Hii Karata waliyocheza CHADEMA inaweza ikawa imetoa mrejesho ulio hasi kwao kwa upande mwingine

Chadema ni chama cha umma ccm ni ni kikundi kinachotawala bila utashi wa watanzania kuna tofauti kubwa hata kama ukisema uwachangie je nani atakubali kuwachangia? police?
Mimi binafsi bora kuchangia mbwa kuliko CCM na Polisi wao
 
Masikini ya Mungu, huyo msaliti wala hata hajui kuwa Chadema haikumtenga kwenye michango as long as matangazo yote chama kilikua kinataja faini million 350 yote including million 30 ya huyo mbwiga anayeleta kejeli baada ya kununuliwa kutoka gerezani.
 
I thought it could have been done within hours, now it is days buda! My questions are kweli chama hakina watu elfu hamsini wa kuchanga ten ten since yesterday, au tuseme wanachama laki mbili wa kuchanga buku mbili mbili jero kweli!?
WACHA TULICHELEWESHE ILI TUENDELEE KUTUMIA MUDA KIKAMPENI NA KUUTANGAZA UOVU WA WATAWALA NA MAHAKAMA ZAO
 
Vipi mbona mmeshindwa kujenga hata ofisi kama kweli ni chama cha wananchi? Mnakaa kweli pagale pale ufipa.!!
Ofisi mlizonazo zinatosha ofisi ziko kwenye miyoyo ya watu milion230+++ ndani ya saa 24 halafu unasema hawana ofisi ama kweli akili ni nyweli kila mtu ana zake na wewe pia una zako
 
Nimeona na kuisikia clip moja ikimuonyesha aliyekuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ambaye sasa ni mwanachama wa CCM Dr. Vincent Mashinji akiwa na Polepole, Mama Kate Kamba, mke wake na viongozi wengine wa CCM mkoa wa Dar es Salaam. Ni baada ya kulipiwa faini yake na kutolewa gerezani.

Katika neno lake la shukrani, Dr. Mashinji, pamoja na mambo mengine, alirusha kijembe kwa chama chake cha zamani CHADEMA. Alisema kuwa mchango wa shilingi milioni thelathini ndani ya CHADEMA ungekuwa ni jambo la kitaifa lakini ndani ya CCM jambo hilo limeratibiwa na mkoa mmoja wa Dar es Salaam tu.

Katika kuongezea nguvu kauli yake hiyo, Dr. Mashinji alisema CCM ni ndugu na chama dume. Kwanza ni kweli kuwa michango inayoendelea CHADEMA ni ya kitaifa. Pili, Dr. Mashinji anapaswa kufahamu kuwa CHADEMA inapaswa kukusanya pesa nyingi zaidi ya milioni thelathini zilizomhusu. Lazima michango iwe ya kitaifa. Tatu, michango ya CHADEMA inatoa ujumbe mzito.

Mosi, michango ya CHADEMA inasadifu uwepo wa chama na wanachama na marafiki wa kichama kila mahali hapa Tanzania. Tena, michango ya CHADEMA inadhihirisha mshikamano, umoja ,upendo kwa viongozi wao na kujitoa kwa wanachama kwa ajili ya chama na viongozi wao. Huu ni ujumbe mzito na muhimu kisiasa.

Kimsingi, kijembe cha Dr. Mashinji kilisahau ujumbe unaobebwa na michango ya CHADEMA inayoratibiwa kitaifa kupata faini ya kuwatoa viongozi wao gerezani. Siasa ni kutangazika!
Mashinji = bidhaa
 
Lipumbavu
 
Sisi Emu
Chadema ni chama cha umma ccm ni ni kikundi kinachotawala bila utashi wa watanzania kuna tofauti kubwa hata kama ukisema uwachangie je nani atakubali kuwachangia? police?
IMG-20200312-WA0041.jpeg
IMG-20200312-WA0052.jpeg

Jr
 
Viongozi wakuu wa CHADEMA, Jana walikutana na Nyundo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, pale walipopatikana na hatia ya jumla ya makosa kumi na mbili(12)na kutakiwa kulipa faini ya jumla ya fedha kiasi Cha Tsh.350 milioni au kwenda jera miezi mitano(5) kwa kila mmoja.

Kama kawaida ya wanasiasa wakaamua kuitumia Hukumu hiyo Kama karata ya kisiasa, wote tunajua Mbowe hawezi kukosa milioni 70, Msigwa hawezi kukosa milioni 30, lakini wakaona ngoja wapime upepo ni kwa kiasi gani bado wana ushawishi katika jamii.

Kwa macho ya kwaida unaweza kusema wamefanikiwa, lakini ukizama ndani zaidi unaweza kuanza kutilia mashaka ushawishi wa chama hiki kikuu Cha upinzani.
CHADEMA walihitaji watu elfu hamsini tu(50000) wawachangie Tsh.10000 wawe wote wametoka ndani Leo hii.

Lakini hadi muda huu, Ni watatu tu Kati ya 7 walikuwa wamelipiwa( hapa Dr.Mashinji si sehemu). Sasa hoja inaweza kiibuka inawezekana vipi katika Taifa lenye watu karibia milioni 60, tuseme watu wazima ni nusu yake, Chama kinachojinasibu kuwa kinakubalika Sana na kulikuwa na habari kuwa kampeni ya CHADEMA ni msingi imetengeneza mamilioni ya Wanachama halafu hadi sasa Chama hiki kimekosa watu elfu hamsini wa kutoa ten ten.

Hii karata inaweza ikawa imewapa umaarufu wa muda CHADEMA lakini inaweza pia ikawa imewaacha uchi hasa kwenye nguvu yao ushawishi kwa Watanzania kwa Sasa.
Ungejua malengo mapana ya Chadema ungemshauri mwenyekiti wenu atoe maagizo watoke bure. Hii issue ina kwenda kuiweka Tanzania uchi. Its a matter of time mtajilaumu.. Hivi una fikiri Chadema wamekosa hizo pesa? Viongozi wenyewe wange changishana wana uwezo wa kuwatoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilikuwa huko mbali,makalioni mwa nchi,nikasikia hizi habari kwenye kiduka kimoja watu wanapiga story,,
Hi habari imesambaa kila Kona asee..
 
CHADEMA haikosi hicho kiasi cha Tsh 350M, lakini lazima ujifunze jambo kubwa katika umma na katika mshikamano wa kitaasisi.

Mfano: Kwanini majanga ya kitaifa ama maafa ambayo hutokea hua serikali ufungua account za wananchi kuchangia na unakuta kiasi kinachohitajiwa si kukubwa?? Je! Serikali haiwezi kua na pesa hizo?

Kwenye uongozi kuna mbinu za kuwaleta watu pamoja, moja ya mbinu na njia hizo ni kuwafanya wanachama ama wafuasi ama wananchi kujihisi sehemu ya utatuzi wa jambo na suluhu ya tatizo, hii inawapa moyo wa umoja na ushirikiano kizalendo katika jambo (spirit of solidarity), hii haina uhusiano wowote na wingi wa pesa wa taasisi ama shirika ama serikali, ni umoja wa kimkakati katika kujenga uimara wa kusaidiana na kuimarishana.

U.S.A ni taifa lenye uwezo mkubwa sana kifedha lakini wanafanyaga fund rise kwa mambo yao yakitokea kama maafa, ile hali serikali inauwezo wa kufanya.

CDM haijashindwa kulipia cash viongozi wao, lakini hili la kuchangia ni hamasa(kwa waonao mbali kisiasa) ni kuwavuta wengi katika muamko wa kuona umuhimu wa kupambania juhudi zinazoaminiwa kufanywa na viongozi hao waliohukumiwa.

Hii inatupa somo kubwa katika taifa kwamba kuna zaidi ya siasa ndani ya siasa, kuna maisha halisi ya watu, utu na umoja mkubwa sana katika ideology hizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Petro E. Mselewa,
Ukisha ingia kule ufahamu unapotea kabisa.Hivyo usihangaike kuwawazia watu wa aina ya huyo kirusi aliyegundulika ndani ya CHADEMA na kupata tiba yake.
 
kajekudya,
Si kwamba wameshidwa kulipa hiyo faini, kati ya 350m, tayari mashinji alipunguza 30m. Kwa hiyo walipaswa kulipa 320m. Mii ninaamini hawajashindwa, ila wanatumia huo mwanya kubaki ndani ili kujiimarisha kisiasa.
 
Still tathimin yako itakuwa haina true details. Maana hujui nani na nani kachangia. About umma hizo ni politics.. lakin pika kwenye umma huo huo kuna wenye nacho na wasio nacho.. so mchango hauwez kuwa sawa kwa jinsi yoyote ile
Aaaah ha ha ha ha ha ha, nafanya tathmini ya huo Umma wanaojinadi nao ambao ndani ya masaa 48 umeshinda kujitokeza kwa idadi ya milioni moja kuchanga jero jero

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom