Hii hapa Picha nyingine bora ya Wiki hii, Imepigwa Tabora

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,789
218,427
Kitu kingine nilichokiona kwenye utawala uliopita ni wananchi kukosa kabisa Uhuru, Amani , furaha na Upendo, kiasi cha kila mtu kuona mwenzake ni Adui.

Kumbe Uhuru, Upendo na Amani vinazalisha Furaha.

Hebu angalia Picha hii halafu toa maoni yako.

JamiiForums1556955921_540x378.jpg
 
Commissioned officers, presidential appointees nadhani hao ndo wenye sifa ya kupigiwa salute

Huyo mangi anafit wapi kwenye hizo criteria tajwa hapo juu
Yaani unaona salute ni kitu cha maana sana! Ingekuwa hilo jeshi lina maadili ungeweza kusema hili. Lakini sio kwa matendo yao machafu na kutumika hovyo na viongozi wa kisiasa hasa wa ccm kinyume na sheria. Na ushahidi wa hilo upo wazi.
 
Yaani unaona salute ni kitu cha maana sana! Ingekuwa hilo jeshi lina maadili ungeweza kusema hili. Lakini sio kwa matendo yao machafu na kutumika hovyo na viongozi wa kisiasa hasa wa ccm kinyume na sheria. Na ushahidi wa hilo upo wazi.
Najua huna ushahidi juu ya suala hili, ila kitendo cha huyo constable kumpigia salute huyo jamaa kinahitaji maelezo marefu sana
 
Kitu kingine nilichokiona kwenye utawala uliopita ni wananchi kukosa kabisa Uhuru , Amani , furaha na Upendo , kiasi cha kila mtu kuona mwenzake ni Adui .

Kumbe Uhuru , Upendo na Amani vinazalisha Furaha .

Hebu angalia Picha hii halafu toa maoni yako .

View attachment 2639634

Hii ndiyo Police Services inayodaiwa kutiwa katika katiba mpya ili jeshi la Polisi litimize wajibu wake bila upendeleo wala kuburuzwa kutumika vibaya dhidi ya raia.

Mwanzo mzuri kwa jeshi la Polisi, muhimu hili jambo litiwe ktk katiba tuepukane na yale ya awamu ya 5 kutumia jeshi la polisi kuwa kama jeshi binafsi la chama fulani - paramilitary

Tunajua jeshi la polisi lilikuwa halipendi kutumika vibaya lakini katiba mbovu iliyochukua hulka za kutoka jeshi la polisi la mkoloni inawabana. Katiba mpya itafanya polisi wetu kuwa jeshi la kulinda mali na usalama wa raia badala ya kutumika kama jeshi binafsi la watawala.


Tazama salute ya askari polisi huyu iliyoambatana na sura ya furaha anayejisikia ametua mzigo mzito wa lawama waliobebeshwa na CCM.
 
Salute ni sawa na neno shikamoo.
Mbowe ni mtu mzima kwa umri na mwenye status yake mwacheni apigiwe saluti akiwa hao sio siku akifa ndio muanze kupiga saluti na kuinama kwenye jeneza lake.
Mpeni maua yake acheni kubana bana hiyo kitu
 
Back
Top Bottom