Hii inatokea na inawezekana tu Tanzania, hivyo acheni wenye Akili watucheke na watudharau kwani tumejitakia na tunastahili

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Rais Mama Samia Suluhu Hassan ameendelea 'Kuchemka' kwa Kujiita ni Rais wa Awamu ya Sita ila amesahau kuwa Leo amehutubia Wabunge waliochaguliwa katika Awamu ya Tano.

Nao Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo muda mwingi walikuwa wakimfurahia, wakimpigia Makofi, wengine hadi kupiga Sarakasi katika Viti vyao na Kumuimbia Rais wa Awamu ya Sita Mama Samia Suluhu Hassan huku wao wakijitambua kuwa ni Wabunge wa Awamu ya Tano.

Huenda Mimi Generalist na baadhi ya Watanzania wenzangu wachache sana Wanaojitambua ( Werevu ) hatujui kuwa kumbe baada tu ya Kifo cha Hayati Rais Dkt. Magufuli tarehe 17 Machi, 2021 Kesho yake kulifanyika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ambapo Rais Samia akaibuka Mshindi wa Kura pamoja na Wabunge na kuwa rasmi ni Rais wa Awamu ya Sita pamoja na hao Wabunge na Madiwani.

Leo Watu wa Mitandaoni tumetishiwa na kuambiwa kuwa kumbe tunajulikana na wakikutaka basi muda wowote ule watatupata.

Nawapongeza kwa hilo ila Rais Mama Samia nae akae akijua kuwa wengine hata ikitokea tumekufa kwa Kulazimishwa ( Kuuawa ) kwa kuwa Wakosoaji wenye Mantiki humu Mitandaoni dhidi ya Utawala wake huwa tunafurahi kwani kwa Mwenyezi Mungu atatupokea kama Mashujaa wa kuwa Wakweli, siyo Waongo na kutopenda Unafiki wala Kujipendekeza Kwake.

Msimamo wangu Generalist ni ule ule tu kuwa Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Sita ndani ya ( katika ) Awamu ya Tano iliyo katika Muhula wake wa Pili ( wa mwisho )

Sipo katika Kundi la 'Vichwa Maji' wengi.
 
Tunachokisema Sisi Watanzania ni kwamba, Mama aachwe afanye kazi na neema itapatikana kwa kila mmoja wetu.

Wasiomtakia mema Mheshimiwa rais wetu Mama yetu kipenzi Mama Samia Suluhu Hassan basi waendelee kutomtakia mema, ila Mungu amemchagua na kupitia yeye taifa letu litaneemeka sana.
 
Hiii ni awamu ya 5 kipindi cha pili hakuna awamu ya 6 ila kuna Rais wa 6 yupo pale kwa Kwa mujibu wa kifungu cha 37 (5) cha Katiba ya nchi hiyo iliyotungwa mwaka 1977

Article 37, subsection 5 states:

Where the office of President becomes vacant by reason of death, resignation, loss of electoral qualifications or inability to perform his functions due to physical infirmity…then the Vice-President shall be sworn in and become the President…
 
Tunachokisema Sisi Watanzania ni kwamba, Mama aachwe afanye kazi na neema itapatikana kwa kila mmoja wetu.

Wasiomtakia mema Mheshimiwa rais wetu Mama yetu kipenzi Mama Samia Suluhu Hassan basi waendelee kutomtakia mema, ila Mungu amemchagua na kupitia yeye taifa letu litaneemeka sana.
Kwahiyo Kumkosoa Rais Mama Samia ndiyo Kumchukia na Kumzuia asiweze Kutuongoza vizuri?

Hebu ficha basi Upumbavu wako sawa?
 
Mama anasisitiza kuwa hii ni awamu ya 6.
Nchi hii ilipata mapinduzi matukufu na muungano.
Kusanyo la kodi kwa sasa ni 1.9trillion kwa mwezi
Industrial park ni lazima
Kodi sio shuruti wala kutumia nguvu
Expatriates wapewe vibali bila kuadhiri wazawa
Usajili wa wawekezaji uharakishwe
Maongezi ya miaka 6 yanaenda kukamilishwa kwa vyovyote vile.
Waliosema Magu katangulizwa atawatafuta, ila wanaosema ni korona wako free ingawa yeye kasema ni moyo.

Kazi iendelee.
 
Msimamo wangu Generalist ni ule ule tu kuwa Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Sita ndani ya ( katika ) Awamu ya Tano iliyo katika Muhula wake wa Pili ( wa mwisho )

Sipo katika Kundi la 'Vichwa Maji' wengi.
Nakubaliana kabisa na wewe.

Samia Suluhu ni Rais wa sita lakini aliye wa awamu ya tano.

Siombei wala sitaki iwe hivyo, ila kwa mfano ikitokea Samia anakufa, basi Philip Mpango atakuwa Rais wa saba katika awamu ya tano.

Hatokuwa Rais wa awamu ya saba!

Kwangu mimi awamu zinaendana uchaguzi baada ya muhula wa Rais kuisha.

Muhula wa pili ya Rais Magufuli haujaisha. Yeye Magufuli kafariki. Na ilivyo kikatiba, makamu wake ndo amekuwa rais.

Not a big deal. But it’s as simple as 1,2,3.
 
wewe hamna bunge la awamu ya tano hili ni bunge la 12 au 13 kama sijakosea, bunge halina uhusiano na awamu za urais
Kwahiyo hawa Wabunge wa Awamu ya Sita ( kwa mujibu wake Rais Samia Suluhu Hassan mwenyewe ) wamechaguliwa katika Uongozi wa Rais Samia au wa Hayati Rais Dkt. Magufuli?

Nikiwadharau hamna 'Akili' msininunie!!
 
Kwahiyo Kumkosoa Rais Mama Samia ndiyo Kumchukia na Kumzuia asiweze Kutuongoza vizuri?

Hebu ficha basi Upumbavu wako sawa?
Nani ameleta habari za kumchukia?? Umelewa sio???

Upumbavu wenu na kosoa kosoa zenu zisizo na msingi hazina nafasi AWAMU hii.

Mheshimiwa rais Mama Samia hana muda wa kusikiliza kosoa kosoa za kipumbavu. Muda wake ameutenga kutumikia Watanzania
 
Back
Top Bottom