MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,011
- 16,748
Rais Mama Samia Suluhu Hassan ameendelea 'Kuchemka' kwa Kujiita ni Rais wa Awamu ya Sita ila amesahau kuwa Leo amehutubia Wabunge waliochaguliwa katika Awamu ya Tano.
Nao Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo muda mwingi walikuwa wakimfurahia, wakimpigia Makofi, wengine hadi kupiga Sarakasi katika Viti vyao na Kumuimbia Rais wa Awamu ya Sita Mama Samia Suluhu Hassan huku wao wakijitambua kuwa ni Wabunge wa Awamu ya Tano.
Huenda Mimi Generalist na baadhi ya Watanzania wenzangu wachache sana Wanaojitambua ( Werevu ) hatujui kuwa kumbe baada tu ya Kifo cha Hayati Rais Dkt. Magufuli tarehe 17 Machi, 2021 Kesho yake kulifanyika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ambapo Rais Samia akaibuka Mshindi wa Kura pamoja na Wabunge na kuwa rasmi ni Rais wa Awamu ya Sita pamoja na hao Wabunge na Madiwani.
Leo Watu wa Mitandaoni tumetishiwa na kuambiwa kuwa kumbe tunajulikana na wakikutaka basi muda wowote ule watatupata.
Nawapongeza kwa hilo ila Rais Mama Samia nae akae akijua kuwa wengine hata ikitokea tumekufa kwa Kulazimishwa ( Kuuawa ) kwa kuwa Wakosoaji wenye Mantiki humu Mitandaoni dhidi ya Utawala wake huwa tunafurahi kwani kwa Mwenyezi Mungu atatupokea kama Mashujaa wa kuwa Wakweli, siyo Waongo na kutopenda Unafiki wala Kujipendekeza Kwake.
Msimamo wangu Generalist ni ule ule tu kuwa Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Sita ndani ya ( katika ) Awamu ya Tano iliyo katika Muhula wake wa Pili ( wa mwisho )
Sipo katika Kundi la 'Vichwa Maji' wengi.