi kuliko viagra!
Mpwa utafanya watu waufyeke Kwa matumiz 😂😂😂
 
Mchicha pori mwekundu je! Unaliwa ama sumu?

Na upandaji wake ni kama mchicha tuliouzoea?

Hivyo nikisema nijaribu kuupanda unakubali kwa all season kwa maana kiangazi na masika?

Mchicha pori nimetokea kuupenda sana sana, ila huu mwekundu unanipa mashaka kama unaliwa.
View attachment 2934369View attachment 2934370

Msaada wenu wanajamvi.

Herbalist Dr MziziMkavu n.k
ni miongoni mwa mboga mujarabu sana huku kwetu,
yote nyekundu na isiyo nyekundu tunaitumia barabara🐒
asubuhi ni mboga ya faster fasta sana, chapchap na kiporo cha kuchoma au kupasha, na mchana na ugali mujarabu wa dona na maziwa mtindi 🐒

wewe acha kabisaa mimi na wanainchi wangu ni bam bam kwenye misosi....
 
Ukisikia mgagani orijino ndiyo huu sasa. Majani yake yana faida lukuki ikiwemo kuongeza nguvu za kiume, kuimarisha kinga ya mwili, kuondoa sumu mwilini, kupunguza cholesterol, kuimarisha uoni wa macho na faida nyingi nyingine.

Hizo mbegu huwa zinavunwa na kusagwa na huuzwa ghali sana. Huwa zinachanganywa na ulezi pamoja na unga kidogo wa mbegu za mabogq kupikia uji ambao unasemekana unafanya kazi vizuri zaidi kuliko viagra!

Mhala sana shimba? Huo sio mgagani, bali ni mchicha pori mwekundu kama ulivyo mchicha pori wa kijani. Mgagani naujua vizuri majani yake machungu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom