Hichi kifo mama anahusika...

Hichi kifo mama anahusika...

Sandeni

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2013
Posts
666
Reaction score
298
Wakuu kuna rafiki yangu mmoja ambaye ni mwajiriwa wa serikali kwenye kitengo
cha usalama ni rafiki yangu sana.
Alikuwa na girl friend wake na kiukweli walipendana sana.

Ila mbaya kabisa mama wa mshikaji wangu hakumpenda kabisa binti
kwa kisingizio kuwa kamzidi kijana wake kwa umri, kitu ambacho
sisi tulikiona kama ni cha kawaida sana,
na hata tofauti ilikuwa haionekani kabisa, mdada alikuwa mchapa kazi kweli kweli
alikubalika kwa baba na kwa watu wengine isipokuwa kwa mama tu.

Hii ilimfanya mama akose support kabisa so upinzani wake ulishindwa coz ilifika sehemu akashindwa
kabisa kuzuia.

watu tukaanza maandalizi ya harusi, kamati zikaundwa na hata kwa upande wa binti
wakafanya maandalizi ya send off.
Aisee haikupita siku nyingi i remember ni wiki ya pili toka kamati ziundwe,

Binti akashikwa na ugonjwa wa kichwa from no where yaani..
Tukadhani labda ni uchovu wa kawaida, kichwa kikazidi kuuma,
akapelekwa hospital mambo yakazidi kuwa mabaya akaamishiwa KCMC still hali
ikawa mbaya hadi yule dada akafa.

Sasa mshikaji anashindwa kusahau kabisa na anaamini
kuwa mama yake ndiyo alichangia kufa kwa huyo dada(mchumba wake).
Hili lilimpa mawazo na kumwaminisha zaidi baada ya kukuta baadhi ya zawadi ambazo yule dada
aliwahi kumpelekea mama wa mshikaji zikiwa hazijatumika hata kidogo,
kuna baaadhi ya vitenge ambavyo mama alipewa na hakuvivaa.

Hivi inawezekana mama wa mshikaji akausika na hiki kifo?
Jamaa hataki kabisa hata kuwa karibu na mama yake, baada ya msiba ule
Hadi sasa jamaa anaamini kuwa mama yake ndiye mhusika.
Hebu tumshauri kijana arudishe Upendo wake kwa mama yake..
As kila anachofanya sasa hakuna mafanikio..
 
Yani hapo mungu ndie anaejua ukweli wa mambo, sisi wengine tutabaki kuhisi tu.
 
Jaman namuonea huruma huyo kaka. wazazi wananguvu ktk kukubaliana au kutokubaliana na mahusiano tulonayo ikitokea migogoro utataman uwe wewe pekeako ufanye kitu bila ya kuulizwa
 
Huwezi kusema zaid juu ya kifo hicho kwani ni ukweli hakuna mwenye uhakika na tuhuma tajwa lakin pia huwezi acha sema au kufikir hivyo kutokana na mahusiano mabovu kati ya Mama na binti,
 
mpenzi/mchumba ama mke mtarajiwa kisha tangulia mbele za haki,inabidi akubaliane na hili halafu baada ya hapo,mama mzazi ni mama tu na asijaribu kushindana nae,licha ya mapungufu yake kama anayo,akumbuke ndie aliemlea tokea akiwa tumboni na ana mchango mkubwa sana,asimdharau hata kidogo,wakati tupatapo wenzi hua tunajipendekeza nao sana kwa wazazi na kuwaambia kila kitu,yalopita yamepita agange yajayo kwa uzoefu alopata,naamin atampata mwingne!.
 
Kama ni coincidence basi imekuja vibaya mno! With time jamaa atasahau na atarudisha upendo kwa mama yake japo haitakuwa kama zamani
 
ukweli ni kwamba familia nyingi sikuiz zimekubwa sana na balaa hilo mpk kuikia hatua ya kuhisiana uchawi...
Familia zinasambaratika, amani na upendo unapotea, Tukumbuke jaman,shetani huwa anatumia nafasi ndogo sana kuharibu amani.Inyo unahitaji busara sana katika kufafanua jambo ili kufanya maamuzi sahihi la sivyo unaweza ukajiharibia maisha yako yote kwa uzembe wa sehemu moja.
That kaka should go to her mother and ask for forgvnec
naamini kinachomfanya azidi kujengeka mawazo hayo ni watu wa pemben na ndugu pia wanaoamini hilo,Sononeko la mama yake litamfungia Hazina dunian na mbinguni..hatofanikiwa kwa chochote.
Mama ni mama hakuna atakaechukua nafasi hiyo,na kifo ni kifo Mungu mwenyewe anajua sababu ni nini na sio mwanadamu...Kama kifo ni cha gafla,wangapi tumeshuhudia wanakufa gafla,umecheka nae jana unaamka siku ya pili unasikia kafariki...
Sometimes unaweza ukamchukia mtu lakini usiweze kumuwazia kifo, tho people tunatofautiana.
Kwakifo cha huyo dada ni Sheteni tu kaingilia kati kuvuruga watu.,,Tena hapo akisema aende kwa waganga wa kienyeji atavurugwa kabisa......Ni bora atulize akili na asali kwa Mungu wake anaemwamin ili amwonyeshe ukweli uko wapi na sio kuturn against his mom...


Imenigusa sana
 
Kumshauri mtu arudishe upendo wake kwa mtu mwingine ni pagumu sana, inabidi mhusika mwenyewe kuridhia na kurudisha moyo wake wa kumpenda tena mama.
 
Ina maana huyo kijana anaamini mama yake ni mchawi? Anafikiria hivyo kwa vigezo gani labda? Halafu na yeye ni mburula, samahani! Hivi unapopeleka mchumba mahali, unatambulisha na umri kwani wanataka kumsomesha? Hilo suala la umri lilifikaje kwa wazazi na nyie marafiki?

muambie ajifunze kujisimamia mwenyewe. Sio kila details za mwenza ni za kujadili na watu. Pili amjue Mungu anaemuamini. Watu wangapi wanakufa kwa kuumwa kichwa ama homa? Kama mama yake ndio amemuua huyu dada, basi asihangaike kuoa tena manake mama akikorofishwa tena basi ajue na yeye atakufa.
 
Yaani nakuelewa kabisaa Vaislay. Familia zinatengana kabisa kwa sababu ya hofu ya uchawi. Na ni aibu chuki zingine zinapandikizwa na hawa manabii wa kisasa. Mama mchawi asikuloge ukiwa mtoto akuloge saa hizi? Ukikosa maarifa lazma uangamie.
ukweli ni kwamba familia nyingi sikuiz zimekubwa sana na balaa hilo mpk kuikia hatua ya kuhisiana uchawi...
Familia zinasambaratika, amani na upendo unapotea, Tukumbuke jaman,shetani huwa anatumia nafasi ndogo sana kuharibu amani.Inyo unahitaji busara sana katika kufafanua jambo ili kufanya maamuzi sahihi la sivyo unaweza ukajiharibia maisha yako yote kwa uzembe wa sehemu moja.
That kaka should go to her mother and ask for forgvnec
naamini kinachomfanya azidi kujengeka mawazo hayo ni watu wa pemben na ndugu pia wanaoamini hilo,Sononeko la mama yake litamfungia Hazina dunian na mbinguni..hatofanikiwa kwa chochote.
Mama ni mama hakuna atakaechukua nafasi hiyo,na kifo ni kifo Mungu mwenyewe anajua sababu ni nini na sio mwanadamu...Kama kifo ni cha gafla,wangapi tumeshuhudia wanakufa gafla,umecheka nae jana unaamka siku ya pili unasikia kafariki...
Sometimes unaweza ukamchukia mtu lakini usiweze kumuwazia kifo, tho people tunatofautiana.
Kwakifo cha huyo dada ni Sheteni tu kaingilia kati kuvuruga watu.,,Tena hapo akisema aende kwa waganga wa kienyeji atavurugwa kabisa......Ni bora atulize akili na asali kwa Mungu wake anaemwamin ili amwonyeshe ukweli uko wapi na sio kuturn against his mom...


Imenigusa sana
 
Last edited by a moderator:
Mi najiuliza tu kwamba mawazo yatakayokuwa yanatolewa hapa utampelekea kila moja ama !!!!

Pili umetaja kazi yake ili iweje!!! Huoni kama utakuwa umeshamharibia kazi yake kwa kumuanika maana kwa maboss wake sasa ni 1+1 na kwa wengine kadhalika!!
 
yehuu..pole kwa wote yliyowakuta..ila anamhisi mamake maama ndiye aliekua.adui yake mkubwa na kibinadamu hwa hivyo..ila si vizuri akamtenga mama yake kwani hana uhakika bali anahisi tuuu..aachane tu mawazo hayo kwani siri anaijua Mungu pekee..na atampatia.tu mwingine na akimtegemea Mungu Ukweli ataujua
 
Ina maana huyo kijana anaamini mama yake ni mchawi? Anafikiria hivyo kwa vigezo gani labda? Halafu na yeye ni mburula, samahani! Hivi unapopeleka mchumba mahali, unatambulisha na umri kwani wanataka kumsomesha? Hilo suala la umri lilifikaje kwa wazazi na nyie marafiki?

muambie ajifunze kujisimamia mwenyewe. Sio kila details za mwenza ni za kujadili na watu. Pili amjue Mungu anaemuamini. Watu wangapi wanakufa kwa kuumwa kichwa ama homa? Kama mama yake ndio amemuua huyu dada, basi asihangaike kuoa tena manake mama akikorofishwa tena basi ajue na yeye atakufa.

mkuu, kuna baadhi ya mambo sijayaandika hapo, ni hivi huyo dada alikuwa anajuana na mke wa kaka yake na mshikaji.
na walikuwa wanaishi jirani, so shemeji yake na jamaa ndiyo aliyasema haya
coz alimjua huyu dada hata kabla hawajawa na mahusiano na jamaa.
 
Mi najiuliza tu kwamba mawazo yatakayokuwa yanatolewa hapa utampelekea kila moja ama !!!!

Pili umetaja kazi yake ili iweje!!! Huoni kama utakuwa umeshamharibia kazi yake kwa kumuanika maana kwa maboss wake sasa ni 1+1 na kwa wengine kadhalika!!

nitakuwa nimemwaribia nini mkuu? nini cha ajabu nilichoandika hapa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom