Hii imenitokea leo kwa shangazi!

Hii imenitokea leo kwa shangazi!

Ha ha ha haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa hii kali kuliko

Daaaah! simnajua tena Jamani daladala za Mwenge-Posta kuna Watoto Wazuri asikwambie Mtu, basi siku ilo asubuhi nimemuona mrembo mzuri maskini hata hawezi kugombania gari, nikaona hapa hapa ndio pa kuchukua ujiko! Nikapanda fasta nikawahi siti ya watu wawili halafu nikakaa katikati ili akija nimpishe,dah! Si likatokea libabu moja limevaa miwani kubwaa kama ya kukatia vitunguu likakaa! Duh linanuka tu sigara,

Yule Mrembo akasimama, limoyo likauma kweli!,Daladala ilipofika Makumbusho nikaona lile Babu linashuka, aisee kama zali na Mrembo akakaa!
Jaman Bahati iliyoje,nikalia nzisha,

DANNY : Mambo Mrembo.

MREMBO : poa,

DANNY : Karibu Karanga (nikatoa viujugu vya kuzugia)

MREMBO : silagi huo Uchafu,labda Pop Corn na Clips.

DANNY : Ok naitwa Chogomundu Pangalashaba, mwenzangu?

MREMBO : He he heee! Jina kama dawa!, mi naitwa Princess Rihanna!,

Wakati naendelea kupata majibu Machungu ghafla Nikaona Gari imefika Namanga, kwa kweli kama huyu mrembo angekuwa anatoa majibu ya kuridhisha ningeenda kushuka nae popote nikamwambia konda "Shusha Namanga", sasa wakati nashuka nikashangaa kumbe na yeye anashuka hapo
hapo!

DANNY : haa kumbe na wewe unashuka hapa?

YEYE : so what?

DANNY : ok umekataa karanga zangu, basi twende hapo kwa Mama ntilie tukagongechai,andazi maharage,

MREMBO : khaa! Unikome, mimi huwanatumia vitu kama Burger,Kuku, sausages,Pizza, Egg Chops na Chipsi Mayai, yaani Uzuri Wangu woote unilishe kwa Mama ntilie? KOMA!,

Dah Mrembo akasepa zake,nikaona hakuna Noma nikaagiza zangu Maharage ya 200,maandazimawili 200 na Chai ya 100, nikaacha kajero hapo nikasepa.

Nimefika Kwa Shangazi akafurahi kweli kuniona.

SHANGAZI : mwanangu Chogomundu Karibu Baba!,

DANNY: asante Shangazi

SHANGAZI: yule mwanangu wa Mwisho unamkumbuka?

DANNY : Si yule Kipandauso?

SHANGAZI: huyo huyo!

DANNY : namjua vizuri,wakati anakuwa namuona,hata nepi nimembadili teh!, yupo wapi siku hizi?

SHANGAZI : amekuwa mkubwa kweli, anasoma Hapo Chuo Cha Kodi TRA pale karibu na ITV, ila yupo alienda Chuo akahisi homa kaona arudi,njoja nimuite,Kipandausooooo! !!

KIPANDAUSO : beeee Mama!

SHANGAZI : Njoo mwanangu,kuna Mgeni!

Hamad! Ndipo Macho yangu yakakutana na Yule Mrembo wa Kwenye daladala, kavaa vitenge vya zamani vya Shangazi, hana Wigi tena,muda huu komwe la ukoo linaonekana, komwe la babu yetu!, mrembo kashika sahani ya Maboga na kikombe cha uji wa Mchele!, Aliponiona Almanusura azimie!!!,
huyu ndiye Kipandauso, Mtoto wa Mwishowa Mjomba Dindoyogo!, ukipenda Muite Kipandauso Dindoyogo!

SHANGAZI : Njoo na Maboga ya kutosha nakikombe kingine cha uji uje unywe na Kaka yako! Dah! akarudi ndani kinoma nomakainamisha sura chini, mi
nikawa najiulizawapi Pizza? Wapi Burger? Wapi Sausage?,anyway bado nipo hapa kwa Shangazi mpaka baadae.
 
Mods mwongozo tafadhali, lifunguliwe jukwaa la watoto...kwa ajili ya watoto kama mtoa mada

Msikariri jamani sio kila muda wa habari ngumu ngumu tu. Muda mwingine akili inahitaji kupumua kidogo.
Halafu ukiona kitu hakijakuvutia unapita kimya kimya unaenda kwenye siasa kule na majukwaa mengine ya kukupa kile unachohitaji
 
Mtoa mada acha kutudanganya wazoefu, hayo maharage ya 200/= na chai na maandazi ya 100/= hayapo siku hizi. Unatudanganya hadi maeneo tuliyobobea? Mwaka wa 20 huu nakula kwa mama ntilie mwenzako

kweli maharage ya 200 na chai ya mia hakuna
 
Hahahahahah nimecheka ati princess rihanna alafu uongo wako umezidi hivi kuna chai ya 100 na maharage ya 100 jamani?

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
nimepata hamu ya maboga na viazi vitamu vya kuchemsha........

nitavipata wapi hapa mjini?[/QUOTE

Huku musoma vipo kwa wingi,nilivyofika nilikuwa navitumia sn,basi wenyeji wakawa wananishangaa kumbe hawajui mwenzao huko nitokako ni vitu adimu.
 
Msikariri jamani sio kila muda wa habari ngumu ngumu tu. Muda mwingine akili inahitaji kupumua kidogo.
Halafu ukiona kitu hakijakuvutia unapita kimya kimya unaenda kwenye siasa kule na majukwaa mengine ya kukupa kile unachohitaji

ahsante kwa kuliona hlo yan kuna mtu zinaroho km paka huku
 
Mhh! Jamaa kapitiliza kwa uongo. Kama ni kweli alikuwa anaenda kwa shangazi asubuhi, ni kwa nini anywe chai njiani? Si angeenda kunywa huko kwa shangazi? Halafu Namanga hakuna mama ntilie wala andazi la sh. 100!

unaisha mkoa gan
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom