Mtuache
JF-Expert Member
- Mar 12, 2021
- 251
- 638
Habari za wakati huu wana Jamii Forums. Nimekuwa nikijiuliza sana hili swali, japo linaweza kuonekana kama halina mantiki kwa baadhi yenu ila ningependa kulileta kwenu. Hii dhana ya Mwaafrika kuitwa Mtu mweusi na Wazungu kuitwa Watu Weupe.
Sikatai na sipingi Waafrika wengi tumebarikiwa ngozi yenye rangi nyeusi. Shida yangu inaanzia hapa kwa wazungu kuitwa watu weupe. Ukiangalia vizuri rangi nyeupe ni tofauti kabisa na Rangi ya ngozi za wazungu. Kiukweli kabisa Wazungu si watu weupe kama wanavyoitwa. Wazungu waliamua kujiita hivyo kama mojawapo ya silaha iliyotumika kumdhoofisha Muafrika ajione yeye si kitu (inferior) alafu wao wazungu waonekana ndo kitu(superior) Huenda waliamua kujiita Watu weupe (Whites) kutokana na maana tofauti tofauti za rangi nyeupe. Nitaelezea kwa uchache maana ya rangi Nyeupe na Nyeusi ambazo Huenda ziliwafanya wazungu kujiita Watu Weupe na sisi Waafrika kutuita Watu weusi, kama ifutavyo:-
1. KIBIBLIA.
Kibiblia Rangi nyeupe humaanisha usafi, utakatifu, nuru. Palipo na weupe hakuna uchafu wowote unaoweza kusitirika. Sehemu nyingi za biblia zinamuonesha Mungu akijitambulisha yeye kama mwenye mavazi meupe, kichwa cheupe na nywele nyeupe (soma Danieli 7:9, Ufunuo 1:14). Ukikutana na Rangi nyeupe kwenye Biblia, sehem kubwa ya ujumbe wake ni utakatafu, Usafi wa Roho na uwepo wa Bwana.
Rangi Nyeusi ni rangi ya giza, upotevu, uchafu, siku zote giza ni jeusi. Gizani ndimo maovu yote hufanyika (soma Yuda 1:13). Katika biblia Rangi nyeusi huonesha nguvu na falme za giza.
2. Kisaikolojia
Rangi Nyeupe Ina maana uhuru wa nafasi na kuondoa vikwazo vyote vilivyopo. Rangi nyeupe katika saikolojia ni ishara ya usawa, mfano wa usafi, hatia, furaha na uaminifu.
Tofauti na Rangi Nyeusi, hii humaanisha kila kitu kilichounganishwa na rangi nyeusi ni hasi. Ikiwa michoro za watoto zinaongozwa na nyeusi, basi unahitaji kushauriana na mtaalamu wa haraka.
HITIMISHO: nahitimisha kwa kusema kuwa Wazungu walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kulemaza bongo za waafrika, kuwafanya waafirka waamini Mzungu ni bora kuliko yeye. Wazungu walitumia silaha ya kujiita wao Watu Weupe na Dunia nzima ikakubali kuwa Wazungu ni watu weupe ilihali Rangi Nyeupe inajulikana na ukweli ni kwamba wao si watu weupe. Waafrika wakaitwa watu weusi wakakubali na dunia nzima ikakubali. Huenda ni wazungu hao hao wakatoa maana tofauti tofauti za rangi nyeupe kama nilivyoelezea kwa uchache hapo juu na maana tofauti tofauti za rangi nyeusi kama nilivyoelezea hapo juu pia. Lengo ni kumfanya Muafrika awe dhaifu milele (weak forever) na wao kuwa wenye nguvu milele.
#JF@Mtuache
#NaipendaAfrika.
Nakaribisha maoni lengo tujifunze sote. Karibuni