Hichi kifo mama anahusika...

Hichi kifo mama anahusika...

nitakuwa nimemwaribia nini mkuu? nini cha ajabu nilichoandika hapa

Tuseme mi ndo rafiki yako, kazi yangu ambayo ni ya siri ambayo hata wewe hukupaswa kuijua kwanini umeitaja kwenye mitandaooo????
 
Kutotumia zawadi hizo ndio sababu ya kufikiria hayo?
Rest in peace mdada....
 
Kijana amrudie Mungu wake, yote haya ni mapito na yeye kama kijana wa kiume yampasa kuvumilia!
 
Mmh jamani twende mbele turudi nyuma, hata kama ingemtokea yoyote kati yetu hapa, kapeleka mchumba nyumbani then mama anagoma kabisa kumkubali harusi inaandaliwa mara mchumba anafariki lazima tungepitia situation kama ya huyu kaka, unajua ni rahisi sana kulipambanua jambo linapokuwa kwa mwenzio lakini likiwa kwako ndo utaelewa uzito ulivyo, am not not saying huyo mama kweli kamuua huyo binti hyo ni siri ya Mungu pekee ili tu ningemshauri huyo kaka kwasasa amlilie sana Mungu aweze kumfungua na kumpa wepesi wa kusahau, kusamehe na kuendelea na maisha yake manake kwa akili yake hataweza ataishia kujijazia uchungu na visasi ambavyo mwisho wa siku vinaweza kuishia kumharibia zaidi.
 
Ina maana huyo kijana anaamini mama yake ni mchawi? Anafikiria hivyo kwa vigezo gani labda? Halafu na yeye ni mburula, samahani! Hivi unapopeleka mchumba mahali, unatambulisha na umri kwani wanataka kumsomesha? Hilo suala la umri lilifikaje kwa wazazi na nyie marafiki?

muambie ajifunze kujisimamia mwenyewe. Sio kila details za mwenza ni za kujadili na watu. Pili amjue Mungu anaemuamini. Watu wangapi wanakufa kwa kuumwa kichwa ama homa? Kama mama yake ndio amemuua huyu dada, basi asihangaike kuoa tena manake mama akikorofishwa tena basi ajue na yeye atakufa.

Mwenzangu...kuna wengine wala hawahitaji kutamka, toka mbali anaonekana....Kuna mdogo wetu mmoja mchumba wake nae..mmh, tunabaki kujisemea rohoni kuwa kama yeye ndio aliyemdondokea yote heri coz ni ya kwao...

Kwa huyu kijana, nafikiri ameenda to the extreme kumshika mama yake uchawi (japo tunasikia yapo)...Kwenye masiha kuna challenges kila kona, na kama hazikuuwi basi zinazidi kukukomaza...Cha msingi ni yeye kusonga mbele...Na hivyo vitenge kutokuvaliwa wala lisimtie simanzi, angejua akina mama tunavyojua kulundika ndani bila kuvaa....
 
Kuna mambo magumu, lakini ninachojiuliza katika maisha yake huyo jamaa ashawahi kuona au kuhisi mama yake kuwa na uwezi wa kufanya jambo hilo?
Maana hizi ni tuhuma kubwa sana mbaya zaidi kwa mama mzazi.
 
Wewe mzazi unaingiliaje mchumba wa mtoto wako bila sababu ya msingi? Kuna sababu kame vile mwizi, mwasherati au tabia tu ambazo kijamii hazikubaliki. Sasa watoto wameshapendana wewe unaanza kuhoji!!! Sasa basi katika hali ya kawaida kila mtu atakuwa na hisia mbaya kwa huyu mama hata kama kifo kile kilikuwa ni kutoka kwa muumba mwenyewe. Pili huyu mtoto wake wa kiume hatakaa ampende wala kumwamini mama yake kabisa. Wapo wazazi wa aina hii!!! Na mengine tumeshuhudia kabisa kwa watu wa karibu. Hivi mnakumbuka yule kijana wa CRDB mchumba alifariki sikua ya kumakia kufunga ndoa? Inasemekana mama hakutaka kijana wake aoe maana alihisi hatapata tena hela toka kwa mtoto!!! Hivi watoto ni ATM mashine jamani? Hata baada ya mchumba yule kufariki na ikamuumiza sana kijana, I remember ile nguo ya harusi alizikwa nayo!!! Mama bado anamfuata mke wa jamaa (alioa tena baadaye tena kwa mbinde) na ndoa yao ni matatizo makubwa!!! Wazazi mtahukumiwa sana, jehanamu yenu itakuwa ya tofauti. Kisa pesa na mali za watoto!!
 
yaliyopita si ndwele agange yajayo na mama ni mama tu hata kama kweli yeye ni mhusika,ni bora akajitahidi kupotezea tu coz inaweza kumtia uchungu zaidi,boraa aanze upya atafute mwingine maisha yaendelee
 
yaliyopita si ndwele agange yajayo na mama ni mama tu hata kama kweli yeye ni mhusika,ni bora akajitahidi kupotezea tu coz inaweza kumtia uchungu zaidi,boraa aanze upya atafute mwingine maisha yaendelee

ile team yenu inaitwaji?
 
RIP Bibi harusi mtarajiwa
Mungu akurehemu uko ulipo
dah inauma lakini.
ila yote yanawezekana ikawa coincidence ya kifo na uingiliaji wa bimkubwa au ikawa anahusika moja kwa moja ila cha msingi ni kumuachia mungu tu.yeye ndo mkamilifu na anajua kila kitu
akimind sana anaweza akaanza kumfanyia investigation bibi wake mkubwa kujua kama anahusika ama vipi.?
 
Hata mim naweza kumuhis mama lol ukikutana na wa mamamkwe wa hiv inabidi uwe mjanja kumzidiu yeyee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom