Lawama ziende kwa dreva wa bus pekee hao wengine hawana kosa, kama kweli wengi tupo barabara nadhi ni washuhuda wa fujo za huko, unafanya wema kuokoa asipate madhara matokeo yake wewe chombo ulichonacho unakigeuza miguu juu na huyo ulikuwa unamuokoa hana mda wa kusimama kujua unaendelaje, unabakia wewe kujikanyaga na safari yako kuishia hapo.
Na huu upuzi wa kukimbia kutegemea mwenzio atakupisha atakupishia wapi barabara zetu nyembamba hizi na unajuaje hilo gari linalokuja mbele litaitikia haraka kujibu hizo prukushani.
Gari nyingi tunaziona zimeanguka huko barabara sababu kuu ikiwa ni hiyo ya kuonyesha wema kwa wapuuzi kama hao, mi mwenyewe nikiona hatutasababisha kupoteza uhai wa watu nakubana ili iwe fundisho na siku nyingine.