HESLB mnataka tufe kwa pressure?

las Casas

JF-Expert Member
Nov 22, 2015
474
1,000
Mimi ni mnufaika wa Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu (HESLB). Nilianza kulipa deni langu la shilingi milioni 6.5 mwaka wangu wa pili tu baada ya kuajiliwa.

Nililipa deni langu katika kipindi cha miaka nane. Nimeshtushwa na barua niliyoandikiwa ofisini kwamba nina deni HESLB.

Nimemaliza deni langu na huu ni mwaka wa pili sasa. Naomba kujua Bodi ya mikopo hili deni wamelitoa wapi wakati katika salary slip zangu zinaonyesha ushahidi wa kukatwa pesa kuanzia mara ya kwanza mpaka nalimaliza miaka miwili imepita sasa.

Hivi kwa mshahara kweli ( take home) nitaweza kuendesha Maisha au ndio utakuwa mwanzo wa depression na hata kupoteza Maisha? SERIKALI NAOMBA MULIANGALIE HILI NAJUA SIO KWANGU HATA KWA WENGINE WAMEKUTANA NALO. SISI NI WANYONGE .

PhotoGrid_Plus_1619627139128.jpg
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
7,713
2,000
Hao bodi mwisho wa siku watapata hasara sana, idadi ya wahitimu kila mwaka wengi wanaishia kukosa ajira na hayo madeni after two years yanaongezeka riba, sioni kama serikali itapata kitu hapo, hii mikopo ya wanafunzi ni sawa na serikali imecheza kamari, wanaoweza kumudu kulipia yote ni wachache sana, na inaonekana huko bodi ya mikopo hawana record za haya mambo yao vurugu tupu.
 

a45

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
1,292
2,000
Usichojua kuhusu hao loan board wao wanaile 6% rentation fee kila mwaka inaongeza kutoka kwenye Deni liliobaki kwa kila mwaka.

hivyo Kama ulimaliza Deni kuanzia siku uliyomaliza Deni ulitakiwa kuwafata hao loan board wakupe statement kuonyesha Hali ya mkopo wako kwakua lazima bado utakua tu na Deni kwani hiyo rentation fee itakuepo tu.

Kwani ilipoanza kuonekana kwenye salary slip yako lilikua Deni lililokuwako wakati ule unaanza- kulipa maana yake rentation fee iliendeleza kujizalisha kila mwaka.

Anyway tukiwaambia hili Deni halilipiki muwe munaelewa
 

Jagarld

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
2,199
2,000
Hii Tanzania hii,

Kila nikiangalia pale bungeni huwa naona mataka taka tu.

Kuna majitu pale yanajua kuvaa tai lakini hayajui hata Yapo kwa ajili gani na ya Nani, Sheria nyingi za hovyo hovyo huwa zinapitishwa kwa Kama hii. Kama Kuna mzigo unalifukarisha taifa Hili ni Hilo zimwi la kuitwa bunge.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom