i411
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 906
- 297

Nimeona hii kwa blog ya jamii na wabongo wengi wakawa wanamponda dogo eti yeye hana nidhamu kwavile anaamukia wakubwa na mkono mmoja mfukoni. Nyie waungwana mwaonaje hili dogo kafanya kosa au kuendana na kazi yake yupo sawa kuwa relax.
Mimi naona kwavile dogo anakipaji sio kosa lake manake yeye anafanya tuu mazoezi na kuongeza kipaji chake alichopewa na muumba. Wakina siye ambao miguu imepinda ndo mambo ya heshima mbele sana. Kwawale walio wahi kuomba kazi wanajuu hili swala na wale walioenda kuomba kuoa mtoyo wa mtu wanaelewa somo. Lakini hii isiwe kigezo cha kulaumu watu wengine kama mnavyomuona dogo umri bado anamengi ya kujifunza na yeye yupo kwenye mambo ya kimichezo na watu kwenye hiyo kazi wanatakiwa wawe relax sio wa kupaparika.