Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,509
- 16,734
Kuna hali sijui kama wenzangu wameshaiona. Hali hii inatokana na mabadiliko ya kihistoria na yawezekana na sababu nyengine ambazo ni nje ya uwezo na matakwa yetu.
Katika miji mingi ya nchi yetu kwa sasa huwezi kusema kuwa Tanzania ni nchi ya waafrika weusi. Ukitaka watu wa rangi hiyo inabidi usafiri mpaka Sudan ya kusini ndiko utawaona wanavyopendeza na vimo vyao.
Kwa mtazamo wangu rangi za Watanzania zimeondoka kutoka weusi kuwa wekundu na hata weupe kabisa. Mwanzoni kuna waliosema wasichana wetu wengi wanajichubua ili wawe na rangi kama za wazungu.
Nimejaribu kupeleleza shutuma hizo na nikagundua uhakika wake hauzidi asilimia 20.Ukweli ni kuwa wengi wao ni rangi zao za kuzaliwa.
Kuna siku nilikutana na dada fulani kabeba mtoto mweupe kabisa kama mzungu au mwarabu nikatamani au wa kwangu. Mimi nikadhani labda ni yaya kwenye nyumba fulani, kumbe bwana ni mtoto wake wa kumzaa kabisa wakati mwenyewe wala hana rangi kama ya mtoto huyo na wala mtoto hana dalili za ulemavu wa ngozi.
Hali hiyo ya kubadilika rangi kutoka weusi kuja wekundu na maji ya kunde kumetufanya sasa wala hatuonekani kushangaana sana mitaani kwetu kama kwamba tumeingiliwa na wageni kama ilivyokuwa wakati wa mababu zetu.
Muhimu nimeona hiyo hali lakini asili na chanzo chake nimeshindwa kupata jibu.
Baada ya hapo nikajiuliza hizi rangi za bendera zetu bado zitabaki na maana zake hizo hizo au zitabadilishwa au zitaongezewa ufito mwengine kuwakilisha makundi ya watu wengine kama hao wekundu au itakuwaje.
Kwenye wikipedia historia ya bendera ya Tanzania imetajwa kama hivi.

Historia ya bendera
Bendera hii imepatikana tangu 30 Juni 1964 kutokana na muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Bendera ya Tanganyika ilikuwa na rangi ya kijani ikiwa na kanda nyeusi katikati yenye milia za njano kando. Buluu imepatikana kutokana na bendera ya Zanzibar ya mwaka 1964 ikimaanisha bahari. Hata hivyo toka mwaka 2005, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilianza kutumia rasmi bendera ya Zanzibar. Hii ni mara ya kwanza toka kuungana kwa Tanganyika na Zanzibar kwa funguvisiwa la Zanzibar kuwa na bendera yake lenyewe.Maana ya rangi
Rangi zinasemekana kuwa na maana zifuatazo:- Kijani kwa ajili ya mashamba, kilimo na misitu. Kijani ni pia rangi ya bendera ya chama cha TANU kilichokuwa chama tawala tangu uhuru.
- Buluu kwa ajili ya bahari na visiwa.
- Nyeusi ni rangi ya Waafrika.
- Njano inakumbusha juu ya utajiri wa madini. Njano ya namna hiyo inaelezwa mara nyingine kuwa ni dhahabu [3], lakini maelezo rasmi mengine kwa Kiingereza yanataja rangi kuwa "Yellow Pantone