Hii hapa nyumba pekee ya Askofu Kakobe

Mleta mada umeshinda ushahidi hakuna.. ila Gwanjima sio mtumishi wa mungu.. ni mfanya biashara ya dini
 
attachment.php

attachment.php

Hii hapa, ndiyo nyumba pekee ya Askofu Mkuu Zachary Kakobe, kama wanavyothibitisha waumini wake, na watu wengi wanaofahamu undani wa maisha yake binafsi. Ni nyumba ya kawaida sana ya vyumba vinne, iliyojengwa katika mtaa wenye nyumba ambazo zimebanana sana, bila kuacha nafasi; eneo la Kijitonyama, Dar-Es-Salaam; umbali mfupi kutoka Kituo cha Polisi, Mabatini.

Kakobe, aliijenga nyumba hii, mwaka 1986, kutokana na kazi aliyokuwa akiifanya, na biashara zake binafsi alizokuwa akizifanya, nyakati hizo; kabla ya kuitika wito wa kumtumikia Mungu. Nyumba hii aliijenga kwa gharama ya shilingi milioni mbili tu (Tsh 2,000,000/=) miaka hiyo, ambapo gharama ya ujenzi Tanzania, ilikuwa haijakuwa kubwa, kama ilivyo sasa. Wakati Kakobe anajenga nyumba hii, Kanisa analoliongoza sasa, la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), lilikuwa bado halijaanzishwa. Kanisa hili, lilianzishwa miaka mitatu baadaye, yaani tarehe 30.4.1989. Mpaka leo, miaka 25 tangu Kanisa hili lianzishwe, Kakobe hajawahi kuishi katika nyumba nyingine au kuwa na nyumba yake nyingine yoyote.

Askofu Kakobe, ana gari moja tu binafsi, "unaloweza kusema kuwa ni gari"; ambalo alipewa zawadi na waumini 84 (themanini na wanne), waliochangishana kwa hiari, wenyewe kwa wenyewe; bila yeye kujua, na wakanunua gari hilo na kulileta Kanisani Jumapili ya tarehe 27.6.2010, bila kumpa taarifa; na kwa kumshitukiza, wakajitokeza mwisho wa ibada, na "kumlazimisha" kupokea zawadi hiyo, kutoka kwao. "Walimlazimisha" kwa risala ndefu, kwa sababu, huko nyuma, aliwahi kupewa mara kadha, zawadi za magari, na baadhi ya waumini, na akayakataa magari yao.
Gari jingine, ni la mke wake Hellen, gari dogo "Toyota Sprinter", mtumba au "used", lenye umri wa miaka takriban 20, alilopewa na waumini watatu akina mama, kama zawadi, mwaka 2007. Vilevile, hakuna mtoto wake yeyote mwenye nyumba au gari.

Hii, ni kinyume kabisa na maneno mengi yanayosikika mitaani, kwa baadhi ya watu, wanaosema kwamba Kakobe anaishi maisha ya kifahari kupindukia, ana majumba mengi ya kifahari, na magari mengi sana ya binafsi, na mali nyingi alizojilimbikizia binafsi, kutokana na "biashara" ya "Kanisa lake".

Akizirejea mali zake hizi, zilizotajwa hapo juu; kwa miaka kadha sasa, Askofu Kakobe amekuwa akizungumzia juu ya mali zake binafsi, katika vyombo mbalimbali vya habari, na kusema kama ifuatavyo, nami ninamnukuu, "Mimi sina nyumba yoyote zaidi ya hii, MAHALI POPOTE DUNIANI, siyo kijijini kwangu, wala mji wowote duniani; na vivyo hivyo mke na watoto wangu wote, hakuna hata mmoja mwenye nyumba mahali popote duniani. Siyo hilo tu, mimi wala mke wangu, hatuna biashara yoyote, shamba, wala mifugo, popote duniani; vilevile, mimi, wala mke wangu, hatuna akaunti binafsi ya fedha, katika BENKI YOYOTE DUNIANI. Kama yuko mtu yeyote mwenye taarifa zozote zilizo tofauti na hizi, basi ajitokeze na kuweka ushahidi hadharani na kuniumbua". Kwa miaka kadha sasa, tangu aseme hivi; hakuna hata mtu mmoja, aliyejitokeza hadharani kutoa ushahidi wa mali zake nyingine, kwa picha, au vyovyote vinginevyo.

Kwa kuwa hapa JF, ni "WHERE WE DARE TO TALK OPENLY", au mahali tunapothubutu kuzungumza kwa uwazi, bila hofu; ili kukata mzizi wa fitina, ebu basi, mtu yeyote hapa, anayejua mali nyingine binafsi za Kakobe, na ufahari wa maisha yake binafsi, wa namna moja au nyingine, ajitokeze hapa, na kutujuza kwa ushahidi wa picha, au vinginevyo; na siyo kwa uzushi tu wa kuambiwa, ili tujue hasa, ukweli ni upi! NAWASILISHA.

nimesoma maelezo yako na nimejitahd kusoma michango ya watu humu nimegundua watu wanazusha tu hakuna mwenye ushahid pasi na shaka kuhusu kile wanachosema kuhusu Kakobe kwa upande mmoja. lakn pia wewe binafs hujaweza kutuwekea ushahd kuhusu hiyo nyumba coz wewe umetuonyesha picha tu na sio umiliki sasa hatujui ni kwel yake au tunadanganywa. suala lingine ni pale anaposema hamiliki nyumban popote dunian wakat sisi tunajua hayo majengo yote ya kanisa ni mali yake binafsi. kuna mdau juz hapa alianzisha mada hapa kuuliza kwanini makanisa ya kiroho hawawatangazii waumin wao sadaka wanazopata na matumiz yake. hapa mimi ndio nilipaona ni pa msingi sana kupajua.
 
Tupe Ushahidi Wa Nyumba ya Kakobe uliyonayo
Suala la Sadaka Mimi naomba turejee ifuatavyo:
1.Migogoro ipo mingi sana kwa sababu watu wengi ni watumwa wa pesa hata wewe umeanza kuhoji pesa na si mambo mengine.
2.Pesa inavunja ndoa Kila siku Mke anataka kujua pesa na kusahau Maisha
3.Kanisani kila mtu anataka kujua pesa lakini hataki kujua neno la Mungu
4.Kiukweli hakuna kanisa lisilo la Kiroho hakuna kabisa ila tofauti yake ni roho ipi? Maana kuna roho ya Shetani pia sasa wale wote wanaopinga neno la Mungu wanafahamika wapo na roho gani
5.Propagada nyingi za CCM dhidi ya CHADEMA huwa ni matumizi ya fedha utaona CCM wanaingilia matumizi ya CHADEMA hata pale ambapo pesa hizo ni za Kwao.
6.Wambea wengi wanafuatilia jirani anakula nini na wakati mwingine kumubuni mke wa mtu kwa kumushawishi kwa Chakula na pesa.
7.Sadaka za kanisa lingine zinakuhusu nini wewe usiyekuwa Kanisa hilo??
8.Tumeona Kanisa la Morovian ambapo Assah Mwambene Mkurungenzi Habari lina mgogoro mkubwa wa Sadaka lakini Serikali ya CCM na wewe hulioni hilo ila unahoji Sadaka za Kakobe ile iweje??
9.Mgogoro wa Sadaka umejitokeza Kanisa KKT linalo ongozwa na Mch Ambilikile Mwasapila Loliondo kwa mgao wa Kikombe. Mgogoro huo haukuisha hadi Askof Thomas Laizer anakufa.

Mimi ninachofahamu mfanyabiashara yoyote yule anapoamua kuunga mkono ukweli na kusema maovu ya watawala huwa ana anza kupelekewa watu wa TRA wakague kodi na kubabikiza Kodi lakini akiwa kama anaunga Watawala basi watamuuzia hada UDA kwa bei chee
Kwa upande wa Viongozi wa dini wanao kosoa utawala huwa serikali inapandikiza waumini feki na kuhoji Sadaka wakati waumini hao hao hawato maana wanahofu zinaibiwa. Hivyo wanahoji sadaka ambazo zinatolewa na watu wengine ndo maana na wewe unahoji sadaka zinazotolewa na watu wengine huku wewe ukiwa --------- bila kujua .

Wewe fuatilia hapa Askofu Gamanywa alisha sema Kikwete ni chaguo la Mungu, JK akabeba familia yake na kwenda huko sasa ulishaona thread ya kuhoji mambo ya Askf Gamanywa humu??
 
nimesoma maelezo yako na nimejitahd kusoma michango ya watu humu nimegundua watu wanazusha tu hakuna mwenye ushahid pasi na shaka kuhusu kile wanachosema kuhusu Kakobe kwa upande mmoja. lakn pia wewe binafs hujaweza kutuwekea ushahd kuhusu hiyo nyumba coz wewe umetuonyesha picha tu na sio umiliki sasa hatujui ni kwel yake au tunadanganywa. suala lingine ni pale anaposema hamiliki nyumban popote dunian wakat sisi tunajua hayo majengo yote ya kanisa ni mali yake binafsi. kuna mdau juz hapa alianzisha mada hapa kuuliza kwanini makanisa ya kiroho hawawatangazii waumin wao sadaka wanazopata na matumiz yake. hapa mimi ndio nilipaona ni pa msingi sana kupajua.

Uzi huu siyo wa leo, upo hapa kwa karibu miezi miwili. Usiwe mvivu, jitume kufanya utafiti kama sisi wengine tulivyokwisha kufanya utafiti, na kuthibitisha kwamba mmiliki wa nyumba hii ni Kakobe. Kuhusu kwamba majengo yote ya Kanisa la FGBF ni mali yake binafsi, huu ni ujinga au uvivu wa kufikiri, wa baadhi ya Watanzania. Kanisa hili lina miaka 25 tangu lianzishwe. Lina "Certificate of Incorporation" kwa zaidi ya miaka 20 sasa, kutoka kwa Mdhamini Mkuu wa Wadhamini, wa RITA, iliyoko Wizara ya Katiba na Sheria. Ili Kupata hati ya Kiwanja cha Kanisa, lazima kipatikane kibali, "letter of consent", kutoka kwa Mdhamini Mkuu wa Wadhamini, na majengo yote ya Kanisa huwa ni mali ya Bodi ya Wadhamini inayotambuliwa na Mdhamini Mkuu wa Wadhamini. Sasa majengo ya Kanisa kama hili lenye umri wa miaka 25, yanawezaje kuwa mali ya mtu binafsi? Fanya homework yako vizuri, hapa ni mahali pa ma-GT (Great Thinkers)!!!!!!
 
Vidonge ni lazima wapewe,wakitema au wakimeza ni shauri yao !!!

hata angekuwa na nyumba ya ghorofa poa tu..nani kasema watumishi wa Mungu ndio waishi kwenye mapagale ni wivu tu...
 
Mbona inaonekana kama haishi mtu............Hakuna harakati za binadamu hapo.......!!!!!!
 
hivi nchi watu mtakuwa maubongo pooza mpaka lini?
maubongo pooza ni watu ambao huwa hawakubali facts wanaenda na assumption tuu
Huyo aliyeleta post hiyo ni kwa sababu kulikuwa na uvumi kwamba Askofu Kakobe anakaa nyumba ya gharama Leo tumejua ukweli kwamba nyumba yake ni ya kawaida saaaaaaaana
salsa tunajulishwa fact miubongo pooza inaanza kuleta assumption zao na nafkiri hawa wamesoma st kayumba ambako hawakufundishwa umuhimu wa fact katika kufanya maamuzi

maubongo pooza hayatakiwi humu JF humu ni kwa macritical thinker...................!
 
attachment.php

attachment.php

Hii hapa, ndiyo nyumba pekee ya Askofu Mkuu Zachary Kakobe, kama wanavyothibitisha waumini wake, na watu wengi wanaofahamu undani wa maisha yake binafsi. Ni nyumba ya kawaida sana ya vyumba vinne, iliyojengwa katika mtaa wenye nyumba ambazo zimebanana sana, bila kuacha nafasi; eneo la Kijitonyama, Dar-Es-Salaam; umbali mfupi kutoka Kituo cha Polisi, Mabatini.

Kakobe, aliijenga nyumba hii, mwaka 1986, kutokana na kazi aliyokuwa akiifanya, na biashara zake binafsi alizokuwa akizifanya, nyakati hizo; kabla ya kuitika wito wa kumtumikia Mungu. Nyumba hii aliijenga kwa gharama ya shilingi milioni mbili tu (Tsh 2,000,000/=) miaka hiyo, ambapo gharama ya ujenzi Tanzania, ilikuwa haijakuwa kubwa, kama ilivyo sasa. Wakati Kakobe anajenga nyumba hii, Kanisa analoliongoza sasa, la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), lilikuwa bado halijaanzishwa. Kanisa hili, lilianzishwa miaka mitatu baadaye, yaani tarehe 30.4.1989. Mpaka leo, miaka 25 tangu Kanisa hili lianzishwe, Kakobe hajawahi kuishi katika nyumba nyingine au kuwa na nyumba yake nyingine yoyote.

Askofu Kakobe, ana gari moja tu binafsi, "unaloweza kusema kuwa ni gari"; ambalo alipewa zawadi na waumini 84 (themanini na wanne), waliochangishana kwa hiari, wenyewe kwa wenyewe; bila yeye kujua, na wakanunua gari hilo na kulileta Kanisani Jumapili ya tarehe 27.6.2010, bila kumpa taarifa; na kwa kumshitukiza, wakajitokeza mwisho wa ibada, na "kumlazimisha" kupokea zawadi hiyo, kutoka kwao. "Walimlazimisha" kwa risala ndefu, kwa sababu, huko nyuma, aliwahi kupewa mara kadha, zawadi za magari, na baadhi ya waumini, na akayakataa magari yao.
Gari jingine, ni la mke wake Hellen, gari dogo "Toyota Sprinter", mtumba au "used", lenye umri wa miaka takriban 20, alilopewa na waumini watatu akina mama, kama zawadi, mwaka 2007. Vilevile, hakuna mtoto wake yeyote mwenye nyumba au gari.

Hii, ni kinyume kabisa na maneno mengi yanayosikika mitaani, kwa baadhi ya watu, wanaosema kwamba Kakobe anaishi maisha ya kifahari kupindukia, ana majumba mengi ya kifahari, na magari mengi sana ya binafsi, na mali nyingi alizojilimbikizia binafsi, kutokana na "biashara" ya "Kanisa lake".

Akizirejea mali zake hizi, zilizotajwa hapo juu; kwa miaka kadha sasa, Askofu Kakobe amekuwa akizungumzia juu ya mali zake binafsi, katika vyombo mbalimbali vya habari, na kusema kama ifuatavyo, nami ninamnukuu, "Mimi sina nyumba yoyote zaidi ya hii, MAHALI POPOTE DUNIANI, siyo kijijini kwangu, wala mji wowote duniani; na vivyo hivyo mke na watoto wangu wote, hakuna hata mmoja mwenye nyumba mahali popote duniani. Siyo hilo tu, mimi wala mke wangu, hatuna biashara yoyote, shamba, wala mifugo, popote duniani; vilevile, mimi, wala mke wangu, hatuna akaunti binafsi ya fedha, katika BENKI YOYOTE DUNIANI. Kama yuko mtu yeyote mwenye taarifa zozote zilizo tofauti na hizi, basi ajitokeze na kuweka ushahidi hadharani na kuniumbua". Kwa miaka kadha sasa, tangu aseme hivi; hakuna hata mtu mmoja, aliyejitokeza hadharani kutoa ushahidi wa mali zake nyingine, kwa picha, au vyovyote vinginevyo.

Kwa kuwa hapa JF, ni "WHERE WE DARE TO TALK OPENLY", au mahali tunapothubutu kuzungumza kwa uwazi, bila hofu; ili kukata mzizi wa fitina, ebu basi, mtu yeyote hapa, anayejua mali nyingine binafsi za Kakobe, na ufahari wa maisha yake binafsi, wa namna moja au nyingine, ajitokeze hapa, na kutujuza kwa ushahidi wa picha, au vinginevyo; na siyo kwa uzushi tu wa kuambiwa, ili tujue hasa, ukweli ni upi! NAWASILISHA.
Kakobe kaacha siasa?
Na TANESCO je, ameacha kulumbana nao kwa sababu zisizoeleweka?
 
siku kakobe akiwa hayopo kanisani nani anaendesha misa?
maana nasikia huwa wanaweka CD's za mahubiri,ni kweli haya?
hizo story tu za mtaani za wapinga kristo nilimshangaa sana Gambo alipokuwa anamkashifu mtumishi wa Mungu kwa story za mtaani neda pale kanisani kashuhudie kama kuna kitu kama hicho.
 
Unajaribu kuaminisha hivyo watu wafunguke juu ya kakobe,upate kuandika report kuhusu huyu jamaa...."siku zote mtu aliye wahi kumiliki pesa siku ukimwambia hakuwai kuwa na chochote atagunguka dili zake zote kwa hasira"napita kwa kunyata nyata
 
attachment.php

attachment.php

Hii hapa, ndiyo nyumba pekee ya Askofu Mkuu Zachary Kakobe, kama wanavyothibitisha waumini wake, na watu wengi wanaofahamu undani wa maisha yake binafsi. Ni nyumba ya kawaida sana ya vyumba vinne, iliyojengwa katika mtaa wenye nyumba ambazo zimebanana sana, bila kuacha nafasi; eneo la Kijitonyama, Dar-Es-Salaam; umbali mfupi kutoka Kituo cha Polisi, Mabatini.

Kakobe, aliijenga nyumba hii, mwaka 1986, kutokana na kazi aliyokuwa akiifanya, na biashara zake binafsi alizokuwa akizifanya, nyakati hizo; kabla ya kuitika wito wa kumtumikia Mungu. Nyumba hii aliijenga kwa gharama ya shilingi milioni mbili tu (Tsh 2,000,000/=) miaka hiyo, ambapo gharama ya ujenzi Tanzania, ilikuwa haijakuwa kubwa, kama ilivyo sasa. Wakati Kakobe anajenga nyumba hii, Kanisa analoliongoza sasa, la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), lilikuwa bado halijaanzishwa. Kanisa hili, lilianzishwa miaka mitatu baadaye, yaani tarehe 30.4.1989. Mpaka leo, miaka 25 tangu Kanisa hili lianzishwe, Kakobe hajawahi kuishi katika nyumba nyingine au kuwa na nyumba yake nyingine yoyote.

Askofu Kakobe, ana gari moja tu binafsi, "unaloweza kusema kuwa ni gari"; ambalo alipewa zawadi na waumini 84 (themanini na wanne), waliochangishana kwa hiari, wenyewe kwa wenyewe; bila yeye kujua, na wakanunua gari hilo na kulileta Kanisani Jumapili ya tarehe 27.6.2010, bila kumpa taarifa; na kwa kumshitukiza, wakajitokeza mwisho wa ibada, na "kumlazimisha" kupokea zawadi hiyo, kutoka kwao. "Walimlazimisha" kwa risala ndefu, kwa sababu, huko nyuma, aliwahi kupewa mara kadha, zawadi za magari, na baadhi ya waumini, na akayakataa magari yao.
Gari jingine, ni la mke wake Hellen, gari dogo "Toyota Sprinter", mtumba au "used", lenye umri wa miaka takriban 20, alilopewa na waumini watatu akina mama, kama zawadi, mwaka 2007. Vilevile, hakuna mtoto wake yeyote mwenye nyumba au gari.

Hii, ni kinyume kabisa na maneno mengi yanayosikika mitaani, kwa baadhi ya watu, wanaosema kwamba Kakobe anaishi maisha ya kifahari kupindukia, ana majumba mengi ya kifahari, na magari mengi sana ya binafsi, na mali nyingi alizojilimbikizia binafsi, kutokana na "biashara" ya "Kanisa lake".

Akizirejea mali zake hizi, zilizotajwa hapo juu; kwa miaka kadha sasa, Askofu Kakobe amekuwa akizungumzia juu ya mali zake binafsi, katika vyombo mbalimbali vya habari, na kusema kama ifuatavyo, nami ninamnukuu, "Mimi sina nyumba yoyote zaidi ya hii, MAHALI POPOTE DUNIANI, siyo kijijini kwangu, wala mji wowote duniani; na vivyo hivyo mke na watoto wangu wote, hakuna hata mmoja mwenye nyumba mahali popote duniani. Siyo hilo tu, mimi wala mke wangu, hatuna biashara yoyote, shamba, wala mifugo, popote duniani; vilevile, mimi, wala mke wangu, hatuna akaunti binafsi ya fedha, katika BENKI YOYOTE DUNIANI. Kama yuko mtu yeyote mwenye taarifa zozote zilizo tofauti na hizi, basi ajitokeze na kuweka ushahidi hadharani na kuniumbua". Kwa miaka kadha sasa, tangu aseme hivi; hakuna hata mtu mmoja, aliyejitokeza hadharani kutoa ushahidi wa mali zake nyingine, kwa picha, au vyovyote vinginevyo.

Kwa kuwa hapa JF, ni "WHERE WE DARE TO TALK OPENLY", au mahali tunapothubutu kuzungumza kwa uwazi, bila hofu; ili kukata mzizi wa fitina, ebu basi, mtu yeyote hapa, anayejua mali nyingine binafsi za Kakobe, na ufahari wa maisha yake binafsi, wa namna moja au nyingine, ajitokeze hapa, na kutujuza kwa ushahidi wa picha, au vinginevyo; na siyo kwa uzushi tu wa kuambiwa, ili tujue hasa, ukweli ni upi! NAWASILISHA.

Bila shaka yoyote, nakubaliana na wewe...

Huyu mzee ni Mtumishi wa Mungu wa kweli!!

Na watumishi wa Mungu aliye hai wa kweli mtawatambua kwa matendo yao sawasawa na Biblia isemavyo!!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Huu ni upuuzi kujivunia kuwa masikini
Ndio maana namkubali mzee wa upako ali diss mtu kujisifia huu ujinga
Yani kakobe watoto wake hawana gari wala nyumba
Ni wazi watakua 30yrs
Na baba yao ndio anaishi hapo
 
Back
Top Bottom