Hii dhana ya Mwaafrika kuitwa Mtu mweusi na Wazungu kuitwa Watu Weupe

Mtuache

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
251
638
Habari za wakati huu wana Jamii Forums. Nimekuwa nikijiuliza sana hili swali, japo linaweza kuonekana kama halina mantiki kwa baadhi yenu ila ningependa kulileta kwenu. Hii dhana ya Mwaafrika kuitwa Mtu mweusi na Wazungu kuitwa Watu Weupe.

Sikatai na sipingi Waafrika wengi tumebarikiwa ngozi yenye rangi nyeusi. Shida yangu inaanzia hapa kwa wazungu kuitwa watu weupe. Ukiangalia vizuri rangi nyeupe ni tofauti kabisa na Rangi ya ngozi za wazungu. Kiukweli kabisa Wazungu si watu weupe kama wanavyoitwa. Wazungu waliamua kujiita hivyo kama mojawapo ya silaha iliyotumika kumdhoofisha Muafrika ajione yeye si kitu (inferior) alafu wao wazungu waonekana ndo kitu(superior) Huenda waliamua kujiita Watu weupe (Whites) kutokana na maana tofauti tofauti za rangi nyeupe. Nitaelezea kwa uchache maana ya rangi Nyeupe na Nyeusi ambazo Huenda ziliwafanya wazungu kujiita Watu Weupe na sisi Waafrika kutuita Watu weusi, kama ifutavyo:-

1. KIBIBLIA.
Kibiblia Rangi nyeupe humaanisha usafi, utakatifu, nuru. Palipo na weupe hakuna uchafu wowote unaoweza kusitirika. Sehemu nyingi za biblia zinamuonesha Mungu akijitambulisha yeye kama mwenye mavazi meupe, kichwa cheupe na nywele nyeupe (soma Danieli 7:9, Ufunuo 1:14). Ukikutana na Rangi nyeupe kwenye Biblia, sehem kubwa ya ujumbe wake ni utakatafu, Usafi wa Roho na uwepo wa Bwana.

Rangi Nyeusi ni rangi ya giza, upotevu, uchafu, siku zote giza ni jeusi. Gizani ndimo maovu yote hufanyika (soma Yuda 1:13). Katika biblia Rangi nyeusi huonesha nguvu na falme za giza.

2. Kisaikolojia
Rangi Nyeupe Ina maana uhuru wa nafasi na kuondoa vikwazo vyote vilivyopo. Rangi nyeupe katika saikolojia ni ishara ya usawa, mfano wa usafi, hatia, furaha na uaminifu.

Tofauti na Rangi Nyeusi, hii humaanisha kila kitu kilichounganishwa na rangi nyeusi ni hasi. Ikiwa michoro za watoto zinaongozwa na nyeusi, basi unahitaji kushauriana na mtaalamu wa haraka.

HITIMISHO: nahitimisha kwa kusema kuwa Wazungu walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kulemaza bongo za waafrika, kuwafanya waafirka waamini Mzungu ni bora kuliko yeye. Wazungu walitumia silaha ya kujiita wao Watu Weupe na Dunia nzima ikakubali kuwa Wazungu ni watu weupe ilihali Rangi Nyeupe inajulikana na ukweli ni kwamba wao si watu weupe. Waafrika wakaitwa watu weusi wakakubali na dunia nzima ikakubali. Huenda ni wazungu hao hao wakatoa maana tofauti tofauti za rangi nyeupe kama nilivyoelezea kwa uchache hapo juu na maana tofauti tofauti za rangi nyeusi kama nilivyoelezea hapo juu pia. Lengo ni kumfanya Muafrika awe dhaifu milele (weak forever) na wao kuwa wenye nguvu milele.
#JF@Mtuache
#NaipendaAfrika.

Nakaribisha maoni lengo tujifunze sote. Karibuni
 
Sasa utofauti hupo wapi kwani ngozi yetu ina rangi hipi na mzungu rangi hipi.
Binadamu wote sawa ila rangi ni tofauti
 
Walipotuletea dini zao, sanamu ya malaika ilikuwa nyeupe na ya shetani nyeusi, hata kubatiza walianza na maneno haya " kama wewe ni binadamu nakubatiza ." Tulidharauliwa na tukapokea dini zao bila hata kuhoji. Walitunga kitabu cha sala na kichwa cha habari " Sala za kuombea washenzi wa Afrika" baadae kitabu kilifutwa.
 
Hivi inaposemwa mtu mweupe na mtu mweusi Ni kwa namna hii labda?
CollageMaker_20210629_214658099.jpg
CollageMaker_20210629_215056134.jpg
 
babu zetu walichapwa ili wakubali kuitwa weusi! sisi hatupendi !!! halafu wanapenda sana kutufuata fuata!! mie nikiwa Rais ni kila mtu akae kwake!! akinigbagua na mie nambagua kisiasa mara saba zaidi ngoma drooo!

Tatizo miafrica inajipendekeza sana kujichekesha tuuuu! yeye aniite ivo na mie namuita zeruzeru kikwapa
 
Waweza kuta Waafrika ndo walianza kuwaita wazungu watu weupe ila tukirudi kwenye fact rangi ya ngozi ya Waafrika inaonyesha kabisa kuwa kuna kitu hakipo sawa kitu kinachothibitishwa kupitia fikra na matendo ya Waafrika.
 
babu zetu walichapwa ili wakubali kuitwa weusi! sisi hatupendi !!! halafu wanapenda sana kutufuata fuata!! mie nikiwa Rais ni kila mtu akae kwake!! akinigbagua na mie nambagua kisiasa mara saba zaidi ngoma drooo!

Tatizo miafrica inajipendekeza sana kujichekesha tuuuu! yeye aniite ivo na mie namuita zeruzeru kikwapa
Wakati Chifu Hangaya anafanya Royal Tour ili kuwavutia watutembelee.
 
Chunguza vizuri uone!! weupe hata kuzaa ni tatizo vitoto viwili vya mawazo! siyo watamu kiviile ni rangi tu unayoiona kwa mbali lkn ukiisogelea utakuwa unaota kila siku kufa kufa! nayo imeongezewa vikorombwezo viingi,

Africa hawa hawa! ''Ke' mweusi, au maji ya kunde ni watamu mnoo!! na wavumilivu kuliko weupe pee! kwa upande wa me sijui labda mdada km Eclat atusaidie!

mzungu akipigwa Jua yule utamkimbia! mbali na viji harufu vyao huwaga wanazimia! Jua tu linamtoa kimasomaso! wao bana hela tu, wanajitahidi sana tusichomoke hapa tulipo si unaona walivyo mfanya Gaddafi!!

yoote yale ni kwa ajili Libya ilikuwa inakuja juu si kawaida, Gadaffi alikomaa na nchi za Africa zinyanyuke kiuchumi!! weee!! alichokipata kila mtu humu anajua, yaani walitoa sababu sizizo na mashiko,

mpaka leo libya ina chakaa pasipo sababu! ajili ya chuki za weupe! anae jua sababu ya kuvamiwa Libya ki-vile na Majeshi ya NATO yakiongozwa na ufaransa aseme hapahapa!

Wangeweza kutuachia tukomae na umaskini wetu , simply waende wasitujue!! tufe kivyetu mbona tungechomoka hatare! na wanajua tulivo na mauwezo km wote! wana mikono mingi ya kutubania! humu barani Africa mkuu!

eti Egyptological studies za Misri, hakuna Mwafrica pale! wala kusoma soma pale

Na yale mabaki yana wahusu Waafrica weusi, ni ya mababu zetu, kwa nini weupe wana ng'ang'ania, ni ili tusijione eti tuta ringa! eti wazungu wanasema jamii ya Wamisri walikuwa ni ALLIENS!! ivo walipotea ghafla kurudi waliko toka!!!!

km ni ivo je na hizo Mummies wanazotoa kwenye mapyramids niza kina nani?
 
babu zetu walichapwa ili wakubali kuitwa weusi! sisi hatupendi !!! halafu wanapenda sana kutufuata fuata!! mie nikiwa Rais ni kila mtu akae kwake!! akinigbagua na mie nambagua kisiasa mara saba zaidi ngoma drooo!

Tatizo miafrica inajipendekeza sana kujichekesha tuuuu! yeye aniite ivo na mie namuita zeruzeru kikwapa
Heee ,
 
Habari za wakati huu wana Jamii Forums. Nimekuwa nikijiuliza sana hili swali, japo linaweza kuonekana kama halina mantiki kwa baadhi yenu ila ningependa kulileta kwenu. Hii dhana ya Mwaafrika kuitwa Mtu mweusi na Wazungu kuitwa Watu Weupe.

Sikatai na sipingi Waafrika wengi tumebarikiwa ngozi yenye rangi nyeusi. Shida yangu inaanzia hapa kwa wazungu kuitwa watu weupe. Ukiangalia vizuri rangi nyeupe ni tofauti kabisa na Rangi ya ngozi za wazungu. Kiukweli kabisa Wazungu si watu weupe kama wanavyoitwa. Wazungu waliamua kujiita hivyo kama mojawapo ya silaha iliyotumika kumdhoofisha Muafrika ajione yeye si kitu (inferior) alafu wao wazungu waonekana ndo kitu(superior) Huenda waliamua kujiita Watu weupe (Whites) kutokana na maana tofauti tofauti za rangi nyeupe. Nitaelezea kwa uchache maana ya rangi Nyeupe na Nyeusi ambazo Huenda ziliwafanya wazungu kujiita Watu Weupe na sisi Waafrika kutuita Watu weusi, kama ifutavyo:-

1. KIBIBLIA.
Kibiblia Rangi nyeupe humaanisha usafi, utakatifu, nuru. Palipo na weupe hakuna uchafu wowote unaoweza kusitirika. Sehemu nyingi za biblia zinamuonesha Mungu akijitambulisha yeye kama mwenye mavazi meupe, kichwa cheupe na nywele nyeupe (soma Danieli 7:9, Ufunuo 1:14). Ukikutana na Rangi nyeupe kwenye Biblia, sehem kubwa ya ujumbe wake ni utakatafu, Usafi wa Roho na uwepo wa Bwana.

Rangi Nyeusi ni rangi ya giza, upotevu, uchafu, siku zote giza ni jeusi. Gizani ndimo maovu yote hufanyika (soma Yuda 1:13). Katika biblia Rangi nyeusi huonesha nguvu na falme za giza.

2. Kisaikolojia
Rangi Nyeupe Ina maana uhuru wa nafasi na kuondoa vikwazo vyote vilivyopo. Rangi nyeupe katika saikolojia ni ishara ya usawa, mfano wa usafi, hatia, furaha na uaminifu.

Tofauti na Rangi Nyeusi, hii humaanisha kila kitu kilichounganishwa na rangi nyeusi ni hasi. Ikiwa michoro za watoto zinaongozwa na nyeusi, basi unahitaji kushauriana na mtaalamu wa haraka.

HITIMISHO: nahitimisha kwa kusema kuwa Wazungu walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kulemaza bongo za waafrika, kuwafanya waafirka waamini Mzungu ni bora kuliko yeye. Wazungu walitumia silaha ya kujiita wao Watu Weupe na Dunia nzima ikakubali kuwa Wazungu ni watu weupe ilihali Rangi Nyeupe inajulikana na ukweli ni kwamba wao si watu weupe. Waafrika wakaitwa watu weusi wakakubali na dunia nzima ikakubali. Huenda ni wazungu hao hao wakatoa maana tofauti tofauti za rangi nyeupe kama nilivyoelezea kwa uchache hapo juu na maana tofauti tofauti za rangi nyeusi kama nilivyoelezea hapo juu pia. Lengo ni kumfanya Muafrika awe dhaifu milele (weak forever) na wao kuwa wenye nguvu milele.
#JF@Mtuache
#NaipendaAfrika.

Nakaribisha maoni lengo tujifunze sote. Karibuni

Hayo maandiko ya Biblia uliyonukuu yanayotukuza rangi nyeupe na kudhalilisha rangi nyeusi pia yaliandikwa na hao hao wazungu wala sio maneno ya Mungu--- waliyaandika ili kuwadhalisha watu weusi na kujikweza wao.
 
Back
Top Bottom