Hii baiskeli ilitengenezwa na Kampuni gani?

thatHUMBLEguy

JF-Expert Member
Nov 25, 2023
223
522
Heri ya Chrismas wakuu.

Visiting home for Christmas kula pilau kwa bimkubwa, nimekuta hii baiskeli kuna bwana mdogo—Uncle wangu yuko form one day school—ameifufua na anaitumia usafiri wa kwenda shule.

Kabla ya ujio wa pikipiki hizi za kichina, Pre–2009, Baiskeli hizi zilikuwa zinatumiwa sana na walimu na watumishi wa umma—hasa halmashauri—kwani zilikuwa zina muonekano mzuri, high comfortability unapokaa na kuziendesha huku kikiwa na carrier ndogo ndogo, light one, yakufaa kubebea mizigo midogo midogo na miepesi kama vitabu, files, briefcase au kilo ya nyama au hata mtoto mdogo—Tofauti na zile Phoenix au Swala ama Avon, uliweza beba hata mtu kwenye 'mgamba', ukawa na abiria watatu, pengine unaweza fanaisha na SPORT CARS😄. Ilikuwa ni usafiri wenye heshima yake.

Kuna Shangazi yangu mmoja mwalimu wa shule ya Msingi enzi hizo, alipata mwanaume na kuanza mahusiano naye. Lakini, hakuwa anamjua vyema yule jamaa, alichojua yeye ni kuwa anafanya kazi kampuni ya Tumbaku na anampenda. Mzee wangu, aliyekuwa mtumishi wa umma eneo lile, alimpinga sana mahusiano yao kwani hakua akimuamini yule jamaa. Miezi nane baadae, yule jamaa alipotea, na gunia kama 25 za mahindi na shilingi Laki 5. That was early 2000s. Alichomuachia ni hii baiskeli 😄. Shangazi aliathiriwa sana na lile tukio, akahama wilaya, hii baiskeli ikaja nyumbani, na ikawa ndio 'Crown' yetu tukienda likizo nyumbani. Kupigia misele mtaani na kwenda kutongozea madem.

Nimekuta dogo kaifufua, nimekumbuka maisha ya uvulana.

Kwa wajuzi, naombeni mnikumbushe, hii baiskeli ilitengenezwa na Kampuni gani!

IMG_20231225_113746_585.jpg
 
View attachment 2852434
Inaonekana ina vibali vyote haidaiwi.
 
Back
Top Bottom