Hii hapa orodha ya wanahiphop bora wa muda wote Tanzania

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,224
22,305
Wakuu pamoja na kupenda siasa za CCM ila pia mimi ni mnazi mkubwa wa muziki wa Hiphop. Tangu utotoni nimekua nikipenda Hiphop. Nimekuwa nikisikiliza nyimbo za GWM, Mr II, Dollar Soul, JCB & Watengwa, Nako2Nako, Juakali, hadi hawa waliopo kwenye chati kina PMawenge.

Nikiwa mdogo nilikuwa napenda sana kwenda pale Uwanja wa basketball Soweto, Arusha kutazama matamasha ya hiphop yaliyokuwa yakifadhiliwa na Sprite. Kiufupi mimi ni mwanafamilia wa Hiphop.

Hii hapa orodha tukufu ya wanahiphop bora kuwahi kutokea nchini, inaanza na bora zaidi hadi namba 10:

1. Mr II (Sugu) - haihitaji kubishana kwamba huyu Joseph Mbilinyi ambaye pia ni mbunge mstaafu wa CHADEMA na mnufaika wa michango ya join The chain kuwa ni mwanahiphop bora zaidi wa muda wote nchini. Ana alama nyingi sana kwenye hiphop Tanzania.

2. Profesa Jay - huyu ni binadamu anayependwa na kila mtu bila kujali itikadi. Kwenye hiphop ya Tanzania ana alama zake zisizofutika.

3. Mikiller Gego - ni mwanahiphop ambaye pia ni mhandisi kitaaluma. He is a scientist & artist. Nyimbo na makala zake zimewagusa hadi wapenzi wa muziki wa Taarabu.

4. Lord Eyes - member wa N2N na sasa Weusi. Kwakweli kwa zile flow alizo nazo Lord Eyes angeweza hata kuwa namba moja sema ana matatizo binafsi ya nje ya Hiphop yanayomfanya ubora wake mara nyingi ushuke.

5. Joh Makini - mwamba wa kaskazini haina haja ya kumzungumzia sana kwa sababu anaeleweka balaa lake.

6. Chid Benz - pamoja na kuwa teja lakini Chid Benz ni mwanahiphop bora wa muda wote. Haihitaji ubishi.

7. Nikki wa II - Ubora wake kwenye Hiphop ulifanya hadi ikulu imtambue na kumteua aisaidie nchi kwenye uongozi ngazi ya ukuu wa wilaya. Ni mwanahiphop anayetajwa kumiliki mtoto mkali hatari yaani MASHINE MNATO.

8. Fid Q - Ngosha the Don hana mambo mengi yanayomfanya awepo kwenye hii orodha tukufu zaidi ya kipaji chake.

9. Nikki Mbishi - ubishi wake ni talent.

10. Dogojanja - hakuna dogo anayeweza kuchana kama yeye.

UPDATE; Kutokana na maombi ya wengi wenu ninaongeza majina namba 11 hadi 20.

11. Zay B - yupo gado. Alibamba miaka ya 2000 mwanzoni na kisha kupotea kabisa.

12. MwanaFA - binamu.

13. Witness - huyu alikuwa na kundi lao na kina Marehemu Langa.

14. Chindo Man (Umbwax)

15. JCB - ukisikia Paah ujue imekukosa.

16. Azma Mponda (Aznas)

17. KR - muziki mnene CD 700.

18. Mansu Li

19. Kala Jeremia

20. Jay Moe.
 
N.W.A niggaz with attitude. the most dangerous group in the world 🌍. Hapo kwenye list Yako nimemuona Nikki mbishi na msukuma pekee tz🇹🇿 kwenye familia ya hip hop #fid_Q
 
4✓
5✓
7✓

List ipo vizuri japo hujaweka in good order

Ilipaswa iwe hivi

1) Joh Makini
2) Professa
3) Lord Eyes
4) Fid
5) Nikki wa Pili
6) Afande Sele
7) Chid Benz
8) Jay Moe
9) Kalapina
10) Sugu

Dogo janja ni mzuri sana but kwa top 10 nahisi bado kuna wakongwe wamemzidi kidogo

Nikki mbishi huyo hata top 20 hawezi kuwemo, ni wa level za kiunderground.
 
Janjaro wa my banana, kamuacha Mr blue heshima ya bongo hip hop, kafikisha miaka 20 juzi tu hapa toka aingie kwenye game.
 
Back
Top Bottom