Hii imekaaje kupatwa kwa jua kuwa Njombe dunia nzima?

Mzururaji

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,559
1,272
Hii imekaaje dunia nzima kupatwa kwa jua kuonekane njombe tuuu
Ina maana dunia nzima inatokea Tanzania tu tena njombe peke yake?

Je Tanzania nzima jua si hili hili moja kwa nini likipatwa lisionekane kote au kote kuwe Giza
Naomba tusaidiane wadau mana naona hii kama fursa kwa Tanzania yetu harafu mi sielewi
 
Vyombo vya habari vingi hapa kwetu vimetilia sana chumvi na ndicho ambacho wamekuwa wakikitangaza kwa wiki kadhaa ... pengine inawasaidia kibiashara.

Ukweli ni kwamba, Tanzania ni sehemu pekee utakayoweza kuona kwa uzuri sana kupatwa huku kwa jua mapema kesho, lakini kuna maeneo mengine pia dunia utakayoweza kuona japo si kwa uzuri kama Mbeya ikiwemo Uingereza kwa siku ya Ijumaa.

Tembelea: @http://www.space.com/33784-solar-eclipse-guide.html
 
hahahaha mkuu kupatwa kwa jua hakuwezi tokea dunia nzima hata siku moja. inatokeaga ktk certain areas ambazo kwa bahati zinakuwa kwenye mstari(alignment) na mwezi.of coz ni zali tu huwainatokea kwani ktk dunia nzima ni maeneo machache tu huwa yana experience hyo hali
 
Njombe wameona fursa wameitumia kutangazwa kwenye vyombo vya habari,japo hata waliopo mkoa wa Mbeya wataona vizuri
 
Hapo ndio focal point ya kupatwa kwa jua yaani ndio kiini cha intersection kati ya jua na dunia zitakapopishana.
 
Hapo ndio focal point ya kupatwa kwa jua yaani ndio kiini cha intersection kati ya jua na dunia zitakapopishana.
Uko sahihi kabisa,ila hapo pana maelezo marefu kidogo kwa asiyekuwa na uelwa kuweza kuelewa.
 
Kwa maelezo madogo kupatwa kwa jua ni kitendo cha mwezi kua katikati ya jua na dunia kama mnavyojua mwezi na dunia huwa vinalizunguka jua.

Sasa katika kulizunguka jua ambalo ndio chanzo kikuu cha mwanga pale ambapo mwezi unatia uzibe mbele ya jua kunatokea kivuli cha mwezi juu ya dunia ambapo ndio eneo hilo kunaonekana kama usiku japo ni mchana

hilo tukio ndio linaitwa kupatwa kwa jua yaani kivuli cha mwezi juu ya dunia (sio kivuli juu ya dunia yote bali ni kijisehemu kidogo ambapo kwa awamu hii ndio patakuwa hapo wanging'ombe) japo na pembezoni pia patatokea japo giza halitakua kali kama kwenye hicho kiini.

_88644788_solar_eclipse_466in.jpg

Ikumbukwe mwezi hautoi mwanga kama wengi wanavyodhani waonapo mwezi unawaka usiku.
Bali mwezi unaakisi mwanga wake kutoka kwenye jua na kuutupa duniani.
 
Kwa maelezo madogo kupatwa kwa jua ni kitendo cha mwezi kua katikati ya jua na dunia kama mnavyojua mwezi na dunia huwa vinalizunguka jua.

Sasa katika kulizunguka jua ambalo ndio chanzo kikuu cha mwanga pale ambapo mwezi unatia uzibe mbele ya dunia kunatokea kivuli cha mwezi ambapo ndio eneo hilo kunaonekana kama usiku japo ni mchana

hilo tukio ndio linaitwa kupatwa kwa jua yaani kivuli cha mwezi juu ya dunia (sio kivuli juu ya dunia yote bali ni kijisehemu kidogo ambapo kwa awamu hii ndio patakuwa hapo wanging'ombe) japo na pembezoni pia patatokea japo giza halitakua kali kama kwenye hicho kiini.

_88644788_solar_eclipse_466in.jpg

Ikumbukwe mwezi hautoi mwanga kama wengi wanavyodhani waonapo mwezi unawaka usiku.
Bali mwezi unaakisi mwanga wake kutoka kwenye jua na kuutupa duniani.
Umemaliza kila Kitu hata ambaye hakusoma ataelewa picha. Thank you.
 
Back
Top Bottom