Hii hapa nyumba pekee ya Askofu Kakobe

Aisee kuna mmoja yupo huku Arusha kisongo ni balaa,,Kondoo wanaliwa sadaka balaa afu walivyo wapole Maskini wanatoa tu hata hawaulizi.
 
Zaidi ya saa 24 sasa zimepita tangu uzi huu uwekwe hapa, na hakuna hata mtu mmoja duniani aliyeweka hapa vielelezo vya majumba ya kifahari na maisha ya kifahari ya Askofu Kakobe. Zilizoko hapa tu muda wote ni blabla tu za "labda". Baadhi ya Watanzania, wanapenda kukaririshwa tu maneno ya mitaani ya "redio mbao"! Tujifunze kutokuamini kila jambo na kulisambaza kwa wengine, bila sisi wenyewe kulifanyia utafiti. Matokeo ya uongo, siku zote ni fedheha!!!!!!!!!

fanya siku moja mumpige akiwa hapo nje ya hiyo nyumba. Btw, me sijasema kwamba anaishi maisha ya kifahari. ninachouliza ni kwamba, mbona hiyo nyumba ina ukungu kana kwamba hakuna anayeishi hapo? au wewe hulioni hilo?
 
Huku ni kutapatapa kwa mfa maji! Tangu lini ukungu kwenye rangi ya ukuta ukazuia watu kuishi kwenye nyumba?
 
Aisee kuna mmoja yupo huku Arusha kisongo ni balaa,,Kondoo wanaliwa sadaka balaa afu walivyo wapole Maskini wanatoa tu hata hawaulizi.
*********************************************************************************************
Hapa tunajadili kuhusu mada iliyoletwa "Hii hapa nyumba pekee ya Askofu Kakobe".Baadhi ya watu wamekuwa wakiwadanganya watu kwa vitu visivyo na ukweli sasa wameambiwa mwenye kukanusha taarifa hii alete ushahidi,kimya na watu wanadhania tu na kuleta blabla tu zisizo na ushahidi.Mwisho wa uongo ni fadheha.Wanaodhani kila mtu ni fisadi wamekosea sana!.
 
tuambie kwanza dhaka na sadaka zinaenda wapi afu ndyo ulete prnpangada zako

ni kweli kabisa, hizo tu ndiyo mali zake binafsi askofu kakobe. Mimi nimekuwa muumini wa kanisa la fgbf, kwa miaka 25 sasa, yaani tangu lilipoanzishwa 1989. Muda huu mrefu, umenipa kumfahamu kwa karibu sana, mchungaji wangu huyu. Ninathibitisha kwamba haya ndiyo maisha halisi ya askofu kakobe, tofauti na uzushi mwingi wa mashetani. Mtumishi huyu wa mungu, analiishi hasa neno la mungu analolihubiri; ndiyo maana waumini tunampenda, kumwamini na kumheshimu; na makelele yote ya mashetani, hayawezi kututenganisha naye. Ninapafahamu mpaka kijijini kwake askofu mkuu kakobe, huko kakonko, kigoma. Kijijini kwake, nako, hana hata banda. Miaka yote hii, akienda kijijini, amekuwa akifikia kwenye nyumba ndogo ya wazazi wake, frank kakobe, na debora kakobe, waliofariki muda si mrefu uliopita. """"[ ungetumia " miezi michache iliyopita ] au [ siku chache zilizopita ]""" ……

kiswahili ni janga .
 
Zaka na sadaka zimefanya kazi kubwa ya Mungu nchi nzima. Majengo ya Makanisa yamejengwa kila kona ya nchi, kila wilaya Tanzania bara, mpaka vijiji vya ndani ndani kabisa. Nenda katika tovuti ya Kanisa: www.fgbfchurch.org katika ukurasa wa matawi ya Kanisa, ili ujionee picha makumi kwa makumi za majengo ya Makanisa haya.

Daah pamoja na kua kakobe is my best pastor kwa tanzania(mimi sio mlokole) lakini suala la kujenga makanisa mikoani limebaki mikononi mwa waumini wenyewe hakuna mchango toka makao makuu wala nini,naongea kwa evidence mfano kanisa la masasi limejengwa kwa nguvu ya waumini na mchungaji wa masasi(dickson) ni mjomba angu kabisa thatbis why alipo amua kujitenga na full gospel kakobe hakuwa na nguvu ya kumzuia....
 
attachment.php

attachment.php

Hii hapa, ndiyo nyumba pekee ya Askofu Mkuu Zachary Kakobe, kama wanavyothibitisha waumini wake, na watu wengi wanaofahamu undani wa maisha yake binafsi. Ni nyumba ya kawaida sana ya vyumba vinne, iliyojengwa katika mtaa wenye nyumba ambazo zimebanana sana, bila kuacha nafasi; eneo la Kijitonyama, Dar-Es-Salaam; umbali mfupi kutoka Kituo cha Polisi, Mabatini.

Kakobe, aliijenga nyumba hii, mwaka 1986, kutokana na kazi aliyokuwa akiifanya, na biashara zake binafsi alizokuwa akizifanya, nyakati hizo; kabla ya kuitika wito wa kumtumikia Mungu. Nyumba hii aliijenga kwa gharama ya shilingi milioni mbili tu (Tsh 2,000,000/=) miaka hiyo, ambapo gharama ya ujenzi Tanzania, ilikuwa haijakuwa kubwa, kama ilivyo sasa. Wakati Kakobe anajenga nyumba hii, Kanisa analoliongoza sasa, la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), lilikuwa bado halijaanzishwa. Kanisa hili, lilianzishwa miaka mitatu baadaye, yaani tarehe 30.4.1989. Mpaka leo, miaka 25 tangu Kanisa hili lianzishwe, Kakobe hajawahi kuishi katika nyumba nyingine au kuwa na nyumba yake nyingine yoyote.

Askofu Kakobe, ana gari moja tu binafsi, "unaloweza kusema kuwa ni gari"; ambalo alipewa zawadi na waumini 84 (themanini na wanne), waliochangishana kwa hiari, wenyewe kwa wenyewe; bila yeye kujua, na wakanunua gari hilo na kulileta Kanisani Jumapili ya tarehe 27.6.2010, bila kumpa taarifa; na kwa kumshitukiza, wakajitokeza mwisho wa ibada, na "kumlazimisha" kupokea zawadi hiyo, kutoka kwao. "Walimlazimisha" kwa risala ndefu, kwa sababu, huko nyuma, aliwahi kupewa mara kadha, zawadi za magari, na baadhi ya waumini, na akayakataa magari yao.
Gari jingine, ni la mke wake Hellen, gari dogo "Toyota Sprinter", mtumba au "used", lenye umri wa miaka takriban 20, alilopewa na waumini watatu akina mama, kama zawadi, mwaka 2007. Vilevile, hakuna mtoto wake yeyote mwenye nyumba au gari.

Hii, ni kinyume kabisa na maneno mengi yanayosikika mitaani, kwa baadhi ya watu, wanaosema kwamba Kakobe anaishi maisha ya kifahari kupindukia, ana majumba mengi ya kifahari, na magari mengi sana ya binafsi, na mali nyingi alizojilimbikizia binafsi, kutokana na "biashara" ya "Kanisa lake".

Akizirejea mali zake hizi, zilizotajwa hapo juu; kwa miaka kadha sasa, Askofu Kakobe amekuwa akizungumzia juu ya mali zake binafsi, katika vyombo mbalimbali vya habari, na kusema kama ifuatavyo, nami ninamnukuu, "Mimi sina nyumba yoyote zaidi ya hii, MAHALI POPOTE DUNIANI, siyo kijijini kwangu, wala mji wowote duniani; na vivyo hivyo mke na watoto wangu wote, hakuna hata mmoja mwenye nyumba mahali popote duniani. Siyo hilo tu, mimi wala mke wangu, hatuna biashara yoyote, shamba, wala mifugo, popote duniani; vilevile, mimi, wala mke wangu, hatuna akaunti binafsi ya fedha, katika BENKI YOYOTE DUNIANI. Kama yuko mtu yeyote mwenye taarifa zozote zilizo tofauti na hizi, basi ajitokeze na kuweka ushahidi hadharani na kuniumbua". Kwa miaka kadha sasa, tangu aseme hivi; hakuna hata mtu mmoja, aliyejitokeza hadharani kutoa ushahidi wa mali zake nyingine, kwa picha, au vyovyote vinginevyo.

Kwa kuwa hapa JF, ni "WHERE WE DARE TO TALK OPENLY", au mahali tunapothubutu kuzungumza kwa uwazi, bila hofu; ili kukata mzizi wa fitina, ebu basi, mtu yeyote hapa, anayejua mali nyingine binafsi za Kakobe, na ufahari wa maisha yake binafsi, wa namna moja au nyingine, ajitokeze hapa, na kutujuza kwa ushahidi wa picha, au vinginevyo; na siyo kwa uzushi tu wa kuambiwa, ili tujue hasa, ukweli ni upi! NAWASILISHA.

Hii story inanikumbusha drama inaitwa "the trials of brother Jero" waliopata kusoma wanajua namaanisha nini!
 
Haya ni maneno ya mfa maji ambaye haachi kutapatapa. Hii ni karibu siku ya nne sasa, tangu uzi huu umewekwa hapa, na hakuna hata mtu mmoja duniani ambaye ameweka hapa, vielelezo vya majumba na mali za kifahari za Askofu Kakobe. Wengi wameshituka na kujua walidanganywa na redio mbao, wewe bado unaendelea kuleta habari za drama hapa! Kinachotakiwa hapa ni VIELELEZO vya maisha ya kifahari ya Kakobe, na siyo blabla za drama ya Jero. Hadanganyiki mtu hapa!
 
Umesema kweli hasa! Hongera kubwa !!! X 7.Uongo na uzushi dawa yake ni ukweli kuwekwa hadharani.Wameumbuliwa kweli kweli.Katika mazingira ya wengi kuishi kwa ujanja ujanja wanadanganywa na kudhani Askofu Kakobe anaishi kama wao!Kumbe ni tofauti kabisa.Hajapatikana yeyote duniani wa kuleta ushahidi wa maisha ya ufahari ya Askofu Kakobe!
 
Sikuzote penye ukweli uongo hujitenga, "Hii hapa nyumba pekee ya Askofu Kakobe".Ukweli umewekwa hapa na mwenye kuukanusha ukweli huu alete ushahidi usio na shaka hapa JF.Uongo na uzushi sikuzote haulipi!Ukweli ndio unaoweza kutuweka huru.Nathibitisha bila unafiki wowote ndani yangu kwamba ni kweli kwa asilimia zote hii ndiyo nyumba pekee ya Askofu Kakobe.

Hii mada ni ya moto naona watu wanarukaruka tu hata mwenye ushahidi simwoni.
 
Haya ni maneno ya mfa maji ambaye haachi kutapatapa. Hii ni karibu siku ya nne sasa, tangu uzi huu umewekwa hapa, na hakuna hata mtu mmoja duniani ambaye ameweka hapa, vielelezo vya majumba na mali za kifahari za Askofu Kakobe. Wengi wameshituka na kujua walidanganywa na redio mbao, wewe bado unaendelea kuleta habari za drama hapa! Kinachotakiwa hapa ni VIELELEZO vya maisha ya kifahari ya Kakobe, na siyo blabla za drama ya Jero. Hadanganyiki mtu hapa!

kaisome hiyo drama ndo utajua namaanisha nini. usikurupuke mkuu!
 
teh teh teh...yamekuwa yakufatilia drama tena, kwa hiyo ushahidi unapatikana kwenye drama?
Mi sio mshabiki wa wa kidini ila hapa wapinzani wa hii thread naona kama mnafuka mimoshi!
 
inawezekana na wewe ni mmoja wao? kana kama Petro tuone!
 
Ubarikiwe kwa kuwaeleza kweli,waongo wote !!! Ni mimi naifahamu nyumba hii ya baba askofu mkuu Kakobe.:israel:

attachment.php

attachment.php

Hii hapa, ndiyo nyumba pekee ya Askofu Mkuu Zachary Kakobe, kama wanavyothibitisha waumini wake, na watu wengi wanaofahamu undani wa maisha yake binafsi. Ni nyumba ya kawaida sana ya vyumba vinne, iliyojengwa katika mtaa wenye nyumba ambazo zimebanana sana, bila kuacha nafasi; eneo la Kijitonyama, Dar-Es-Salaam; umbali mfupi kutoka Kituo cha Polisi, Mabatini.

Kakobe, aliijenga nyumba hii, mwaka 1986, kutokana na kazi aliyokuwa akiifanya, na biashara zake binafsi alizokuwa akizifanya, nyakati hizo; kabla ya kuitika wito wa kumtumikia Mungu. Nyumba hii aliijenga kwa gharama ya shilingi milioni mbili tu (Tsh 2,000,000/=) miaka hiyo, ambapo gharama ya ujenzi Tanzania, ilikuwa haijakuwa kubwa, kama ilivyo sasa. Wakati Kakobe anajenga nyumba hii, Kanisa analoliongoza sasa, la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), lilikuwa bado halijaanzishwa. Kanisa hili, lilianzishwa miaka mitatu baadaye, yaani tarehe 30.4.1989. Mpaka leo, miaka 25 tangu Kanisa hili lianzishwe, Kakobe hajawahi kuishi katika nyumba nyingine au kuwa na nyumba yake nyingine yoyote.

Askofu Kakobe, ana gari moja tu binafsi, "unaloweza kusema kuwa ni gari"; ambalo alipewa zawadi na waumini 84 (themanini na wanne), waliochangishana kwa hiari, wenyewe kwa wenyewe; bila yeye kujua, na wakanunua gari hilo na kulileta Kanisani Jumapili ya tarehe 27.6.2010, bila kumpa taarifa; na kwa kumshitukiza, wakajitokeza mwisho wa ibada, na "kumlazimisha" kupokea zawadi hiyo, kutoka kwao. "Walimlazimisha" kwa risala ndefu, kwa sababu, huko nyuma, aliwahi kupewa mara kadha, zawadi za magari, na baadhi ya waumini, na akayakataa magari yao.
Gari jingine, ni la mke wake Hellen, gari dogo "Toyota Sprinter", mtumba au "used", lenye umri wa miaka takriban 20, alilopewa na waumini watatu akina mama, kama zawadi, mwaka 2007. Vilevile, hakuna mtoto wake yeyote mwenye nyumba au gari.

Hii, ni kinyume kabisa na maneno mengi yanayosikika mitaani, kwa baadhi ya watu, wanaosema kwamba Kakobe anaishi maisha ya kifahari kupindukia, ana majumba mengi ya kifahari, na magari mengi sana ya binafsi, na mali nyingi alizojilimbikizia binafsi, kutokana na "biashara" ya "Kanisa lake".

Akizirejea mali zake hizi, zilizotajwa hapo juu; kwa miaka kadha sasa, Askofu Kakobe amekuwa akizungumzia juu ya mali zake binafsi, katika vyombo mbalimbali vya habari, na kusema kama ifuatavyo, nami ninamnukuu, "Mimi sina nyumba yoyote zaidi ya hii, MAHALI POPOTE DUNIANI, siyo kijijini kwangu, wala mji wowote duniani; na vivyo hivyo mke na watoto wangu wote, hakuna hata mmoja mwenye nyumba mahali popote duniani. Siyo hilo tu, mimi wala mke wangu, hatuna biashara yoyote, shamba, wala mifugo, popote duniani; vilevile, mimi, wala mke wangu, hatuna akaunti binafsi ya fedha, katika BENKI YOYOTE DUNIANI. Kama yuko mtu yeyote mwenye taarifa zozote zilizo tofauti na hizi, basi ajitokeze na kuweka ushahidi hadharani na kuniumbua". Kwa miaka kadha sasa, tangu aseme hivi; hakuna hata mtu mmoja, aliyejitokeza hadharani kutoa ushahidi wa mali zake nyingine, kwa picha, au vyovyote vinginevyo.

Kwa kuwa hapa JF, ni "WHERE WE DARE TO TALK OPENLY", au mahali tunapothubutu kuzungumza kwa uwazi, bila hofu; ili kukata mzizi wa fitina, ebu basi, mtu yeyote hapa, anayejua mali nyingine binafsi za Kakobe, na ufahari wa maisha yake binafsi, wa namna moja au nyingine, ajitokeze hapa, na kutujuza kwa ushahidi wa picha, au vinginevyo; na siyo kwa uzushi tu wa kuambiwa, ili tujue hasa, ukweli ni upi! NAWASILISHA.

attachment.php

attachment.php

Hii hapa, ndiyo nyumba pekee ya Askofu Mkuu Zachary Kakobe, kama wanavyothibitisha waumini wake, na watu wengi wanaofahamu undani wa maisha yake binafsi. Ni nyumba ya kawaida sana ya vyumba vinne, iliyojengwa katika mtaa wenye nyumba ambazo zimebanana sana, bila kuacha nafasi; eneo la Kijitonyama, Dar-Es-Salaam; umbali mfupi kutoka Kituo cha Polisi, Mabatini.

Kakobe, aliijenga nyumba hii, mwaka 1986, kutokana na kazi aliyokuwa akiifanya, na biashara zake binafsi alizokuwa akizifanya, nyakati hizo; kabla ya kuitika wito wa kumtumikia Mungu. Nyumba hii aliijenga kwa gharama ya shilingi milioni mbili tu (Tsh 2,000,000/=) miaka hiyo, ambapo gharama ya ujenzi Tanzania, ilikuwa haijakuwa kubwa, kama ilivyo sasa. Wakati Kakobe anajenga nyumba hii, Kanisa analoliongoza sasa, la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), lilikuwa bado halijaanzishwa. Kanisa hili, lilianzishwa miaka mitatu baadaye, yaani tarehe 30.4.1989. Mpaka leo, miaka 25 tangu Kanisa hili lianzishwe, Kakobe hajawahi kuishi katika nyumba nyingine au kuwa na nyumba yake nyingine yoyote.

Askofu Kakobe, ana gari moja tu binafsi, "unaloweza kusema kuwa ni gari"; ambalo alipewa zawadi na waumini 84 (themanini na wanne), waliochangishana kwa hiari, wenyewe kwa wenyewe; bila yeye kujua, na wakanunua gari hilo na kulileta Kanisani Jumapili ya tarehe 27.6.2010, bila kumpa taarifa; na kwa kumshitukiza, wakajitokeza mwisho wa ibada, na "kumlazimisha" kupokea zawadi hiyo, kutoka kwao. "Walimlazimisha" kwa risala ndefu, kwa sababu, huko nyuma, aliwahi kupewa mara kadha, zawadi za magari, na baadhi ya waumini, na akayakataa magari yao.
Gari jingine, ni la mke wake Hellen, gari dogo "Toyota Sprinter", mtumba au "used", lenye umri wa miaka takriban 20, alilopewa na waumini watatu akina mama, kama zawadi, mwaka 2007. Vilevile, hakuna mtoto wake yeyote mwenye nyumba au gari.

Hii, ni kinyume kabisa na maneno mengi yanayosikika mitaani, kwa baadhi ya watu, wanaosema kwamba Kakobe anaishi maisha ya kifahari kupindukia, ana majumba mengi ya kifahari, na magari mengi sana ya binafsi, na mali nyingi alizojilimbikizia binafsi, kutokana na "biashara" ya "Kanisa lake".

Akizirejea mali zake hizi, zilizotajwa hapo juu; kwa miaka kadha sasa, Askofu Kakobe amekuwa akizungumzia juu ya mali zake binafsi, katika vyombo mbalimbali vya habari, na kusema kama ifuatavyo, nami ninamnukuu, "Mimi sina nyumba yoyote zaidi ya hii, MAHALI POPOTE DUNIANI, siyo kijijini kwangu, wala mji wowote duniani; na vivyo hivyo mke na watoto wangu wote, hakuna hata mmoja mwenye nyumba mahali popote duniani. Siyo hilo tu, mimi wala mke wangu, hatuna biashara yoyote, shamba, wala mifugo, popote duniani; vilevile, mimi, wala mke wangu, hatuna akaunti binafsi ya fedha, katika BENKI YOYOTE DUNIANI. Kama yuko mtu yeyote mwenye taarifa zozote zilizo tofauti na hizi, basi ajitokeze na kuweka ushahidi hadharani na kuniumbua". Kwa miaka kadha sasa, tangu aseme hivi; hakuna hata mtu mmoja, aliyejitokeza hadharani kutoa ushahidi wa mali zake nyingine, kwa picha, au vyovyote vinginevyo.

Kwa kuwa hapa JF, ni "WHERE WE DARE TO TALK OPENLY", au mahali tunapothubutu kuzungumza kwa uwazi, bila hofu; ili kukata mzizi wa fitina, ebu basi, mtu yeyote hapa, anayejua mali nyingine binafsi za Kakobe, na ufahari wa maisha yake binafsi, wa namna moja au nyingine, ajitokeze hapa, na kutujuza kwa ushahidi wa picha, au vinginevyo; na siyo kwa uzushi tu wa kuambiwa, ili tujue hasa, ukweli ni upi! NAWASILISHA.
Usidanganyike na hilo ndugu kuna watu wanamiliki magorofa mjini lkn nyumba wanazoishi ni za kawaida tu!
 
Back
Top Bottom